Naomba ushauri: Naishi na mtoto wa mke wangu, wangu anaishi kwa bibi yake nashindwa kumchukua

Hapo Kuna mawili from my point of view.

Either mtoto wangu Aende Kijijini kwenye elimu bora or niichukue familia ya mume wangu wake mjini tukae wote kwenye maisha bora.

Ndo Maana nilisema Ni pagumu.
Love u
 
Huyu jamaa bila shaka nishemeji yangu NIMEKUTAMBUA

wewe unalalama kuwa mtoto wa dada yangu anakula nakusaza mbona nawewe unamkula mama yake (dada yangu) nakumsaza?
 
Kwa trend ya matukio ya unyanyasaji Wa watoto hasa na hawa mama wakambo nikusihi endelea kumuacha huyo mwanao kwa bibiye.

Hakikisha unamtumia mama yako pesa ya kutosha ili asione shda kumlea mjukuu wake ili hali babaye upo.
Kama ushauli wote huo ndio nimeona kidogo ni point kwa xababu hiyo jitàhid kupeleka mahitaji ya kutosha nyumban kwa mama ili mabint zetu wawil na mama yetu waishi maisha ya peponi jalibu kubalance mamb ya town na village tuma pesa zà kutosha
 
Kwa jins unavyoonekana tyu jiandae kujibu kes ya mauaji coz uñàonekana ni mtyu ambae una hacra uchungu na wivu juu ya hako katoto. Take care ipo siku utaua
 
Kaka unajua kuna siku huyo mtoto ataangusha glasi na utampiga nusu kumuua au kumchoma vidole kumbe ni unataka kutoa huo uchungu wa kuona anakula vyako bure bure?

Mama zetu hua hawaombi vikubwa. Lakini chochote utachomtumia anaweza figure out namna ya kufanya walio nyumbani waridhike. Kama kweli shule ya kwa bibi ina ufaulu mzuri si umpeleke na huyu uliyenaye nyumbani ili naye afaulu?

Mimi nafikiri una shida ya ubinafsi na mapenzi kwa wakati mmoja. Now kabla havijakuchanganyia drop huyo mdada na mwanae chukua bibi, mwanao na mtoto wa kaka ishi nao.

Au drop huyo binti kisha nenda kaishi kwa bibi kama concern yako ni kufaulu.

Ushauri wangu umezingatia matukio ya wazazi wanaochoma moto watoto wa kambo au hata kuwaabuse sexually.

Ushauri tafadhali!

Umeoa mke mwenye mtoto na unaishi naye huyo mtoto ukihudumia huduma zote!!

Huko nyumbani nawe una mtoto pia yuko kwa bibi yake (mama yako) anaishi na kusoma, mama wa mtoto wako ametangulia mbele ya haki.

Hapo kwa bibi yake anaishi na mtoto wa kaka yako (dada yake) wanaofanana umri, na historia ikiwemo ya kufiwa mama. hawa watoto wamekuwa kama mapacha, hawatenganishiki.

Ukinunua kitu lazima uwanunulie wote, ukitaka akutembelee mtoto wako bila huyo mwingine basi lazima utaonekana mbaguzi na hauko sawa na huyo utakayemuacha atakuwa kwenye msongo wa mawazo sana.

Maisha ya kuishi kwa bibi yana changamoto zake za hapa na pale; huduma hazitoshelezi, kukosa hela ya shule, kukosa vitafunwa, kukosa nguo, kutoshiba, kutokula unachotaka n.k. Umbali kati yako na mtoto huchangia zaidi changamoto hizi.

Uwezo wako hautoshi kuhudumia kwa kiwango sawa pande hizi mbili, frankly, upande wako na mkeo unapata huduma bora zaidi.

Katikati ya changamoto hizi kwa mtoto wako wa kumzaa, mtoto wako wa kambo unayeishi nae anakula hadi anasaza, anaoga anavyotaka, anapata 200 au zaidi ya kutumia shule kila siku, ananyosha kwa umeme wako kila siku, anapendeza, ananawiri kwa huduma.

Kama nilivyoeleza juu, wako ni tofauti kwani unyoshaji hufanyika kwa pasi ya mkaa, ulaji si wa kuamua, kukosa hela na vitafunwa ni jambo la kawaida, kulala na mlo wa ugali usiku ni kawaida n.k.

Unafikiria kumhamisha na kumleta unakoishi, lkn kuna changamoto hizi zinakutatiza;

1. Shule ya msingi iliyopo eneo lako ni mbovu kuliko huko kwa bibi anakoishi - walimu wachache, ufaulu si wa kuridhisha

2. Ukimhamisha huyo basi kuna uwezekano mkubwa ukalazimika kumhamisha na huyo mwenzie anayeishi nae. Nae ni mkiwa na anahitaji msaada; kaka yako hali si nzuri na yuko mbali huko katika kuhangaika na maisha.

3. Bibi (mama yako) nae ni changamoto nyingine kwani hao watoto ndo kampani yake kuu, upweke atakaojisikia ukiwatoa si wa nchi hii.

