Naomba ushauri tafadhali....

Naomba ushauri tafadhali....

Huyu utakuta anasababu zingine za kuolewa na huyo bwana na si mapenzi. Mapenzi yana wivu ati. Mapenzi sio unyonge vile. Aombaye msamaha hubadilika. Huyo mwanaume anajua amekukamata huchomoki.
Jithamini uthaminiwe. Inawezekana akakuacha leo na kesho ukapata mwingine. Sidhani umeishiwa market kihivyo kiasi kwamba akuhenyeshe kiasi hicho, na wewe ukubali.
 
Sasa madhila yote hayo halafu soon unaolewa naye!
Kwa nini mabint mkiahidiwa ndoa uwezo wenu wa kufikiri unayeyuka?
Mko mbali ugomvi kila uchao,mkiishi pamoja hata Hiyo nyumba utaitamani kweli?

Ennie mpnz ndomana nahitaji ushauri mamii

Thnx
 
we binti tafuta wimbo wa SIKILIZA- NGWEA feat.Jay Dee,FA

utakusaidia
 
............... girls get married thinking once married their man/ husband will change but the truth is they dont.

za kuambiwa changanya na zako dada Filomena

Asante
 
Last edited by a moderator:
Tatizo lenu hapa ni kule kuka wachumba kwa miaka mingi amekuzoea umechuja thamani yako ungekuwa mke angekuwa na hofu maana uchumba unaweza kuvunjika muda wowote kwa hiyo pima mahusiano yenu hayo halafu chukua hatua
 
Dada huna pa kuupeleka huu upendo wako unakostahili?
Hujui kuwa kuna watu watauheshimu na kuuthamini huu upendo wako?
Mbona unaudhalilisha namna hii huu upendo?

Kosa kubwa sana ambalo hua mnajidanganya ni kuwa mnadhani kuwa kuna mtu anaweza kumbadilisha yoyote yule

Ukweli ni kwamba hakuna mtu anaeweza kumbadilisha yoyote yule

Mtu hubadilika mwenyewe akitaka

Kama kuna mtu ambae amembadilisha mtu basi ujue huyo aliyebadilika ni kwasababu za woga fulani tu na siku huo woga ukiisha utaziona rangi zake

Dada sasa mko kwenye uchumba na umeona vituko na unyanyasaji mkubwa kiasi hicho halafu bado unataka kuingia kwenye hiyo ndoa,au unataka kufa?

Kudhani kuwa mtu atabadilika ni kujidanganya dada yangu

Ngoja nikupe siri moja kubwa sana,duniani kuna wajinga wakubwa na wengi sana ambao wao kupendwa ni ishara ya ujinga,hivyo ukimpenda mtu wa aina hiyo ni sawa na kuweka chakula kitamu mbele ya mwendawazimu ataishia kukimwaga chini chakula hicho na kwenda kula jalalani

Huyo bweg.e [samahani kwani sina namna nyingine ya kumuita] anajua kuwa unampenda ndio maana anafanya hayo madudu

Onesha msimamo kwa kufanya yafuatayo:
Sitisha uchumba

Sitisha mipango ya ndoa

Acha kumtembelea

Katisha mawasiliano naye

Yote hayo yafanye kimya kimya,najua utajisikia maumivu sana lakini usiogope wala kutetereka kwani hata sindano nayo inauma lakini inakuponya

Ukiona unapita muda na hakutafuti endelea na maisha yako

Akija kukutafuta mkaushie kwanza hadi umuone ameteseka vya kutosha maana watu wa aina hiyo huwa ni dhaifu sana,kisha kaa nae chini na umuambie namna unavyohitaji mahusiano yenu yawe,kisha weka time frame ya kumkagua

Time frame ni muhimu kwakuwa hao hawakawii kurudia madudu yao,ukimuona amejirekebisha fungua taratibu za ndoa,ukiona hafai tupa kule!!

Asante sana kwa ushauri..,. God bless u
 
Pole sna.ila waswahili wanasema.dalili za mvua nimawingu basi hapo hakuna future inakubidi umuombe mungu akupatie mwezi unaendananae kuliko wewe kumbadilisha.ukisubiri subiri utakuja kujuta humeshaharibu mfumo mzima wa maisha yako.mtu hujilekebisha mwenyewe na mungu wake.
 
Piga chini huyo jamaa hatakufaa kabisa kuwa mmeo
 
Huyu utakuta anasababu zingine za kuolewa na huyo bwana na si mapenzi. Mapenzi yana wivu ati. Mapenzi sio unyonge vile. Aombaye msamaha hubadilika. Huyo mwanaume anajua amekukamata huchomoki.
Jithamini uthaminiwe. Inawezekana akakuacha leo na kesho ukapata mwingine. Sidhani umeishiwa market kihivyo kiasi kwamba akuhenyeshe kiasi hicho, na wewe ukubali.

Ni mapenzi tu double R ninakazi nzuri najitosheleza...
 
Siku 3 za weekend unaona nyingi, vipi kuhusu 'hadi kifo kiwatenganishe'?

Dhumuni la uchumba ni kuchunguzana, umeshamjua chukua hatua mwenyewe.

Usifikiri atabadilika, maana kama kashindwa kuwa 'at his best' wakati wa uchumba; unategemea akishakuweka ndani ndio ataboreka?

Kumbuka ni maisha yako, na beneficially wa kwanza baada ya Mungu ni wewe na sio mashosti au wazazi au mtu mwingine. Ni bora ukosee kwa yule anayejitahidi kuficha mapungufu yake kuliko huyo asiyejali hisia zako tangu mwanzo.

Siku njema.
 
Ameshaona hauwezi kumwacha,ila hakuna mtu anaeweza kumbadilisha mtu zaidi ya mtu kuamua kubadilika,
 
Si wewe umbadilishe,ila yeye mwenyewe akubali kubadilika......huwezi kumbadilisha mtu hata siku moja,kama ni mlevi,mgovi,mnyanyasaji u better liv with tht..jambo muhimu unalotakiwa kujua ni "some dreams were'nt meant to come true"........run before its to late.
 
Hatuaminiani na nikienda sehem ntakuwa naulizwa muda wote narudi saa ngapi na kununiwa juu wakati yeye anaenda popote haijarishi kanambia au lah....

umesema mnaishi mikoa tofauti, huwa anajuaje kama umekwenda sehemu? Au huwa unajuaje kama kanuna wakati mnaishi mikoa tofauti? Au mkitembeleana wikiendi baada ya kusalimiana mmoja wenu anakwenda kutembea sehemu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom