baharia 1
JF-Expert Member
- Sep 13, 2019
- 1,452
- 1,583
Habari wakuu,
Mimi ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 25. Nilikuwa kwenye mahusiano na mwanamke ambaye ananizidi umri kwa miaka 7. Yeye ana mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 kutoka kwenye mahusiano ya awali. Katika mahusiano yetu, mwanamke huyu alipata mimba ya watoto mapacha.
Kila siku namuachia shilingi 20,000 kwa matumizi, na mara chache sana ambapo nimekosa, namuachia shilingi 15,000.
Kwa mwezi, inaweza kuwa mara 5 hadi 6 ambapo namuachia shilingi 15,000. Ikitokea siku sijatoa hela, lazima kesho yake nimuachie shilingi 25,000 hadi 30,000 ili kufidia siku iliyopita.
Huyu mwanamke ananipa lawama nyingi sana na anaona hela ninayomuachia haitoshi. Maneno yake mabaya yamenichosha kabisa, nimefika kiwango Cha mwisho cha uvumilivu kwa ajili ya mdomo wake.
Anataka nimskilize na nimfuate kila anachosema, lakini mimi sijaumbwa hivyo kumskiliza mwanamke anachotaka ndo nikifanye.
Anaona kama ananikomoa kwenye matumizi.
Pia Mimi ni mnywaji wa pombe na naweza kutumia zaidi ya shilingi 50,000 nikiwa na marafiki zangu basi huyu mwanamke hapendi marafiki zangu na hata akikuta nimekaa nao, hawasalmii, wakimsalmia haitikii, Yani amenichosha. Nimemchoka mwili hadi akili, sina raha kabisa. Hata haka katoto chake ni kajeuri balaa na kalikuwa hakaniamkii kakawa kanipigwa na mama ake sasahivi ndo kananiakia shkamoo mjomba kakaniona kananua Yani Kila mtu ananichosha kwakweli Yani nachoka ntakufa sasa, WAKUU NIMECHOKA MWILI HADI AKILI.
Naombeni ushauri wenu wakuu nifanyaje maana akili yangu inachoka kabisa. Nimechoka mwili na akili, sina raha.
Asanteni.