Ni sahihi kumpa dawa (coldril) mtoto mdogo wa miezi 2?

kikiboxer

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
3,076
8,132
Wakuu habari zenu!

Nina mtoto mdogo wa miezi 2 na siku kadhaa juzi alienda kliniki akachomwa sindano ya chanjo sasa jana kaamka na mafua hali inayopelekea kulia muda mwingi.

Mama watoto leo asubuhi ilibidi aende kizahanati fulani kupata ushauri wa daktari, wakamwandikia dawa ya coldril awe anampa mtoto kutibu mafua.

Mimi sikuwepo nyumbani ilibidi anipigie kuniambia nami sababu sina utaalamu nikampigia mdogo wangu mmoja(kiumri) ambae ni daktari akanishauri tusimpe hiyo dawa sababu mtoto bado mdogo hivyo figo zake bado hazikomaa kuhimili madawa.

Sasa wakuu napenda kupata maoni yenu humu je ni sahihi kwa mtoto kupewa hizo dawa?
Na je ninahaki ya kuuliza elimu ya daktari/mtu anaeni attend kabla hajaanza kunipa huduma kwa zahanati zetu hizi ndogo ili kupunguza risk ya kupata huduma ambayo si sahihi?
Naomba kuwasilisha mada nikisubiri majibu wakuu.

N:B kama kuna aliewahi kuuliza ishu ya namna hii basi nitaomba mnitag. Asanteni
 
Mpeleke/Mrudishe mtt hospital.. Tafadhali.

Na hakikisha unamuona Daktari. Na unaeleza kila kitu kinachomsumbua mtoto au ambacho si cha kawaida ya mtoto hata kama ni kidogo kiasi gani.
 
Mpeleke/Mrudishe mtt hospital.. Tafadhali.
Na Hakikisha unamuona Daktari. Na unaeleza kila kitu kinachomsumbua mtt.. au ambacho si cha kawaida ya mtt.. hata kama ni kidogo kiasi gani.
Nimekuelewa mkuu lakini hizi dawa aliandikiwa hapo zahanati na daktari wao.
So nataka kujua kama ni sahihi kumpa aendelee kutumia baada ya kupata ushauri wa huyu jamaa yangu mwingine
 
Usimpe mtoto coldril bado mdogo sana. Kwa mafua nadhani vichanga wana dawa za matone za kuimgiza puani ila pia mama akazane kunyonyesha sana maziwa ya mama ni dawa. Mwisho kabisa ampeleke kwa daktari mwingine kama hali itakuwa sio nzuri
 
Mwambie mkeo asage kitunguu swaumu punje kumi, achanganye na maji kijiko kimoja ampake kwenye unyayo wa miguu. Akiamka mafua yameisha yote.

Kama kuna shida nyingine aende hospitali, ila hiyo ni dawa ya mafua ya asili na inatibu vizuri sana.
 
Asante sana mkuu. Nashukuru kwa mchango huu hata daktari huyu mwingine aliniambia tu kukazana kunyonyesha maziwa ni dawa tosha.
 
Mwambie mkeo asage kitunguu swaumu punje kumi, achanganye na maji kijiko kimoja ampake kwenye unyayo wa miguu. Akiamka mafua yameisha yote.

Kama kuna shida nyingine aende hospitali, ila hiyo ni dawa ya mafua ya asili na inatibu vizuri sana.
Shukrani sana mkuu hii naona ni mpya kwangi lakini pia haina madhara. Nitazingatia.
 
Mkuu msimpe ni mdogo sana haishauriwi,wangu akipata mafua nakata vitunguu maji namuekea kwenye soks,vingine naweka kwenye sahani/kisosi kwenye kimeza ndani ya chumba alimo mtoto,haichukui muda mafua yanaisha.

Na kuna Dr anashauri yakizidi yakiwa yanaziba pua apewe *saline drops*nimesahau kidogo nliona muda i hope nimekumbuka sahihi
 
Mafua kwa mtoto wa miezi 2 ili mradi anapumua sio ugonjwaa yanii...!! Katapona tu mzee acheni kumchosha mtoto na nadawa mapema. Yakizidi kuna nasal drops andondoshewa.
 
Si vyema ka umri wa mtoto kumpa dawa husika. Dawa hizi zina viambata vyenye asili ya alcohol/pombe. Hivi huingilia mfumo wa makuzi ya akili ya mtoto kiakili. Mara nyingi dawa hizi na za kikohozi hushauriwa kwa watoto wenye umri wa miaka 2.

Unachoweza kufanya ni kupata hiyo saline drop ambayo ni maji na chumvi chumvi au chemsha maji safi, yaache yapoe, weka chumvi kidogo na umdondoshee puani kama hiyo saline.
 
Peleka mtoto hospitali. Usicheze nq afya ya mtoto mdogo, mama mjamzito au anayenyonyesha ! !

Codlril, vitunguu thomu na blablq nyingine hujui vitaathiri vipi afya ya mtoto wa miezi 2!!!
 
Nashkuru sana kwa michango yenu wakuu.
 
Back
Top Bottom