Naomba ushauri, nataka kufungua biashara ya stationery

cha1509

JF-Expert Member
Jul 6, 2018
258
402
Habari wanaJF,

Natumai hamjambo nyote

Mimi nipo Singida Manyoni nina kamtaji kangu, wazo lililonijia ni kufungua biashara ya vitu vya stationery, ila changamoto yangu sijui navipata wapi kwa bei nzuri, nataka niwe nauza jumla na reja reja pia, hivyo naomba mwenye kujua anijuze napata wapi mzigo kwa bei rafiki?

Karibuni sana kwa mwenye kufahamu anifahamishe.

1619510514384.png

Maana kuna duka moja tu la anayeuza jumla hapa! So nahisi ni fursa moja wapo nzuri.
 
Kwa kuanzia inatosha. Ila lazima uwe na computer, printer, binding machine, lamination machine, paper cutting machine, ili office ionekane ni stationery. Vitu unaweza kununua zamzam au masumin au Kariakoo.
Ununue mzigo Masumin au Zamzam ukauze jumla Singida? Big NO Nenda Mtaa wa Kongo na Swahil au Kongo na Kipata kuna maduka ya jumla ya viandishi vya kila aina kwa Bei unazoweza kuuza jumla, Pia kama uko serious naweza kukupa namba za ajenti wa Karatasi za Maestro (Mondi) na Double A ukawa unapata mzigo kwa bei sawa na wauzaji wa Kariakoo. Ingawa huo mtaji kwa kuanzia ni mdogo kwa serious business walau ungekuwa na 50m unaweza kufanya kitu cha maana badala kuwa msindikizaji.
 
Yaani uweke million 50 kwa bihashara ya stationery. Bihashara ya msimu. Wanafunzi wakifungua ndio bihashara ipo, baada ya apo maumivu
 
Boss naomba namba hizo
 
Yaani uweke million 50 kwa bihashara ya stationery. Bihashara ya msimu. Wanafunzi wakifungua ndio bihashara ipo, baada ya apo maumivu
Hizo pesa mie ningetafta channel ya vanilla nijiweke humo! Biashara za hela kubwa usilenge faida za kitoto always!
 
Habari wanaJF,

Natumai hamjambo nyote

Mimi nipo Singida Manyoni nina kamtaji kangu, wazo lililonijia ni kufungua biashara ya vitu vya stationery, ila changamoto yangu sijui navipata wapi kwa bei nzuri, nataka niwe nauza jumla na reja reja pia, hivyo naomba mwenye kujua anijuze napata wapi mzigo kwa bei rafiki?

Karibuni sana kwa mwenye kufahamu anifahamishe.

Agiza nje mashine kama printer, lamination na etc. Utaweza nunua kwa bei nafuu sana kuzidi huku kama hauna haraka maana mzigo kutokea nje utachukua mpaka mwezi kufika kwa meli
 
Back
Top Bottom