Naomba ushauri wa jinsi ya kumpa dawa mtoto

JimCarrey

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
214
124
Wadau leo limenikuta jambo ambalo limenifanya nijute kumpa dawa mwanangu.... Mtoto anasumbuliwa na mafua tukampeleka hospital amepewa dawa Kama 3 Coldril, Amoxillin na panadol zote za maji.

Kutokana na uwoga wa dawa na kulia sana wakati anapopewa dawa mama ake huwa anashindwa kabisa kumpa dawa maana huwa ni vurugu mtindo mmoja plus huruma za wanawake ndo kabisaaa.

Kitendo ambacho huwa kinanifanya niingilie Kati zoezi hilo..... Sasa leo asubuhi nimempakata mtoto vizuri nikampa dawa ya kwanza kwa nguvu Kama ilivyokawaida matokeo yake ile dawa ilimpalia na ikakaa kwenye koo Kama sekinde10 mtoto akawa ahemi ametoa macho na mdomo tu.

Nilichanganyikiwa sana na zoezi likaishia hapohapo.

Naombeni ushauri huenda nakosea namba ya kumpa dawa.
NB: Mtoto anamiezi6
 
Duhhh pole sana,vipi mtoto anaendeleaje sasa?...... kabla ya kushauri ni vizuri kujua ni namna gani huwa unampa kwa nguvu,huwa unafanyaje ? Matendo gani hufanya?
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Anaendelea vzuri dada..... Hua namlaza juu ya mkono wangu wa kushoto huku mkono wake wa kulia naupitisha katikati ya mkono wangu wa kushoto na mwili wangu( kwenye kwapa kwa chini kidogo) halafu ule mkono wake wa kushoto naushikilia na mkono wangu wa kushoto kisha namnywesha dawa kwa kutumia mkono wangu wa kulia.... Nafanya hivyo maana ni mbishi na anafujo sana wakati wa dawa
 
Mungu mwema kama anaendelea vizuri, sasa unapokuwa unamnywesha mtoto mbishi kama huyo usisahau na kumziba pua pale unapoingiza dawa mdomoni namaanisha tayari umeshaweka mdomoni zibane pua zake kwa vidole vyako, ni kitendo cha sekunde tu hii hufanya dawa kuingia moja kwa moja kwenye njia yake bila kuingia kwenye njia ya hewa, na njia hii huzuia mtoto kupaliwa, pia kitendo cha kuminya pua zake lazima kitamstua na hatapenda lazima Ile dawa ataimeza moja kwa moja.

Pia jitahidi kumfanyia michezo mbalimbali ya kumfurahisha ambapo unaweza kumpa dawa hata bila ya kutumia nguvu,michezo hiyo husaidia kumsahaulisha habari za dawa,pia kny michezo hiyo na wewe unaweza kutest kuonyesha unakunywa hiyo dawa na ni kitu kitamu siyo cha kumtisha ,kwa kufanya hivyo ataanza kuzipenda dawa, na uzuri dawa nyingi za kitoto ni Tamu tamu, ongea naye maneno matamu wakati unampa dawa watoto wanasikia hata kama ni mchanga wee jiongeleshe tu., kila la Heri kwenye malezi Bora,na Hongera kwa kuwa baba anayejali.
 
nashukuru kwa ushauri mzuri dada nitaujaribu mapema kesho.... Thanx for the compliment
 
Dawa ya maji imekaaje kooni sekunde 10 mkuu?

Limpalia mtoto akawa amekosa pumza kwa muda mkuu.... Alikua ameachia mdomo na macho yamemtoka..... Hujawahi kupaliwa hata na maji yakakukaba kaka...????? Isitoshe dawa za maji zinauzito fulani mithili ya asali that's makes it even more worse
 
Mungu mwema kama anaendelea vizuri, sasa unapokuwa unamnywesha mtoto mbishi kama huyo usisahau na kumziba pua pale unapoingiza dawa mdomoni namaanisha tayari umeshaweka mdomoni zibane pua zake kwa vidole vyako, ni kitendo cha sekunde tu hii hufanya dawa kuingia moja kwa moja kwenye njia yake bila kuingia kwenye njia ya hewa, na njia hii huzuia mtoto kupaliwa, pia kitendo cha kuminya pua zake lazima kitamstua na hatapenda lazima Ile dawa ataimeza moja kwa moja.

Pia jitahidi kumfanyia michezo mbalimbali ya kumfurahisha ambapo unaweza kumpa dawa hata bila ya kutumia nguvu,michezo hiyo husaidia kumsahaulisha habari za dawa,pia kny michezo hiyo na wewe unaweza kutest kuonyesha unakunywa hiyo dawa na ni kitu kitamu siyo cha kumtisha ,kwa kufanya hivyo ataanza kuzipenda dawa, na uzuri dawa nyingi za kitoto ni Tamu tamu, ongea naye maneno matamu wakati unampa dawa watoto wanasikia hata kama ni mchanga wee jiongeleshe tu., kila la Heri kwenye malezi Bora,na Hongera kwa kuwa baba anayejali.
Kumziba pua mtoto ni hatari
 
Unaweza ukamwekea kwenye chombo ambacho ni invisible yaani haioneshi ndani kuna nini, pia ni vizuri kabla ya kumpa dawa unaanza kumpa kitu kingine kitamu kama juice alafu inafuata dawa ambayo atakunywa kwa kudhani nayo pia ni juice
 
Ni kweli BT lakini hii huwa kwa sekunde chache tu halafu mtoto asiwe chali sana kichwa chake kiwe kimeinuka juu ukilinganisha na kiwiliwili chake. Hili zoezi ni gumu lakini mzazi ni lazima alifanye ili kuhakikisha mtoto anakunywa dawa husika ili kumponya.
Asante kwa ufafanuzi mzuri.....be blessed
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ninavyofahamu dawa za watoto ni syrup tena ni tamu. Nenda kwenye maduka ya dawa (phamarcy) nunua syringe (bomba) weka dawa mpe mtoto mdomoni, ukiwa unacheza nae. Ukishatumia tupa kuavoid infection kwakua zile ni disposable.
 
Ipo haja ya wanandoa kupata semina elekezi kabla ya ndoa na wakikaribia kupata mtoto
 
Mungu mwema kama anaendelea vizuri, sasa unapokuwa unamnywesha mtoto mbishi kama huyo usisahau na kumziba pua pale unapoingiza dawa mdomoni namaanisha tayari umeshaweka mdomoni zibane pua zake kwa vidole vyako, ni kitendo cha sekunde tu hii hufanya dawa kuingia moja kwa moja kwenye njia yake bila kuingia kwenye njia ya hewa, na njia hii huzuia mtoto kupaliwa, pia kitendo cha kuminya pua zake lazima kitamstua na hatapenda lazima Ile dawa ataimeza moja kwa moja.

Pia jitahidi kumfanyia michezo mbalimbali ya kumfurahisha ambapo unaweza kumpa dawa hata bila ya kutumia nguvu,michezo hiyo husaidia kumsahaulisha habari za dawa,pia kny michezo hiyo na wewe unaweza kutest kuonyesha unakunywa hiyo dawa na ni kitu kitamu siyo cha kumtisha ,kwa kufanya hivyo ataanza kuzipenda dawa, na uzuri dawa nyingi za kitoto ni Tamu tamu, ongea naye maneno matamu wakati unampa dawa watoto wanasikia hata kama ni mchanga wee jiongeleshe tu., kila la Heri kwenye malezi Bora,na Hongera kwa kuwa baba anayejali.
Wewe ni muuaji kabisa wala hufai, kitendo tuu cha mtoto kupaliwa ni kosa kubwa sana halafu unashauri amzibe pua, shule gani hiyo umesoma??????? Zaa wa kwako umfanyie hivyo.
Mtoto ukimlazimisha ndio anazidi kuogopa kabisa, inabidi uingize "fun" wakati wa kumpa dawa, mfano unaweka then unamwambia yy akunyweshe kwanza halafu wewe unamnywesha nk nk, hizi shauri zingine wala husifuate
 
Asante ndugu ubarikiwe,wewe mwenye Elimu uliyesoma Marekani toa ushauri .......Wala siyo ugomvi na huna haja ya kutumia lugha za matusi,soma btn line utaelewa .
 
Kwa hili la jinsi ya kumpa dawa mtoto sina ushauri. Ukiwa na shida ya jinsi ya kuficha dawa mtoto asizibwie niulize.

Pili- mtoto anaumwa mafua unampa amoxillin? Kwani ana maambukizi aka bacteria infection yeyote?
 
Back
Top Bottom