Naomba ushauri nifanyeje

Naomba ushauri nifanyeje

Meeks

Member
Joined
Jul 12, 2014
Posts
15
Reaction score
12
Mambo vipi wana JF, nahitaji ushauri wenu kwenye hili.

Ni mwaka sasa umepita toka nianze mahusiano na huyu msichana. Wakati tunaanza mahusiano alikua akiishi hostel za chuo chao but after miezi mitatu akaniambia anahamia kwake kwani mama yake kamkubalia kumpangishia nyumba.

Baada ya kuhamia kwake kama mwezi ukapita nikaenda kumtembelea kwake palinishtua kidogo alikua amepanga zaidi ya chumba kimoja kama nilivyofikiri nyumba ilikua na Sebule, jiko, chumba cha kulala na pia alikua na vitu vya ndani vyote ikiwa mziki mkubwa, tv-flat, masofa, kabati n.k.

Ilinishtusha kwamba mama yake ampangie ghafla hivyo na vitu vyote vya gharama hivyo but alinihakikishia ni mama yake na kunihakikishia zaidi mama yake alikua akija kumtembelea ananitumia mpaka picha.

Wakati huo wote mimi pia nlikua nikiishi kwangu tho pia nlikua nasoma chuo. Alifanya sherehe ya kuhamia kwake na alialika marafiki zangu na marafiki zake wachache pia but marafiki zangu walishtuka baada ya kupaona kwake but niliwaambia ni mama yake na huwa anakuja mara kwa mara so wakaamini hivyo kwa shingo upande.

Ki ukweli ananipenda sana kiasi kwamba kwenye watsup dp yake ananiwekaga mimi tu mda wote na instagram full kuweka picha zangu na ujumbe wa mapenzi kuonesha ulimwengu ananipenda sana.

Nikajiaminisha napendwa sana.Kwa sababu kwangu nipadogo(chumba kimoja) aka ning'ang'aniza ni hamie kwake. Nika hamia tho niliamia na rasket tu vitu vingine vilibaki kwangu na niliendelea kulipa kwangu kodi tho nimehamia kwa demu tiyari.

But juzi akaamua kuniapasualia ukweli wote tukiwa kitandani. Kuwa kwao maisha ni ya chini sana tofauti na ninavyomuona na jamii inavyomchukulia pia kwao hawawezi ata kumlipia ada ya shule na matumizi tofauti na nlivyokuwa nafikiria kabla.

Baada ya miezi miwili ya kuaanza mahusiano yetu alifukuzwa chuo kwa kukosa ada baada ya ndugu aliyekua anamsaidia kutofautiana nae na baada ya hapo alikutana na mbaba flani ambae alimuonea huruma na kuamua kumlipia ada na hela ya matumizi kama mwanae.

Lakini eti baada ya miezi mitatu yule mbaba akampeleka nje kidogo na jiji na kulala nae mchana kwa hoteli na wamesha lala mara nne toka wakutane sasa ikiwa ni karibu mwaka na vitu vyote vya ndani,ada na hela tunazokula sio za mama yake ni za huyo mbaba.

Na ananiambia hayo yote coz ananipenda sana na anataka kuachana na huyo mzee coz karibu anamaliza chuo na ameshamlipia ada tayari.Ndugu nilihisi naota ndoto kumbe ilikua ni kweli nilishindwa kumjibu mpaka leo na jibu sina.

Ni kamuuliza mbona mama yako alikua anakuja kwako akaniambia mama yake anajua pale ni kwangu na nilikua nimesafiri.

Wana JF naomba ushauri nimkimbie, nimvumilie tho sina hela zakumpa akiachana na huyo mtu wake,ama nifanye nini?

Tumeshapima afya zetu wote tupo wazima. Na bibie anaforce kumwambia huyo mzee waachane sasa nafikiria wakiachana nani atampa hela ya matumiza kila siku mimi sina hizo hela?
 
uamuzi ni wako uendelee nae au vipi muhimu mkapime afya hawa wazee wahongaji sometime wanakuwa hawako fit ndo mana hawaoni hasara
 
siku zote prefer gesti na hoteli.....kulala vitanda ambavyo hujatoa pesda kununua kunaweza kukuletea hatari kubwa
unaweza poteza maisha.......

cha kwanza hama hama hapo na usirudi tena....hata ukiendelea na huyo msichana hapo usikanyage
 
Mkuu shukuru kakwambia ukweli sababu ungejua kutoka kwa mtu mwingine ingeuma zaidi.

Msisitize aachane na huyo mzee kama kweli una nia ya kuwa nae ila kama hutaki muache aendelee nae.
 
Shukuru kwa kuambiwa ukweli... pia kuna mambo mawili kakueleza ili umpe nafasi usiendelee kumganda na pia yawezekana kakwambia ili ujue ukweli... ukweli anaujua mwenyewe.... ila nashindwa kukuelewa na baadhi ya wanaume wengine unapata wapi nguvu ya kwenda kulala kitanda cha mwanamke tena unahamia kabisa mi naona ni fedheha na kutokujielewa.. badala ya wewe kuona kakupiga gape uchakarike wewe unahamia kwenda kushare umaskini.... ona sasa mda wote kakufanya zoba jinga na vivu... leo anakupa live ni aibu... namshukuru bibie kakufunza kama unajielewa uwez kubali lala tena kwenye nyumba ya mwanamke...
 
Mkuu shukuru kakwambia ukweli sababu ungejua kutoka kwa mtu mwingine ingeuma zaidi.

Msisitize aachane na huyo mzee kama kweli una nia ya kuwa nae ila kama hutaki muache aendelee nae.

Akiachana na huyo mzee maisha aliyozoea kuishi bibie ataweza kumpa?... asimshawishi kuachana na huyo mzee ila amwache bibie afanye maamuzi mwenyewe..... ila ukiangalia kwa undani binti anahitaji space jamaa kashindwa kureact angemjibu dry ndiyo angejua ukweli kabisa.........uwezi kuwa na power while u have nothing..... . Kijana jamani kakaa kimya anashindwa hata afanyaje kaishi maisha ya juu sasa anatakiwa kurudi chini kwa kweli ni tatizo
 
Hivi nyie wakaka mbona mnapenda sana kujidhalilisha? Unaanzaje kuhamia kwenye nyumba ya girl wako, whether kajipangishia au kapangishiwa na wazazi wake? Ulienda tu na kibegi chako but soon ungehamishia kabisa na vitu vyako vyote huko.

Shukuru Mungu mdada kakuambia ukweli coz kuna siku ungeshangaa tu umeng'olewa kucha kumbe kisa unakula mali ya kigogo. Huyo girl wako amejiandaaje kuishi bila support ya kigogo? Will you be the one taking care of her? Coz kumaliza chuo sio guarantee ya kufanikiwa, kuna msoto heavy kitaa, ataishije? Na je huyo kigogo ni mpole sana kiasi kwamba atawaacha tu mkaishi kwa raha zenu even after spending so much on her?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Subiri UGRADUATE WITH AIDS WAKATI WENZIO WANAGRADUATE NA A's ndo kijijini kwenu watakulilia kweli! Namaaaaaaaf zako, taifa linaingia deni lisilolipika msome fu kupign FREE tu huko ndo biashara yenu!
 
Subiri UGRADUATE WITH AIDS WAKATI WENZIO WANAGRADUATE NA A's ndo kijijini kwenu watakulilia kweli! Namaaaaaaaf zako, taifa linaingia deni lisilolipika msome fu kupign FREE tu huko ndo biashara yenu!

Washauri sasa hapo umewasaidia
 
Pole swahiba najua kwa sisi wachangiaji ni kitu rahisi ila kwako unapitia wakati mgumu sana kufanya maamuzi sahihi.
Kama unaamini kasema anataka kuachana nae sio kesi hold on with her maana sisi sote inawezekana hawa tunaowaita wapenzi au wake zetu tunachangia na wenzetu ila tofauti na wewe sisi hatujui labda muda bado,jambo la msingi ni kujua kama ataweza kuishi maisha ya kawaida baada ya kuachana nae maana simply kazoea maisha ya juu asifikiri kumaliza chuo ndio mwisho wa matatizo muulize kipindi kinachofuata ni kubeba bahasha ya khaki kusaka ajira vipi atakua mwaminifu au kule aendako na bahasha atawapa tena maana ukizoea njia fupi huwezi kupita njia ndefu.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom