Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 9,299
- 27,767
Miaka ya 2005-2008 nilikuwa napita sana barabara ya Goba-Makongo Juu hadi Chuo. Kipindi hicho lile daraja la Goba kwenda Makongo Juu halijajengwa.
Plus ujana ulikuwa bado mwingi nikapuuzia tu eneo hilo. Itoshe tu kusema yalikuwa mapori, viwanja hata kuanzia 1mln kushuka chini ulikuwa unapata vikubwa tu. Goba kalikuwa kakijiji leo nikipita huwa naumia sana.
Ni kweli hata leo unaweza kupata maeneo hapo Goba lakini kwa gharama kubwa sana. Eneo ambalo hasa nyumba zilikuwa zimejengwa ni Makongo juu na wengi inaonekana walipachukulia poa sana Goba ila baada ya barabara ya lami tu kupita na madaraja kujengwa daaah maeneo yakawa hayashikiki.
Kuanzia miaka ya 2010s nilipoanza ujenzi Salasala nikawa napitapita sana njia ya Madale kukiwa pori kipindi hicho barabara ya vumbi wakati wa masika hupiti na gari hilo tope. Hapo ndipo nikasema sifanyi tena makosa ya Goba, nikajichanganya na madalali na wenyeji nikapata viwanja vikubwa hapo Madale kukiwa bado pori.
Sasa hivi lami imepita Madale, leo ukifika Madale viwanja vimepanda bei sana na inaenda kuwa kama Goba. Ukweli ni kwamba mpaka leo sijaheal kwa yaliyonikuta Goba.
Hapo Dar na Pwani usiseme sehemu mbali, mbali kutokea wapi? Na sio tu Dar na Pwani popote pale nunua ardhi ili mradi inafaa kwa makazi au kilimo.
Usiseme hakujachangamka nunua tu, wewe ni miongoni mwa watakaopachangamsha. Twenzetu Mabwepande.