NAOMBA USHAURI WAKUBWA,

Kipempe

Member
Sep 22, 2021
17
5
Wakubwa,
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 21, mhitimu wa kidato cha sita mwaka 2021,

Nilichaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dar Es salaam, katika shahada ya kwanza ya POLITICAL SCIENCE AND PUBLIC ADMINISTRATION, Ambayo ada yake ni Tsh 1.3 milion,

Kama mnavyojua maajabu ya mwaka huu wa bodi ya mikopo wamenilipia tsh 400500 tu, yaan kama 900k natakiwa kulipa mwenyewe,
Kiukweli hali ya famili sio nzuri sana kwa sasa,

Nilichokuwa nawaza atleast nisome course yenye ada ndogo, ya hapo Hata uwalimu japokuwa sio ndoto yangu kabisa, ambayo ada ni 1milion,

Naombeni ushauri ndugu zangu nifanyaje ???
 
Kama ni program ya ndoto yako unaweza kujinyima kwenye boom ukajazia ada.
 
Wakubwa,
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 21, mhitimu wa kidato cha sita mwaka 2021,

Nilichaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dar Es salaam, katika shahada ya kwanza ya POLITICAL SCIENCE AND PUBLIC ADMINISTRATION, Ambayo ada yake ni Tsh 1.3 milion,

Kama mnavyojua maajabu ya mwaka huu wa bodi ya mikopo wamenilipia tsh 400500 tu, yaan kama 900k natakiwa kulipa mwenyewe,
Kiukweli hali ya famili sio nzuri sana kwa sasa,

Nilichokuwa nawaza atleast nisome course yenye ada ndogo, ya hapo Hata uwalimu japokuwa sio ndoto yangu kabisa, ambayo ada ni 1milion,

Naombeni ushauri ndugu zangu nifanyaje ???
Umepata vipengele vingapi katika mkopo wako...!Ili tuweze kukushauri vzr
 
Unaenda kwa loan officer unaomba boom lako ndio lilipe ada

Shida ipo kwenye usajili ambapo wanataka nusu ya ada ya semister ilipwe, ambayo ni laki NNE na nusu, nikifanya utaratibu huo naweza kusajiliwa?? Yan ela nyingine ya usajili ikatwe kwenye boom
 
Kopeni hata kwa riba unalipia ada nusu halafu boom ikija unafeeel the gepu kikubwa usifate makundi na starehe utapotea
 
Shida ipo kwenye usajili ambapo wanataka nusu ya ada ya semister ilipwe, ambayo ni laki NNE na nusu, nikifanya utaratibu huo naweza kusajiliwa?? Yan ela nyingine ya usajili ikatwe kwenye boom
Hakuna kinachoshindikana. Usajili uko ndani ya mamlaka ya chuo, wakiamua hata usilipe wanaweza ni wao wenyewe. Ila hawataki usumbufu kabisa, mko maelfu ya watu wenye shida kama wewe. Hapo ni bahati yako na upambanaji. Ukifanikiwa kama una akili soma sana yani sana ukimaliza mwaka unadhaminiwa ada kwa matokeo. Wako watoto wa kishua wanasoma bure kwa ufaulu tu

Kuacha kozi kisa 300k kwa mwaka sio maamuzi sahihi
 
Nashukuru sana mkuu,
Kwenye suala la ufaulu unalipiw ada nimelisikia Mara kadhaa naomba ufaganuzi kidogo kama hutajali
 
Wakubwa,
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 21, mhitimu wa kidato cha sita mwaka 2021,

Nilichaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dar Es salaam, katika shahada ya kwanza ya POLITICAL SCIENCE AND PUBLIC ADMINISTRATION, Ambayo ada yake ni Tsh 1.3 milion,

Kama mnavyojua maajabu ya mwaka huu wa bodi ya mikopo wamenilipia tsh 400500 tu, yaan kama 900k natakiwa kulipa mwenyewe,
Kiukweli hali ya famili sio nzuri sana kwa sasa,

Nilichokuwa nawaza atleast nisome course yenye ada ndogo, ya hapo Hata uwalimu japokuwa sio ndoto yangu kabisa, ambayo ada ni 1milion,

Naombeni ushauri ndugu zangu nifanyaje ???

Nicheki WhatsApp +255753715912 Nikupe Maelekezo Full Na Mi Nipo Udsm Hapo PSPA kama ww.
 
Nashukuru sana mkuu,
Kwenye suala la ufaulu unalipiw ada nimelisikia Mara kadhaa naomba ufaganuzi kidogo kama hutajali
Huo ufafanuzi utakufaa ukishajiandikisha maana unategemea matokeo, na hufanyi mtihani bila kulipia ada. Ukishafika chuo ukakaa miezi michache utakuwa ushajua mwenyewe bila kuuliza
 
Wakubwa,
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 21, mhitimu wa kidato cha sita mwaka 2021,

Nilichaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dar Es salaam, katika shahada ya kwanza ya POLITICAL SCIENCE AND PUBLIC ADMINISTRATION, Ambayo ada yake ni Tsh 1.3 milion,

Kama mnavyojua maajabu ya mwaka huu wa bodi ya mikopo wamenilipia tsh 400500 tu, yaan kama 900k natakiwa kulipa mwenyewe,
Kiukweli hali ya famili sio nzuri sana kwa sasa,

Nilichokuwa nawaza atleast nisome course yenye ada ndogo, ya hapo Hata uwalimu japokuwa sio ndoto yangu kabisa, ambayo ada ni 1milion,

Naombeni ushauri ndugu zangu nifanyaje ???
Hayo mambo ya mkopo hayana umuhimu kwangu.. naomba nijibu haya maswali..

1. Unataka kusoma polical science ili badae iweje? Ujiajiri au uajiriwe?

2. Kama ni kujiajiri ujiajiri kwenye nini?

3. Kama ni kuajiriwa je ulisha wahi ona tangazo la kazi la hiyo kozi yako?

4. Ulisha wahi kuwa na malengo ya kusoma political science before?

5. Kama sio kwann leo unataka kuisoma ilihali hujawahi kuwa na malengo nayo?

NB: elimu ni uwekezaji, wa pesa na muda na hilo boom ni mkopo na utatakiwa kulipa siku moja. Naomba ya hayo maswali yangu ili nijue kama uwekezaji wako una tija au la.

NB2: Tafadhali jibu maswali yote bila kuruka hata moja.
 
  • Thanks
Reactions: 911

Sasa hapa unatoa ushauri au unafanya careers Guidance!

Anachokisoma ndio alichokichagua Sasa unataka kumtoa kwenye njia..

#Usitoe ushauri mpaka uombwe.
 
Yuko sahihi kwa akili zenye akili. Mara nyingi Injinia Upepo huwa anauliza mustakabali wa huyo msomi na degree inayoenda kutafutwa.

Mfano huyu hapa hana laki 9 ya kumalizia ada alafu anaenda kusoma political science. Kuna maelezo unataka tena kuelewa concern yake?
 
Sahihi.
 
Hayo mambo ya mkopo hayana umuhimu kwangu.. naomba nijibu haya maswali..

1. Unataka kusoma polical science ili badae iweje? Ujiajiri au uajiriwe?

2. Kama ni kujiajiri ujiajiri kwenye nini?

3. Kama ni kuajiriwa je ulisha wahi ona tangazo la kazi la hiyo kozi yako?

4. Ulisha wahi kuwa na malengo ya kusoma political science before?

5. Kama sio kwann leo unataka kuisoma ilihali hujawahi kuwa na malengo nayo?

NB: elimu ni uwekezaji, wa pesa na muda na hilo boom ni mkopo na utatakiwa kulipa siku moja. Naomba ya hayo maswali yangu ili nijue kama uwekezaji wako una tija au la.

NB2: Tafadhali jibu maswali yote bila kuruka hata moja.
Hakuna anayesomea kazi, Tunasoma fanii,
Hakuna watu wamesoma PSPA na wamefanya mambo mengine mbali na walichofundishwa??
Magufuli alikuwa mwalimu, alikuwa Rais wako, Zitto ni mwana uchumi Leo ni mwana siasa,
Anyway, ushauri nilioomba sio ulichokiandika hapa,
N.B ITS BETTER TO DO WHAT YOU LIKE MOSTLY
 
Yuko sahihi kwa akili zenye akili. Mara nyingi Injinia Upepo huwa anauliza mustakabali wa huyo msomi na degree inayoenda kutafutwa.

Mfano huyu hapa hana laki 9 ya kumalizia ada alafu anaenda kusoma political science. Kuna maelezo unataka tena kuelewa concern yake?
Hana cha maana alichoandika,
Maswali aliyoyauliza hayana maana yoyote kama unafahamu nini maana ya elimu na lengo la elimu,
 
Mojawapo ya malengo ya elimu ni kuongeza ufahamu na kuondoa ujinga. Hayo malengo ni ya watoto wa wanaojiweza, kuna Wahindi nimekuta wamesomea udaktari kwa kupenda na wamefaulu vizuri sana ila hawajawahi kuingia hospitali kufanya kazi bali wameendeleza biashara za familia. Sasa sisi wa mazingira duni hatusomi tu from nowhere eti kuongeza ufahamu. Hatukopi millions of money ambayo ukicheza utalipa miaka na miaka just for the sake of kuongeza ufahamu

Hapo huna laki 9 kwa mwaka alafu unajifunika kwenye lengo la elimu. Hiyo fani ya political science kina Kibajaj, Babu Tale na Musukuma wameivamia bila kusomea. Ila huyo Magufuli uliyemsema alikuwa na kazi ndio akaonekana, alafu yeye ni kiongozi wala si lazima asome siasa. Tafuta idadi ya wanasiasa wenye political science alafu tafuta watu wenye political science kwenye fani nyingine

Njoo chuo uone hata uongozi wa wanafunzi hakuna hao political science. Ili uwe mwanasiasa bongo inabidi ujue kusoma na kuandika, vigezo vyepesi kuliko udereva

Haya yote tunasema sio kukutisha. Je una option nyingine endapo utakosa kuwa mteule? Kama unajiamini sana katika hilo then nenda bila kusita
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom