Naomba ushauri nini nifanye inapokosekana ada ya Chuo kwa kijana wangu?

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
997
828
Kutokana na Shughuli zangu za kubangaiza kwenda kombo, huenda nitashindwa kuendelea kumlipia gharama za Chuo Kijana wangu (me) anayechukuwa Diploma ili aweze kuchukua Digrii, naomba msaada ninachotakiwa nikifanye kama Mlezi.

Pamoja na yote ila bado sijamwambia Mlengwa naombeni ushauri wa nitakachomwambia naogopa nisije nikamchanganya zaidi kuliko kutengeneza Saikolojia yake, tunakusanya nguvu pamoja na mwenyewe ili mwakani arudi Chuo.
 
Kwa nijuavyo kila chuo na utaratibu wake ni vyema ungeulizia kwa chuo husika. Mfano kuna vyuo vingine unaandika barua ya kwenda kwa uongozi wa chuo kuonesha huwezi kulipa ada kwa wakati wakuvumilie hadi utakapo pata (kuna muda maalumu unasema katika barua kua utakua ushalipa hiyo ada).

Kwa hiyo hapo mara nyingi inatagemea na utaratibu wa chuo husika ni vema ukaulizia kwa chuo chao.
 
Ila wazazi bado mna ulimbukeni sana wa "mavyeti" ya vyuoni.

Taaluma ni uwekezaji.

Huwezi kutoa mapesa kulipa ada in exchange for makaratasi ambayo hayatarudisha pesa.

Sasa kama alimaliza Diploma ulikuwa na sababu gani ya kumpeleka Degree directly wakati hana uelekeo wowote wa kazi ?

Au Ndio mashindano mtaani na yeye lazima awe na Degree ?

Anyway! Kama ukishindwa kabisa, mwambie FREEZE mwaka MMOJA atulie maana vyuo vinaruhusu mpaka miaka miwili.
 
Mkaruka, Huu ni ushauri wa walionacho siku zote,

By the way mleta mada fanya jitihada mpaka mwisho mwanao apate Ada mrudishe chuon aendelee kusoma ada hulipi kwa mara moja

Tumia njia yakuandika barua kwa uongoz wa chuo wakuomba kuongezewa muda wakulipa' hii anaweza kuandika ata mwanao mlipiwa ada

Tumia jitihada zako had mwisho huku chuo kikiona jitihada zako anaweza akasoma ata mpaka akafika kwa mtihan wa mwsho kwa njia hz.....

HAKUNA MBADALA WA ELIMU MSOMESHE MWANAO

HAO WAKUITA CHETI KARATASI WAPUUZE KABISA KABISA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
j6dulle,
Mkuu sishauri mtu asiende chuo.

Ninachoshauri huyo mwanaye kama anamaliza Diploma atafute kazi kwanza ndio aende chuo.

Mwisho wa siku hata ukiwa na PhD umeisoma mfululizo kuanzia standard ONE, kwenye maisha ni lazima utalazimika kuanzia chini.
 
Mkuu pia nawewe ninakushukuru kwa maoni yako, ila naomba nikuulize kwasasa ndio anamaliza masomo yake je! Kwenye Digrii wanaweza kumpokea bila Ada?
Aise kumbe tayar ana diploma ,

Elimu ya juu si lazima Ndugu vyema atumie hyo diploma Kwanza Tena Kama wewe ni mzazi HONGERA kazi yako hapo imeisha muache atumie hyo diploma Kwanza


Diploma yake n field gan??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anachotaka kusoma ni International Relations, lkn kwasababu alikosa Points za kuanza Digrii ikabidi aanze Diploma kwenye Human Resources.
j6dulle,
 
Anatafuta GPA akasome Uhusiano wa Kimataifa, kwasasa ana Diploma ya HR. Asante kwa ushauri.
j6dulle,
Una sehemu ya kumweka bada a kuhitimu hio kozi ?

Maana kozi hio haijibebi yenyewe mpaka Network ukichukulia kwamba atakuwa na ZERO Experience.
 
Kutokana na Shughuli zangu za kubangaiza kwenda kombo, huenda nitashindwa kuendelea kumlipia gharama za Chuo Kijana wangu (me) anayechukuwa Diploma ili aweze kuchukua Digrii, naomba msaada ninachotakiwa nikifanye kama Mlezi.

Pamoja na yote ila bado sijamwambia Mlengwa naombeni ushauri wa nitakachomwambia naogopa nisije nikamchanganya zaidi kuliko kutengeneza Saikolojia yake, tunakusanya nguvu pamoja na mwenyewe ili mwakani arudi Chuo.

Professional certification: Angalia uwezekano wa kumshauri afanye professional certification ya kitu fulani, badala ya kwenda masomo ya shahada.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom