Nahitaji ushauri wa watu wenu ndugu zangu wenye busara.
Ninaishi Canada kwenye nyumba ya serikali (HLM) pamoja na mke wangu na watoto wangu wawili. Baba yangu ana miaka 46. Nilimchukua aishi kwangu kwa sababu alikuwa ana maisha magumu, lakini tangu ameingia kwangu maisha yamekuwa magumu sana.
Tabia zake zimekuwa changamoto kubwa:
Ni muongo kupita kiasi, hasemagi ukweli hata nikimwomba nimsaidie kupata kazi.
Ni mvivu wa kazi, hajawahi kuendelea na kazi yoyote. Wiki 3 sasa hana kazi wala kipato.
Anadanganya kuwa anaenda kazini kumbe anazurura tu mitaani.
Ni mlalamikaji, mbishi, na anakasirika haraka.
Ni mbeya na ana historia ya kuleta migogoro ndani ya familia. Kwasababu ya uongo wake
ALimkataa mama yangu 2017 tena kwa talaka cha ajabu yeye ndo anateseka zaidi na wakati aliaminisha jamii kuwa mama yangu ndo mbaya
Ana tabia ya kutumia watu, akishapata mahali pa kula na kulala, anajisahau kabisa.
Anapenda kula sana, na gharama za chakula zimepanda sana. Zamani nilikuwa natumia $200–$300 kwa mwezi, sasa tunatumia $700+.
Hatoi chochote kwenye matumizi, mimi ndiye nabeba kila kitu.
Kwenye nyumba ya serikali (HLM) siruhusiwi kuishi na mtu mwingine yeyote ambaye hajatajwa kwenye mkataba. Hii inaniweka kwenye hatari ya kufukuzwa na kupoteza makazi yangu pamoja na familia yangu.
Ukweli mwingine mgumu ni kwamba baba yangu amezoea kufukuzwa kila mahali anapokwenda kwa sababu ya tabia zake. Akiachiwa aishi kwa watu, harudi tena kwao mpaka apate shida. Baridi ikianza ndipo anarudi kuomba msaada.
Nimejaribu kila njia za kumwonya, kumueleza, kumsaidia, kumuelekeza, lakini haelewi kabisa. Kila siku ni uongo, visingizio, lawama na kuonyesha ubabe. Ukimwambia jambo analalamika au kuchukia.
Sasa nimefika mwisho nataka kumfukuza ila kuna wakati huruma unanijaa moyoni tu
Ila Nina hofu kwa watoto wangu, mke wangu, ikiwa tutapoteza nyumba yetu kwa kuvunjiwa mkataba na serekali sisi ndo tutaangaika zaidi . Lakini pia ninajua huyu ni baba yangu mzazi, na akitoka kwangu atakuwa hana pa kwenda
Swali
Nifanye nini katika hali kama hii?
Nimfukuze kwangu kwa ajili ya usalama wa familia yangu, au niendelea kumvumilia huku familia yangu ikiteseka?
Naomba ushauri wenu