Naomba msaada wa kisheria kwenye jambo hili

Free Again

Senior Member
Dec 20, 2015
114
93
Habari za majukumu wanajukwaa!

Kwa mara ya kwanza natua kwenye jukwaa hili jukwaa,nikiwa na shida ya ushauri kutoka kwenu!

Niende moja kwa moja kwenye suala lenyewe.

Kuna jamaa mmoja tulifahamiana 2019. Mimi nikiwa na genge,yeye akiwa anachota maji ziwani kisha anayauza mtaani kwa mia mbili.

Na mara nyingi nilikuwa namtuma aende standi,akanibebee mzigo nilioagiza mjini kwa ajili ya kuuza gengeni.

2020, hali ya pale tulipokuwa ilibadilika sana kwasababu tulikuwa tunategemea samaki kwenye mzunguko wa uchumi, lakini samaki zilikuwa hazipatikani yaani ziliadimika sana.

Watu wengi walihama Maana hakuna mzunguko wa fedha.

Mwenzangu hali ilikuwa mbaya ZAIDI kwasababu watu walikuwa wachache na hawanunui maji wanaenda kuchota wenyewe kulingana na uchumi.

Kwangu kulikuwa na afadhali kidogo japo na mimi mauzo yalipungua sana ila nilikuwa sikosi hela ya kula, lakini mwenzangu alikuwa anakosa mara nyingine anashinda njaa.

Kipindi hicho nilikuwa sijaoa kwa hiyo nilimwambia awe anakuja tunapika tunakula,ukiwa hivyo, mpaka ambapo niliamua kukodi pikpik na kuenda kusavei eneo lingine la biashara.

Tulienda naye na tukapata sehemu nyingine iliyokuwa imechangamka kwa biashara. Basi nikakodi toyo nikapakia mizigo yote nikahamia kule.

Niliamua kwenda naye Maana hakuwa na mbele wala nyuma. Tukafika kule mimi niliendeleza biashara ya genge kama kawaida,yeye aliendelea kuuza maji.

Kuna kipindi alifiwa na mama yake mzazi,ikabidi aondoke kwenda Musoma,lakini hakuwa na nauli. Akaniambia pesa anayopata huishia kula na kutumia familia nyumbani.

Ikabidi nimpe laki moja,kwa ajili ya nauli na nilimwambia akirudi tutasaidiana kukabilia na changamoto ya uchumi.

Sio kwamba nilikuwa na kipato kikubwa ila nilikuwa na afadhali na niliona huruma kuona mtu anashindwa kwenda kumzika mama yake kwasababu ya ukata wa fedha. Na alisema hana ndugu yeye ndo wanamtegemea.

Aliporudi niliamua kumfungulia kibanda cha mpesa mahali ambapo niliona kuna mzunguko na hakukuwa na huduma hiyo.

Wakati nakabidhi line na pesa hatukuandikishana. Hesebu zake zilikuwa vizuri na hakukuwa na alikuwa mwaminifu na alikuwa anatolea hesebu hadi mia aliyotumia.

Kwasababu commission zilikuwa vizuri, nilimwambia achukue laki mbili aweke genge. Pesa ya faida ya genge ndo utakuwa mshahara wake.

Mambo yalikuwa yanaenda vizuri nami kiroho safi sikuwa na ajizi ILA nilimwambia mtaji na commission asiguse yaani asichukue.

Tulikuwa tunapiga hesebu kila mwisho wa mwezi na hesabu zilikuwa vizuri.

Mwezi wa nane mwaka jana nilisafiri nikaenda mbeya takribani miez mitatu nikawa huko,tulikuwa tunawasiliana kwa simu vizuri tu ila kwa miezi hiyo hatukupiga hesabu.

Kuna siku nilipiga simu akawa hapatikani,nilishangaa kwasababu sio kawaida na tulikuwa hatujawasiliana karibia wiki na zaid.

Nakaamua kumpigia simu jiran yake, jiran yake akasema mbona huyu alishaondoka hapa saiv ni wiki moja. Nilipomuuliza kuwa kaenda wapi alisema ameenda singida.

