Naomba ushauri wana JF

Naomba ushauri wana JF

Eddy Bway

Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
5
Reaction score
0
kuna msichana mmoja she is my best friend, ila nimeanza kumpenda kutokana na tabia pamoja na uzuri wake ,tumefahamiana ni zaidi ya mwaka ,ila kumueleza hisia zangu kwake nimeshindwa kabisa ,nimeamua kuja kwenu wana jf nifanyeje?
 
Kwanza, kwa nini umeshindwa kumwelezea jinsi unavyojisikia juu yake? Ni kwamba wewe ni domo ulimbo na hujui uanzie wapi na uanze vipi, au hasa tatizo ni nini ?

Au unaogopa kupigwa kibuyu (baada ya kufunguka) na uwezekano wa kuharibika kwa urafiki wenu?

Na yeye kwa jinsi ulivyomsoma, mwelekeo wake unauonaje? Kakupa hata dalili njema zinazoashiria mafanikio?
 
Kwa ufupi wa maelezo yako huenda ndio unachipukia, vinginevyo fafanua ni kwa vipi unashindwa kuongea nae?
 
Funguka Mkuu umwambie ukweli kuhusu hisia zako kwake ila uwe tayari kujibu maswali kutoka kwake kama yatakuwepo.

kuna msichana mmoja she is my best friend, ila nimeanza kumpenda kutokana na tabia pamoja na uzuri wake ,tumefahamiana ni zaidi ya mwaka ,ila kumueleza hisia zangu kwake nimeshindwa kabisa ,nimeamua kuja kwenu wana jf nifanyeje?
 
Ongea nae mbona hakuna shida . Mweleze kilichoujaza moyo wako juu yake. Wanasema ukienda kuazima jamvi usianze kupiga hadithi eleza mapema shida yako aweza kuja mwingine nyuma yako mwenye hitaji kama lako halafu unabaki kumuambia mmiliki mimi pia nilikuja kuomba jamvi which is gonna be too late
 
  • Thanks
Reactions: BAK
kuna msichana mmoja she is my best friend, ila nimeanza kumpenda kutokana na tabia pamoja na uzuri wake ,tumefahamiana ni zaidi ya mwaka ,ila kumueleza hisia zangu kwake nimeshindwa kabisa ,nimeamua kuja kwenu wana jf nifanyeje?

mwambie coz u never know labda nae anakupenda
 
Huyu jamaa tatizo lake ni kwamba bado anasubiri matokeo yake remix toka kwa mulugo.
 
Mapenzi huharibu urafiki. Bora umpende mtu asie rafiki yako hata mkishindwana unatupa kuleeeeeeee! Yaani urafiki uje kwa ajili ya mapenzi. Mtizamo wangu lakini
 
kuna msichana mmoja she is my best friend, ila nimeanza kumpenda kutokana na tabia pamoja na uzuri wake ,tumefahamiana ni zaidi ya mwaka ,ila kumueleza hisia zangu kwake nimeshindwa kabisa ,nimeamua kuja kwenu wana jf nifanyeje?
unataka tuwe makuwadi wako??? Mimi siwezi kutumika maana sijajua kama nia yako ni ovu au njema
 
jipange nenda kaseme yako mapema kabla hujapokonywa tonge mdomon
 
kuna msichana mmoja she is my best friend, ila nimeanza kumpenda kutokana na tabia pamoja na uzuri wake ,tumefahamiana ni zaidi ya mwaka ,ila kumueleza hisia zangu kwake nimeshindwa kabisa ,nimeamua kuja kwenu wana jf nifanyeje?
Bway kwanza kuna mambo ambayo unatakiwa kujua kabla hujamtamkia,
1.Tangu muanze urafiki wenu amekwishawahi kukusifia kuwa u mfano bora wa mwanaume anayemtaka?
2.Yupo katika mahusiano na mtu mwingine?Kama ndio achana na wazo lako,ila kama hapana jaribu kumuuliza kama yupo katika mahusiano,hii itakufanya uwe huru kufanya uamuzi sahihi.
Kwa kuwa ni wewe pekee ndiye unayejua namna ambavyo urafiki wenu ulivyo na mnavyozungumza hivyo kama kweli unamtaka sidhani kusema ni jambo gumu ila epuka kufanya maombi kwa kutumia ujumbe wa simu.
 
Mueleze ukweli2 usiogope kujibiwa vibaya huenda nayeye anakupenda anasubiria uanze jitose kijana.
 
Mapenzi huharibu urafiki. Bora umpende mtu asie rafiki yako hata mkishindwana unatupa kuleeeeeeee! Yaani urafiki uje kwa ajili ya mapenzi. Mtizamo wangu lakini

I second you, ila urafiki baada ya kutengana unawezekana japo kwangu ni ngumu sana..
 
Funguka tu mueleze ya moyoni,ila uwe tayar kwa jibu lolote,na ikiwa NO usikasirike ama kumchukia ama kuvunja urafiki uwe normal tu.
 
Back
Top Bottom