Wakuu, naomba ushauri wenu kwenye mradi wangu wa ufugaji wa kuku

Akhi

JF-Expert Member
Jul 12, 2021
2,835
4,607
Assalam alaykum,
Habari zenu wapendwa

Mimi ni mhitimu wa chuo, ni muaminifu sana kuliko UMUGHAKA uaminifu wake kwa Ally Mpemba.

Nilibahatika kupata ukarani katika Sensa ya mwaka 2022 namshukuru nikapata chochote kitu ila mimi mawazo yangu toka mwanzo nikafuge kuku mna nyenzo zipo za kutosha
Sasa toka nilivoanza mradi wa kufuga kuku nilianza na kuku 200 baadae nikawauza.

Alhamdulillahi nikapata kitu
Sasa mimi nikaendelea na ufugaji hivo hivo japo kipindi cha pili soko likawa gumu sio kama nilivotarajia lakini nashkuru likapita na nikauza kuku.

Sasa nikaweka vifaranga vingine 200 vya broiler ambavyo ndo ninavyo mpaka sasa nategemea baada ya wiki 2 wanaweza kua tayari kwa ajili ya Soko, Baada ya mafanikio ya kujituma huku kuna watu wakaona jitihada zangu leo hii watu wawili kwa nyakati tofauti wakanambia wanataka wawekeze kwenye mradi wangu ili tuje kugawana faida.

Je niwakubalie kwa ombi lao hilo?

Wasiwasi wangu ni kua ufugaji ni risk sanaa sasa siku nikija kuwaambia kuku wamefariki je watanielewa? Natamani ningepata mtu angenishika mkono kwa kunipa hela niukuze mradi halafu nimrudishie pesa yake ila hili la kufanya Partnership mimi naona sijaliafiki.

Ushauri wenu wakuu.
 
Sikushauri uwekeze na watu kuku ni kama kamari tu mda mwingine, mie ninafuga kuku wa kienyeji. Kuna mda kuku wanakufa tu huwelewi hata shida nini, pia unawapa chanjo ila hizi chanjo nazo kama ziko defaulted na hakuna anayefatilia. .

Broiler unatakiwa uhakikishe soko unalo kwa sababu wakifika siku ya kutoka na ukaendelea kuwafuga ujue wanakula vibaya na wanavyokula unapunguza faida. .

Mungu akufanyie wepesi kwenye ufugaji wako. .
 
Umesema Mara ya kwanza soko,lilikuwa shida na ukauza kwa shida kidogo,je unauhakika ukiongeza mtaji Hilo soko la kuuza Mara moja utalipata? Pia hao wanaotaka mfanye partner Mara nyingi wanakuwa ni watu ambao hawaijui biashara wengi wanaona njia rahisi ya kupata faida ni wao kuweka pesa na kupata gawio bila kusaidia chochote(Yani kuhudumia kuku,kutafuta soko) vp ukipata hasara watalibebaje? Kwa mim nitafanya hivyo endapo mtu ninaefanya nae biashara atakuwa na connection ya soko au atakuwa active partner 💯
 
Sikushauri uwekeze na watu kuku ni kama kamari tu mda mwingine, mie ninafuga kuku wa kienyeji. Kuna mda kuku wanakufa tu huwelewi hata shida nini, pia unawapa chanjo ila hizi chanjo nazo kama ziko defaulted na hakuna anayefatilia. .

Broiler unatakiwa uhakikishe soko unalo kwa sababu wakifika siku ya kutoka na ukaendelea kuwafuga ujue wanakula vibaya na wanavyokula unapunguza faida. .

Mungu akufanyie wepesi kwenye ufugaji wako. .
Yani ndo ninaloliona kuwekeza na mtu mimi sijaliafiki hilo jambo

Asante sana
 
Umesema Mara ya kwanza soko,lilikuwa shida na ukauza kwa shida kidogo,je unauhakika ukiongeza mtaji Hilo soko la kuuza Mara moja utalipata? Pia hao wanaotaka mfanye partner Mara nyingi wanakuwa ni watu ambao hawaijui biashara wengi wanaona njia rahisi ya kupata faida ni wao kuweka pesa na kupata gawio bila kusaidia chochote(Yani kuhudumia kuku,kutafuta soko) vp ukipata hasara watalibebaje? Kwa mim nitafanya hivyo endapo mtu ninaefanya nae biashara atakuwa na connection ya soko au atakuwa active partner
Hpna mara ya kwanza soko lilikua zuri tu ila mara ya pili ndo soko likawa gumu ila kwa sasa ivi soko lipo zuri mna saivi broiler ni wa kutafutwa watu waliogopa kuingia mzigoni baada ya kuona soko gumu kipindi cha nyuma apo

Saivi wateja wapo baada ya kujulikana kua na mimi ni mfugaji kwaio wateja wapo
Nina order mbili mpk sasa za kuku
 
kuku hawataki kuwa karibu na msongamano na makazi.
sababu ni rahsisi kupata magonjwa mfano panya,wanyama kama mbwa,mbuzi na ng'ombe.

hakikisha eneo uliopo ni mbali na makazi ya watu ufugaji.
usinunue kukuovyo hakikisha una mbegu yako unayozalisha hapo.

nunua mashine ya kuzalisha chakula na kichanganya ikiwezekana ili kuepuka magonjwa na chakula kisicho andaliwa sawa.

Hakikisha kuwa na josho la kujipulizia dawa kabla mjaingia bandani.
 
Dah kwa sisi wadogo hatuna uwezo wa mashine
 
Assalam alaykum,
Habari zenu wapendwa

Mimi ni mhitimu wa chuo, ni muaminifu sana kuliko UMUGHAKA uaminifu wake kwa Ally Mpemba.

Nilibahatika kupata ukarani katika Sensa ya mwaka 2022 namshukuru nikapata chochote kitu ila mimi mawazo yangu toka mwanzo nikafuge kuku mna nyenzo zipo za kutosha
Sasa toka nilivoanza mradi wa kufuga kuku nilianza na kuku 200 baadae nikawauza.

Alhamdulillahi nikapata kitu
Sasa mimi nikaendelea na ufugaji hivo hivo japo kipindi cha pili soko likawa gumu sio kama nilivotarajia lakini nashkuru likapita na nikauza kuku.

Sasa nikaweka vifaranga vingine 200 vya broiler ambavyo ndo ninavyo mpaka sasa nategemea baada ya wiki 2 wanaweza kua tayari kwa ajili ya Soko, Baada ya mafanikio ya kujituma huku kuna watu wakaona jitihada zangu leo hii watu wawili kwa nyakati tofauti wakanambia wanataka wawekeze kwenye mradi wangu ili tuje kugawana faida.

Je niwakubalie kwa ombi lao hilo?

Wasiwasi wangu ni kua ufugaji ni risk sanaa sasa siku nikija kuwaambia kuku wamefariki je watanielewa? Natamani ningepata mtu angenishika mkono kwa kunipa hela niukuze mradi halafu nimrudishie pesa yake ila hili la kufanya Partnership mimi naona sijaliafiki.

Ushauri wenu wakuu.

Kuna kitu kinaitwa MOU…
Hicho kinaelezea Dos and Donts…Ingieni huo mkataba
 
Back
Top Bottom