Niliendelea kumtafuta nikampata,nilipomuuliza uko wapi akasema singida na eneo akataja. Nikamuuliza kwanin umeondoka bila ruhusa yangu na bila taarifa? Akasema pale aliona hali ni mbaya hivyo alijiongeza. Nikamwambia anitumie line zote zikiwa na mtaji wote lakini hakutuma akawa ananizungusha kwa miezi miwili hadi nikaamua kumfuata huko huko.

Nikamfuata nikamkuta,alishituka sana Maana nilienda bila taarifa, nilimwambia nimefuata line tu,akanipatia lakini hazikuwa na kitu yaani hazina pesa na ZAIDI amekopa lakini saba na NUSU KWENYE huduma ya wezesha ya voda inayompa wakala fursa ya kukopa.

Kwa hiyo mtaji uliokuwa umefikia million 2 haukuwemo na zaid kulikuwa na deni. Nilimwambia ndani ya wiki awe amerudisha pesa zote,kisha nikaenda kufungua kesi kule tulipokuwa tunakaa.

Sasa naomba ushauri kwenu hio kesi ikifika mahakamani itakuwaje? Kwa sababu hakuna tulipo andikishana. Je anaweza kukana kuwa sijawahi kumpa fedha na sio yeye aliyekopa?

Alafu je RB inatolewa popote au kule tu ulikofungulia kesi Maana polis waliniambia nirudi nikachukue RB Kule nilikofungulia kesi.

Wadau hii kesi ikoje kwa upande wangu, nawezaje nikarudisha stahiki zangu hizi? Naombeni mnisaidie!
 
Kwanza maelezo Yako yakikaa ivo bila kubadirika kutakua hakuna kesi. Kwasababu kumpa mtu kazi na mshahara wake eti ataupata kwenye faida ya biashara huo ni utapeli. Faida ya genge aitumie kujilisha na kujivisha na malipo ya mwezi! Ulizingua.

Chakufanya inatakiwa uyakane maelezo Yako mwenyewe na utengeneze mengine. Maelezo yawe Hivi. Mtuhumiwa alikua ni mfanyakazi wako ambae alikua akifanya kazi ya uwakala na genge Kwa muda wa miaka miwili. Namalipo yake Kwa mwezi yalikua laki Moja na nusu na ulikua ukimlipa Kwa wakati.

Mtaji wa biashara na m pesa ulikua na kufikia milioni mbili na laki 5. kwamaana ya mtaji wa genge laki 5 na m pesa milioni mbili. Mwaka Jana ukipata safari ya ghafla kutokana na matatizo ya kifamilia na ulimuachia mtaji auendeleze. Safari hiyo ulikaa miezi mitatu na ulichomuambia au kuruhusu ni kuwa achukue mshahara wake tu Kwa Kila mwezi na Hela ya kula elfu 30 Kwa Kila mwezi maana katika kazi yenu unamlipa 150 na chakula Cha mchana juu Yako.

Kwa trend ya kamisheni za Kila mwezi ilikadiriwa angeingiza milioni 1.1 ( laki 3.5 Kwa mwezi) Kama na angetoa mshahara na matumizi basi kamisheni tu ungekua na laki 4+ hivyo pesa ambayo ungeikuta ni million 2.5 pamoja na genge likiwa hai.

Hivyo huyo mfanyakazi wako aliuza bidhaa za genge na kukimbia na mtaji wote hivyo wewe unadai pesa taslimu milioni 2.9 alizokimbia nazo. Ukijumlisha na deni alilokopa laki 7 basi Kuna 3.6milioni.

Kesi iwe ya wizi. Kama anauwezo wa kukulipa mkomalie ila Kama Hana mtie adabu.

Akikana kuwa ulikua humlipi basi atakua amekubali kuwa alikua mfanyakazi wako.

Mashahidi, ni majirani zenu kibiashara wawili tu.
 
Ndugu yangu Vitalis Msungwite ,nakushukuru sana tena sana. Niseme tu Mungu akubariki. Umenisaidia sana
 
Nyongeza ya kutafuta ushahidi kuwa unamdai:

Mpigie simu ukiwa umeweka kwenye recording mode alafu muulize au jadilianeni namna atakavyokulipa, ongea nae kirafiki naye atafunguka kwamba pesa yako atakulipa tu. Tunza hiyo voice record itakuwa ushahidi hapo baadae.
 
Back
Top Bottom