Naomba ushauri wa kisheria katika jambo hili

MR KUO

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
1,513
2,000
Wakuu mniwie radhi kwa uandishi mbovu,

Mwaka 2013 huko nilinunua viwanja vitatu, kimoja karibu na mji viwili nje kidogo ya mji,..kwenye hiki kiwanja Cha karibu nikajenga nyumba na ikafika wenye lenta nikashindwa kuimaliza kutokana na ghalama za uezekaji kuwa kubwa nikaiacha hivyo hivyo mpaka mwishoni mwa mwaka Juzi 2019 mwezi wa nane nikaoa ndoa ya kanisani kabisa na kwa Sasa ndoa Ina mwaka na kitu hivi huku tuna mtoto wa miezi nane.

Sasa kule kwenye kiwanja nilichojenga nyumba ilibaki nafasi kubwa baada ya kuoa nikaona nijenge nyumba ndogo vyumba vitatu ili tukae tuachane na kero za kupanga,ujenzi ukaanza na Sasa iko hatua ya kuezeka na bati nilipewa Kama zawadi na wanakamati wa harusi yangu, kimbembe kimekuja wakati huu ndani ya ndoa kumeibuka mgogoro unaohatarisha kuisambalatishia mbali ndoa hii.

najiuliza endapo tutaachana italazimu kumgawia Mali zangu hizi nilizochuma mwenyewe?

Au Kuna namna nyingine ya kufanya?

Msaada tafadhari.

Nje ya muda, hii migogoro ya ndoa za siku hizi nahisi Kuna shetani ndani yake na kumshinda imekuwa mtihani mgumu kweli kweli.
 

Vitalis Msungwite

Verified Member
May 11, 2014
2,188
2,000
Nyumba mliyojenga na mali mlizotafuta pamoja zitathaminishwa na kugawanywa. Kutokana na mama kuwa na mtoto mdogo utatakiwa kumuachia nyumba ili asipate taabu na mtoto. Kwahiyo hukumu sheria itagawa lakini atakaebaki na mtoto ndio atapewa kipaumbele.
 

MR KUO

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
1,513
2,000
Nyumba mliyojenga na mali mlizotafuta pamoja zitathaminishwa na kugawanywa. Kutokana na mama kuwa na mtoto mdogo utatakiwa kumuachia nyumba ili asipate taabu na mtoto. Kwahiyo hukumu sheria itagawa lakini atakaebaki na mtoto ndio atapewa kipaumbele.
Hiyo nyumba haijaisha kabisa na iko kwenye kiwanja kimoja.
 

Lob

JF-Expert Member
Jul 24, 2017
491
1,000
Pole sana hili ni tatizo Kubwa sana kwa Wanaume, Kimsingi sheria inasema vitu vilivyopatikana ndani ya ndoa ni Vya wanandoa, ila kwenye kugawana itaangaliwa nani alichangia zaidi. hivyo hio nyumba wanaweza sena aslimia tano au kumi iende kwa mke.
La sivyo uende kwa mwanasheria uandike ni ya Mtoto ila lazima mahakamani watasema akae hapo na mtoto.

Mwanaume ukioa ujue umebeba msalaba kwani sheria na jamii inambeba mwanamke,
Suluhisho ni kuzaa nao, tunza Mtoto akiwa Mkubwa chukua, lakini usiishe naye ni shida, Wanaume Wengi wanakua masikini kwa sababu ya wanawake, utakuta kijana anajitahidi na Anakua na maendeleo akishaona matatizo yanaanza na mwisho wa siku anakufa mapema na anaacha mali alizozihangaikia.
 

Vitalis Msungwite

Verified Member
May 11, 2014
2,188
2,000
Hiyo nyumba haijaisha kabisa na iko kwenye kiwanja kimoja.
Utalazimishwa na mahakama uikamilishe kwaajili ya mama na mtoto. Kama huna uwezo itathaminishwa ikiwa ivo ivo na kugawanya thamani yake na mmoja wenu atamfidia mwenzake ili abaki na nyumba.
 

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
14,232
2,000
Yaani ndoa inaonyesha hata miezi sita bado......duuh changamoto,kama hata bati ni zawadi ya harusi........
 

MR KUO

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
1,513
2,000
Pole sana hili ni tatizo Kubwa sana kwa Wanaume, Kimsingi sheria inasema vitu vilivyopatikana ndani ya ndoa ni Vya wanandoa, ila kwenye kugawana itaangaliwa nani alichangia zaidi. hivyo hio nyumba wanaweza sena aslimia tano au kumi iende kwa mke...
Hii Ni kweli mkuu yanaenda kunikuta ndo nikaomba msaada hapa maana nimehustle mno mnoooo kaa jasho kubwa halafu vitu viende kilahisi hivi?

Kama Ni Mali nyingine Niko radhi kumpa zote ila sio hivi viwanja na nyumba noo.
 

Lob

JF-Expert Member
Jul 24, 2017
491
1,000
Hii Ni kweli mkuu yanaenda kunikuta ndo nikaomba msaada hapa maana nimehustle mno mnoooo kaa jasho kubwa halafu vitu viende kilahisi hivi?

Kama Ni Mali nyingine Niko radhi kumpa zote ila sio hivi viwanja na nyumba noo.
Unachoweza kufanya ni kuhama kwenye hio nyumba mliyopangisha kwa sasa, kwani sheria inasema mkitengana kwa Miaka 2 inaruhusiwa kuomba talaka. ila muone Mwanasheria mwanaume mwenye uzoefu kwa ushauri zaidi. ila kwa kuanza ni kuondoka hapo na kupanga nyumba nyingine.
 

B'REAL

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
4,098
2,000
Ndoa changa hamna hata miaka miwili mnaamua kutalakiana,kaeni chini mmalize tofauti zenu mlee mtoto wenu
 

chapangombe

Member
Sep 28, 2014
66
125
Kwanza issue ya kugawana Mali mahakani inakuja kutokana na uchangiaji was wote katika familia na mahakama Wana utaratibu wa kugawa kwa pacentage pia Kama mwanamke huyo alikuta kiwanja na ujenzi wa hiyo nyumba na kuna vitu ali changia kukamilisha aki prove mahakamani atapewa let say 30percentage au 20percentage
 

GODZILLA

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
5,722
2,000
Si nasikia siku hizi sheria ni kwa Kiswahili, vipi wewe bado hujapata madodoso na nakala husika?

Nilitegemea uwe mjuzi wa sheria za Kiswahili?
 

MR KUO

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
1,513
2,000
Si nasikia siku hizi sheria ni kwa Kiswahili, vipi wewe bado hujapata madodoso na nakala husika?

Nilitegemea uwe mjuzi wa sheria za Kiswahili?
Brother sio kila mtu anajua kila kitu,istoshe Niko frustrated vibaya mno huo muda wa kutafuta madodoso na kuyaelewa kwa Sasa nautoa wapi?

Ila kwa ushauri wa wadau hapa nimepata matumaini kabisa hofu imepungua na kumbe sijafika kwenye hatari kubwa.nitajaribu kuongea nae kwa Mara ya mwisho asipoelewa sitakuwa na jinsi zaidi ya kukubali matokeo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom