Naomba ushauri, nataka kwenda Dubai

johbizzy

Member
Sep 8, 2015
73
49
Wakuu poleni na majukumu, mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 32, nimepambana sana bongo nikafanikiwa kujenga kibanda na kununua gari ndogo Mambo yalikuwa vizuri lakini baada ya Samia kuingia madarakani ndipo Mambo yalipoanza kuharibika.

Nilivunjiwa vibanda vyangu vya tigo pesa, m pesa, yaani mtandao kiujumla, nikaibiwa pesa zangu zote bahati mbaya nilikuwa na mkopo bank maisha yakaanza kuyumba, nikajikuta nashindwa kulipa Deni, gari yangu Nikaifanya Uber na bolt lakini mambo bado magumu.

Sasa nakuja kwenu wazee nimepata mchongo Dubai wa kulipwa dollar 500 kwa mwezi kulala, chakula, bima juu ya boss, naomba ushauri wazee niende au niendelee kupambana bongo japo mambo magumu.
 
Wakuu poleni na majukumu Mimi nikijana mwenye umri wa miaka 32 nimepambana Sana bongo nika fanikiwa kujenga kibanda na kununua gari ndogo Mambo yalikuwa vizuri lakini baada ya Samia kuingia madarakani ndipo Mambo yalipo Anza kuhalibika nilivunjiwa vibanda vyangu vya tigo pesa...
1800dhs ndogo sana mkuu

Nenda ukafanye huo mchongo huku ukitafuta mchongo mwingine ukouko unaolipa zaidi ya huo vinginevyo komaa tu apaapa au uza gari ufanye mtaji uanze upya
 
Wakuu poleni na majukumu Mimi nikijana mwenye umri wa miaka 32 nimepambana Sana bongo nika fanikiwa kujenga kibanda na kununua gari ndogo...
Pole sana kwa yote uliyopitia. Inasikitisha kusikia kuhusu changamoto unazokabiliana nazo. Kuhusu mchongo Dubai, kabla ya kufanya uamuzi, ni muhimu kuzingatia gharama za maisha huko pamoja na mshahara unaopokea.

Kwa kuwa Dola 500 kwa mwezi ni sawa na takribani Tsh 1,160,000 kwa mwezi kwa kiwango cha sasa cha kubadilisha fedha, unahitaji kuzingatia kama hii ni kiasi cha kutosha kufunika gharama za maisha Dubai.

Gharama za makazi, chakula, usafiri, na bima ya afya huwa ghali katika miji mingi ya nchi za nje. Kwa hiyo, ni muhimu kupata taarifa sahihi kuhusu gharama za maisha Dubai kabla ya kufanya uamuzi.

Pia, ni vizuri kuzingatia uwezo wako wa kukabiliana na hali ngumu kwa uzoefu wa kazi katika mazingira mapya. Ni muhimu kufanya uamuzi sahihi ambao utakusaidia kufikia malengo yako ya kazi na kuboresha hali yako ya kifedha.
 
Pole sana kwa yote uliyopitia. Inasikitisha kusikia kuhusu changamoto unazokabiliana nazo. Kuhusu mchongo Dubai, kabla ya kufanya uamuzi, ni muhimu kuzingatia gharama za maisha huko...
Asante Sana kaka kuhusu gharama za chakula ,maladhi, bima ni juu ya muajiri wangu mkuu ndio nasubiri mkataba nisome vizuri then nichukue mamuzi ila mpaka Sasa Kaka nadaiwa na bank More than 7 million
 
Asante Sana kaka kuhusu gharama ,za chakula ,maladhi, bima ni juu ya muajiri wangu mkuu ndio nasubiri mkataba nisome vizuri then nichukue mamuzi ila mpaka Sasa Kaka nadaiwa na bank More than 7 million
Ni vizuri kujua kwamba mwajiri wako atagharamia gharama za chakula, makazi, na bima. Hata hivyo, inaonekana kwamba una deni kubwa na benki.

Ni muhimu kuweka malipo ya deni lako kipaumbele kabla ya kuzingatia maamuzi makubwa ya kifedha, kama vile kuhamia nchi nyingine.

Je, Umewahi kufikiria kutafuta ushauri kutoka kwa mshauri wa kifedha au mshauri wa deni ili kukusaidia kusimamia deni lako na kuunda mpango wa kulilipa?
 
Asante Sana kaka kuhusu gharama ,za chakula ,maladhi, bima ni juu ya muajiri wangu mkuu ndio nasubiri mkataba nisome vizuri then nichukue mamuzi ila mpaka Sasa Kaka nadaiwa na bank More than 7 million
Acha uoga nenda huko Duniani,
Humu waweza kutishwa tishwa sababu wabongo wengi mfumo wetu wa malezi ni kufungiwa ndani na sio kutolewa kuiona Dunia,

Kama kuna mchongo mwingine wanahitaji madereva wa kike nipatie niende.
 
Ni vizuri kujua kwamba mwajiri wako atagharamia gharama za chakula, makazi, na bima. Hata hivyo, inaonekana kwamba una deni kubwa na benki. Ni muhimu kuweka malipo ya deni lako kipaumbele kabla ya kuzingatia maamuzi makubwa ya kifedha, kama vile kuhamia nchi nyingine. Je! Umewahi kufikiria kutafuta ushauri kutoka kwa mshauri wa kifedha au mshauri wa deni ili kukusaidia kusimamia deni lako na kuunda mpango wa kulilipa?
Atalilipaje bila kutafuta pesa si ndio aende akazitafute ili alipe deni
 
Back
Top Bottom