MR KUO
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 2,397
- 3,248
Wakuu mniwie radhi kwa uandishi mbovu,
Mwaka 2013 huko nilinunua viwanja vitatu, kimoja karibu na mji viwili nje kidogo ya mji,..kwenye hiki kiwanja Cha karibu nikajenga nyumba na ikafika wenye lenta nikashindwa kuimaliza kutokana na ghalama za uezekaji kuwa kubwa nikaiacha hivyo hivyo mpaka mwishoni mwa mwaka Juzi 2019 mwezi wa nane nikaoa ndoa ya kanisani kabisa na kwa Sasa ndoa Ina mwaka na kitu hivi huku tuna mtoto wa miezi nane.
Sasa kule kwenye kiwanja nilichojenga nyumba ilibaki nafasi kubwa baada ya kuoa nikaona nijenge nyumba ndogo vyumba vitatu ili tukae tuachane na kero za kupanga,ujenzi ukaanza na Sasa iko hatua ya kuezeka na bati nilipewa Kama zawadi na wanakamati wa harusi yangu, kimbembe kimekuja wakati huu ndani ya ndoa kumeibuka mgogoro unaohatarisha kuisambalatishia mbali ndoa hii.
najiuliza endapo tutaachana italazimu kumgawia Mali zangu hizi nilizochuma mwenyewe?
Au Kuna namna nyingine ya kufanya?
Msaada tafadhari.
Nje ya muda, hii migogoro ya ndoa za siku hizi nahisi Kuna shetani ndani yake na kumshinda imekuwa mtihani mgumu kweli kweli.