mimi nimeoa jirani sana na nyumbani kwetu. tangu nimeoa sijawahi kulala ukweni kwa sababu ni mwendo wa dakika tu kutoka kwetu hadi ukweni. rafiiki yangu anasema kuwa kitendo cha kutolala na mke wangu kwao ni kutomtendea haki kwani yeye analala kwetu. anasema ni vizuri kwa mahusiano kulala ukweni na mkeo eti inakuongezea heshima toka kwa wazazi wa mke wako! mimi kweli sielewi lakini mke wangu anasapoti. naombeni ushauri wenu.