Kwanza hongera kwa wazo la kujenga.
Nianze kwa kusema hivyo viwanja vizuri ghali kama unavyosema vingi vipo pempezoni mwa mji na unaweza kukipata.
Cha kwanza nikushauri kamwe usinunue na kujenga sehemu ambayo hujapapenda sababu tu kukosa pesa ya kiwanja sehemu unayoipenda(ni bora kutafuta namna nzuri kuhifadhi pesa yako uiongeze kiasi cha kutosha kuweza kununua sehemu uipendayo), hii itakusaidia kuwa comfortable na makazi yako ya kudumu.Pia maeneo ambayo unaweza kuyaona sio mazuri kwa sasa pembezoni mwa mji miaka michache ijayo inaweza ukapashangaa na usiamini jinsi patakavyokiwa pazuri(so kiwanja kiwa pembezoni mwa mji isikutishe).
mfano miaka michache iliyopita nilinunua eneo pembezoni mwa mji wakati huo wengine walikuwa wakija kupaona wanaondoka na kusema huku bado sana(kulikuwa hakuna umeme,maji ,nyumba ni chache,barabara mbovu i.e usafiri shida l...lakini sasa ni sehemu nzuri sana inayotamaniwa na wengi.
Tatu;ukiamua kununua kiwanja na kujenga nakushauri usijibana sana eneo...ni bora ukasubiri uongeze pesa ununue eneo la kujidai mambo ya kujenga pembezoni mwa mji unapata nafasi ya kujenga na parking tu kwangu mimi sio sawa.
Ukinunua eneo la kuishi wewe hakikisha unapata eneo la kujenga,parking,bustani,e.tc