Naomba ushauri wa namna ya kumkwepa huyu binti

Watu mna bahati hambahatiki !kama ana respect na anakujali alafu unamwacha!!! ingekuwa inawezekana ungenipasia nibak nae, nishaangaika sana sijaona mwenye respect wala kujali naambulia tu ma changudoa.
 
Ikiwa bado huja muweka Ndani unamuona sio wa hadhi yako(Humpendi), sasa je utaweza kumpenda kweli Ndani ya Ndoa ambapo sura na figure hubaki suala la kawaida tu kwa wanandoa.?

Niheri umwambie ukweli, japo ataumia sana kwa mda mfupi kisha atasahau, kuliko kuja kuishi maisha Marefu ya Ndoa na mtu asiye mpenda, usije mpa stress mtoto wa watu kwa Michepuko utakayokuwa unatoka nayo ambayo ni Hadhi yako.

Ikiwa binti hana mimba wala mtoto wako hapo hakuna cha kumuonea huruma, Kwani bado ananafasi kubwa ya kupata mchumba.

NB. KUMUACHA MCHUMBA WAKO KIPINDI CHA UCHUMBA SIO DHAMBI KABISA,

KWANI UCHUMBA NIKIPINDI CHA KUFAHAMU YALE ULIPASWA KUFAHAMU KWA MCHUMBA WAKO KABLA YA NDOA ILI USIJE JUTA KWA KUSEMA NINGALIJUA WAKATI ULIKUWA NA MDA WA KUJUA.

IlA DHAMBI NI KUMUACHA MKE AU MME WAKO.
 
Umefanya kosa kubwa sana kumdanganya na kumpotezea muda. Ila kumuoa binti usiye na mapenzi naye nayo sio sawa, maana maisha yenu yatakuwa majanga mwanzo mwisho. Ukimtosa kienyeji, huo ukatili utakurudia na maisha yako yatakuwa ni hasara kubwa. Salama yako muombe msamaha na umuahidi na kutekeleza kumjengea/kumnunulia nyumba, kumuendeleza kielimu au kumfungulia biashara.
 
Jamani,mapenzi hayalazimishwi,sasa mtu kama namuona hanifai tena,ya nini kuendelea kumdanganya?
 
Haikuhitaji akili kubwa kugundua matatizo ya akili ya vijana wa nyakati hizi.....na hii inatokana na kuwa watumwa wa matamanio ya viungo vyao vya siri kiasi wameacha kabisa kutumia akili zao kabisa........
Ni mwanamke gani atajivunia kuwa na mwanamume wa aina hii ambaye anashindwa kuyaongoza maisha yake na badala yake anaongozwa na hisia za ngono......

Watu kama hawa hawa ndio wanaokuja kutunga nyuzi kamwe hawatakuja kuoa single mama kana kwamba hao singo mama wameteremshwa au hizo mimba walijipa wenyewe........

Kama shida yako ni huduma ya ngono tu kwanini usiende kwa wanaojiuza ili ukakidhi haja za mwili wako.........

Ndio maana mabinti wa siku hizi hawaoni umuhimu wa kuolewa ikiwa waoaji wenyewe ndio kama huyu mtoa mada.....maana ni vigumu kumjua mkweli ni na muongo ni yupi maana wote wanakuja katika sura za tabasamu na sura zenye bashasha.......

Ukitaka kujua madhara au machungu ya hichi unachokifanya jaribu kuvaa uhusika wa huyo binti.....ni tukio lenye kuchoma moyo kama sio kuumiza moyo.........

What goes around ,comes back around........hichi unachotaka kukifanya kitakuja kukurudia kwenye maisha yako katika namna ambayo hata wewe hutakuja kuelewa lakini machugu yake yatakuwa ni makali kuliko hata haya unayotaka kumsababishia huyo binti.......
 
Bwana yesu asifiwe enyi watu wa Mungu!
Wakuu,kuna binti nilimuahidi kuwa nitamuoa pindi atakapomaliza chuo,anamaliza chuo mwezi huu 7,nilimpa hii ahadi hewa ili niliendelee kumtafuna kisela tu,kiukwel binti wa watu kanionyesha respect na kunijali kipindi chote hiki alichokua masomoni.lakini me sina hata chembe ya mapenz ya dhati kwake na naona sio wa hadhi yangu,sasa cku za hivi karibuni ndio naona mapenzi yake kwangu yameongezeka x2 zaidi ya mwanzo,na anaonekana bado anaikumbuka ile ahadi ya kuoana nilyompa miaka mitatu iliyopita wkt ndio anaenda kuanza chuo maana kama leo kaniambia eti kaota kuwa amekua officially mke wangu maana kaota tuko kanisan tunafunga ndoa.sasa wakuu,mie nataka nimuache huyo manzi solemba kwenye mataa,kwa kifupi nataka kuingia mitini.nitumie njia gani kumkwepa wakuu?
NB:kama huna cha kuchangia,pita kimya kimya tu ili tusikwazane.

nasemaga wanaume kama hawa walaaniwe...binti wa watu kajiheshimu kwa ajili yako akijua wew ni baba bora wa baadae kumbe ni kingasti....kaka ukimuacha huyu dada utakuja kujutia maishani mwako..ipo siku utakutana na kiboko yako utampenda wew yeye hakupendi atakufanyia visa ,,,utamkumbuka huyu uliemuona anafaa kugegeda lakini kwa ndoa hafai...

nasema ipo siku wanaume wataumizwa mioyo yao waitazame mbingu iwe ardhi na wwawatafute mabinti waliowaumiza moyo wawatulize muda huo utakuwa umechelewa kaka....wanaume ipo siku yenu mtaumizwa moyo kama mnavyotuumiza sisi...ipo siku nasema mtatukumbuka ila mtakuwa mmechelewa...
 
bora tu umuache akapate anayempenda! maana una roho ya chatu anakumeza na miguu yako. miaka 3 daahh nimeumia kama ndo mimi
 
Miaka yote unamnaniliu mdada wa watu hukujua kama sio wa hadhi yako saivi ndo unakumbuka hilo hangaika tu utakutana na unachokitafuta.
 
KikulachoChako ,sijaomba uniandikie risala,me nimeomba ushauri.

Hapo ndipo penye mzizi wa tatizo lako na bahati mbaya hutaki kulishughulikia tatizo na badala yake unatoana jasho na matokeo ya matatizo yako........

Ngoja nikuambie jambo moja la msingi sana....ingawa sikufahamu lakini ni dhahiri kutokana na maandiko yako wewe ni kijana mdogo ....na bado una malengo makubwa uliyojiwekea kwenye harakati za maisha yako.....
Kwa namna moja au nyingine ili uweze kuyafikia malengo yako unahitaji mazingira mazuri kuanzia kiafya na kiakili......lakini haya yote yanategemea sana na uhusiano wako na jamii iliyokuzinguka.........

Hili jambo unalotaka kulifanya ambalo wewe unaliona dogo na kulichukulia la kawaida lakini linaweza kukuletea matatizo makubwa kwenye maisha yako.....kumbuka unacheza na hisia kali za mapenzi kwa binadamu mwenzio ambazo maumivu yake yanaweza kuamsha hisia kali za visasi na kukomoana........kupitia hasira na visasi huwezi jua huyo binti ataamua kukuchukulia hatua gani ukizingatia kuwa umempotezea muda wake mwingi kwa ahadi zako hewa.......

Kwa usalama wako na kujiweka mbali na laana za mateso ya huyo msichana unatakiwa utumie hekima na busara za hali ya juu kumalizana na huyo binti....otherwise majuto ni mjukuu........


Samahani kwa maelezo yangu marefu......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom