nature is always nature: Yote haya ni jinsi gani mnahuisha ndoa yenu na jinsi gani mpo open kwenye mawasaliano. Jamii zetu za kiafrika zimelea wanawake kama wanaongojea kuambiwa, kuanzwa, kupapaswa nk. Ni ngumu kutoa ghafa kitu mtu anachoamini hivyo ukielewa makuzi na culture ya mtu unaweza ku edit baadhi ya vitu , mfano
- mwekee mazingira ya kusikilizwa na umuweke huru aongee na wewe jambo lolote, after all she is your wife. Wanaume wengi hawajui kuwa kiu kubwa ya wanawake ni maongezi. Na mara nyingi mama anapoanza stories na vitu kama hivyo baba anaweza kumzima ghafla. Pia elewa kuwa perception zako mwanaume na za mwanamke ni tofauti hivyo unavyoua story zake (hata kama ni kuhusu a simple movie) basi unapunguza ile intimacy
- pamoja na ubize kumbuka kumtoa outing : Hii simaanishi kutembelea ndugu au jirani, la bali mtoe outing mara moja kwenye sehemu nafuu na kama uwezo upo sehemu nzuri. Na muende wawili maana ukiwa na watoto mnakosa bonding. Na endelea kumuweka wazi kuwa unampenda na unapenda maisha yenu yawe ya amani .
- zawadi ndogo ndogo: A blouse, underwear , a handkerchief mara moja moja
- wasiliana nae mchana kuwa unampenda , unamiss ; muulize anaendeleaje nk , kama mliachana asubuhi anaumwa kichwa mpigie mchana muulize anajisikiaje
- epuka mawazo mabaya bila sababu maalumu: Ni kawaida mwanamke kutokuwa na hamu kama hakuna mawasiliano, hukumsikiliza vema katika issue fulani, umemdharau , nk --maana sex kwa mwanamke inaanzia kwa jinsi mnavyowasiliana, nk . Kwa mwanaume hamu ya tendo ipo tu hata kama mmetoka kugombana. Ukielwewa tofauti hizi zitakusaidia sana.
- umewahi kusema samahani ukikosea au unassume tu kuwa mambo yameenda sawa sawa?
- unasaidia mara moja moja kumbeba mtoto , kazi fulani au anafanya yote?
- unamjali matumizi ya nyumbani nk?
- kubwa ya yote : Mpeni mungu nafasi ya pekee katika ndoa yenu , awaongoze katika umoja wenu , mnie moja , kusiwe na uchoyo nk
maisha ya ndoa ni rahisi kama mume atakaa kama mume, wanawake ni rahisi sana kuadjust kama mwanaume anaonyesha muongozo katika kuweka mahusiano yakawa wazi, ya kirafiki, nk.