Kama binadamu, dukuduku fulani linajaa kila siku kifuani kwamba mtoto asiye wangu anafaidi vyangu huku wangu akihangaika, inafikia kipindi mpaka unamuota binti yako kwa mawazo. Hisia za kukosa baraka kwa Mungu kwa hili zinaanza kukujia kichwani maana unaona kama unamuonea huyu mtoto!!

Mawazo yenu wadau katika hili.......
Mkuu heshima yako

Haya maisha yalivyo ili upate kitu unatakiwa kuwa radhi kupoteza kitu,
Una mambo mawili hapo
1. Mahusiano yako ya kindoa na mkeo
2.mahusiano yako kama mzazi na mwanao

Mahusiano hayo namba moja kihalisia yanaweza kugeuka Muda wowote,kutegemea na Hali yako ya wakati huo ni reversible (namaanisha kupatana na kuachana)

Mahusiano yako ya damu na mwanao ni absolute hayabadiliki kamwe,

Sikushauri uache mkeo ila

Mke wako leo anaweza kuwa mke wa mtu mwingine kesho Ukiwa hai ama Ukiwa umekufa
Mwanao atabaki kuwa mwanao Ukiwa hai ama Ukiwa umekufa, ndio kumbukumbu yako.

Kulea mtoto asiye wako kwa kutegemea atakusaidia mbeleni ni sawa na KUBET,unaweza kupata au kukosa, labda ulee huyo na mwanao akiwa hapo hapo,ni mara mia ulee mwanao hata asipokusaidia ni sawa tu,utakuwa na amani ya kutimiza wajibu wako kikamilifu,wajibu wako KWA mwanao haukomi,ni wako kipindi chote Ukiwa hai kulingana na uwezo wako

Watoto waliofiwa mama mara nyingi ni wapweke kama yatima maana mlezi mkubwa wa watoto ni mama,mwanao anaangukia kundi hili,ni jukumu lako kubeba majukumu yako kama baba na mama kwa wakati mmoja,ujue mtoto amelala wapi na amekula nini

Wababa huwa hatueleweki na watoto sababu tunajua kuwa baba ni kutoa hela ya matumizi tu (unakumbuka lile swali tulikuwa tunaulizana utotoni Kati ya baba na mama nani Afe ,tulikuwa tunajibu,baba afe mama abaki),kwa mwanao imekuwa kinyume,mama ameondoka umebaki wewe ila amini usiamini anatamani walau mama angekuwepo wewe uwe umeondoka(hapa natania)

Mahusiano yako na mwanao akiwa mtu mzima yanategemea ukaribu wako na yeye saizi,sio ukaribu wa kupiga simu,jukumu la kulea mwanao ni lako ww sio la bibi

Baada ya kusema hayo nguvu ya maamuzi inabaki kwako
 
1. Acha ubinafsi/uchoyo/roho ya kwanini, huyo mtoto hana kosa na wala hakujileta hapo. NI WAJIBU WAKO KUMTUNZA hiyo ni sehemu ya familia yako.

2. Pafanye kwenu kuwa pazuri kama hapo, watoto wapate mahitaji muhimu, mama na watoto wale balanced diet.

3. Kusaza au kunyooshea pasi ya umeme siyo vitu vya msingi sana. hakikisha pande zote unatimiza wajibu wako.

4. Usiwaze vitu vidogo kama hivyo, Hadi kumwangalia mtoto mdomoni wakati anakula ili uone atamaliza au atabakisha. eti na mtoto wa kaka ambaye ni kama Pacha naye unamhesabia. PAMBANUA AKILI, WAZA WAZUA KUPATA HELA NYINGI ZIWATOSHE WOTE. ACHA UJINGA WAJIBIKA MDA WOTE HADI USIPATE MDA WA KUHESABU UJINGA HUU
 
Chukua mtoto wako hiyo incidents ilinikuta ila watoto wangu kwanza napua nikawaweka chini nakuwambia hakuna aliyena haki kumzidi mwingine nyote ni watoto wangu haki sawa shughuli ikaisha.
 
1. Acha ubinafsi/uchoyo/roho ya kwanini, huyo mtoto hana kosa na wala hakujileta hapo. NI WAJIBU WAKO KUMTUNZA hiyo ni sehemu ya familia yako.

2. Pafanye kwenu kuwa pazuri kama hapo, watoto wapate mahitaji muhimu, mama na watoto wale balanced diet.

3. Kusaza au kunyooshea pasi ya umeme siyo vitu vya msingi sana. hakikisha pande zote unatimiza wajibu wako.

4. Usiwaze vitu vidogo kama hivyo, Hadi kumwangalia mtoto mdomoni wakati anakula ili uone atamaliza au atabakisha. eti na mtoto wa kaka ambaye ni kama Pacha naye unamhesabia. PAMBANUA AKILI, WAZA WAZUA KUPATA HELA NYINGI ZIWATOSHE WOTE. ACHA UJINGA WAJIBIKA MDA WOTE HADI USIPATE MDA WA KUHESABU UJINGA HUU
ahsante,

ila mimi si mchoyo wala mbinafsi mkuu. si kwamba namchukia huyo mtoto kiasi cha kumwangalia kwa jicho baya kama unavyodhani, hapana. ni vile tu kwamba nafsi ni km inanisuta hivi kuwa si sawa 'asiye wangu' kunufaika zaidi kuliko wangu!

halafu unafikiri sihangaiki mambo yawe sawa mkuu?!!!!! kuhangaika na kufanikiwa ni vitu viwili tofauti. sababu moja ya kuleta hoja hii ni kwa vile kasungura kenyewe hakatoshi sawasawa kuweza kumudu kwa usawa pande zote.........ningekuwa vema mbona upande wa mwanangu ndo kipaumbele kikuu.
 
Mkuu heshima yako

Haya maisha yalivyo ili upate kitu unatakiwa kuwa radhi kupoteza kitu,
Una mambo mawili hapo
1. Mahusiano yako ya kindoa na mkeo
2.mahusiano yako kama mzazi na mwanao

Mahusiano hayo namba moja kihalisia yanaweza kugeuka Muda wowote,kutegemea na Hali yako ya wakati huo ni reversible (namaanisha kupatana na kuachana)

Mahusiano yako ya damu na mwanao ni absolute hayabadiliki kamwe,

Sikushauri uache mkeo ila

Mke wako leo anaweza kuwa mke wa mtu mwingine kesho Ukiwa hai ama Ukiwa umekufa
Mwanao atabaki kuwa mwanao Ukiwa hai ama Ukiwa umekufa, ndio kumbukumbu yako.

Kulea mtoto asiye wako kwa kutegemea atakusaidia mbeleni ni sawa na KUBET,unaweza kupata au kukosa, labda ulee huyo na mwanao akiwa hapo hapo,ni mara mia ulee mwanao hata asipokusaidia ni sawa tu,utakuwa na amani ya kutimiza wajibu wako kikamilifu,wajibu wako KWA mwanao haukomi,ni wako kipindi chote Ukiwa hai kulingana na uwezo wako

Watoto waliofiwa mama mara nyingi ni wapweke kama yatima maana mlezi mkubwa wa watoto ni mama,mwanao anaangukia kundi hili,ni jukumu lako kubeba majukumu yako kama baba na mama kwa wakati mmoja,ujue mtoto amelala wapi na amekula nini

Wababa huwa hatueleweki na watoto sababu tunajua kuwa baba ni kutoa hela ya matumizi tu (unakumbuka lile swali tulikuwa tunaulizana utotoni Kati ya baba na mama nani Afe ,tulikuwa tunajibu,baba afe mama abaki),kwa mwanao imekuwa kinyume,mama ameondoka umebaki wewe ila amini usiamini anatamani walau mama angekuwepo wewe uwe umeondoka(hapa natania)

Mahusiano yako na mwanao akiwa mtu mzima yanategemea ukaribu wako na yeye saizi,sio ukaribu wa kupiga simu,jukumu la kulea mwanao ni lako ww sio la bibi

Baada ya kusema hayo nguvu ya maamuzi inabaki kwako
mkuu ahsante sana sana!
hizo paragraphs za kati hapo zimenigusa sana..........itoshe tu kusema kuwa nimekuelewa sana kiongozi!!!
 
Kama ni mm, naiacha situation iendelee ilivyo. Mtoto wa kambo, kwa kuwa ulimpenda mama yake na ulimuoa ukijua kabisa anaye, mtunze tu. Yote ya Mungu, huenda akakufaa baadaye , huwezijua.

Kuhusu watoto hao wawili, kwa point moja tu kuwa WANAMPA KAMPANI KUMBWA MAMA, nitawaacha huko huko na kutuma ninachoweza kuwasaidia huko huko.
mm pia nimewaza wanaishije kwa tabu kwa mama yake, inamaana hamtunzi mama yake inavyotakiwa. angefanya hayo hakuna tabu hapo
 
Imenipa ugumu kidogo kufikiria ila nmepata majibu haya hope yatakusaidia.

Kama upo mjini na umepanga hamia sehem yenye shule nzuri then kawachukue wale watoto kwa bibi wote wawili uishi nao.

Bibi yao au mama yako nenda kaongee nae muelezee vizuri unavyojiskia naamini yeye kama mzazi atakuelewa na kukuruhusu uwachukue kwa moyo mmoja. Swala la upweke atavumilia tu na kila likizo watoto wataenda kukaa na bibi yao kumpa kampan kwa muda.
 
Kuna kitu kigumu ambacho nahisi wanaume wengi hushindwa kuoa single mother kama kufikiria kuwa watoto wataishi vipi,je hakuta kuwa na manyanyaso, wanawake wengi huwa hawapendi wanawake wa wenzio hiyo ipo wazi na haipingiki,

Achilia mbali sisi wanaume tunaweza mprnda mtoto ambaye mwanamke amekuja naye ila mwanamke hawezi mpenda mtoto wa mme wake,
Mpaka hapo nashindwa nikushauri vipi maana najaribu kuvaa viatu vyako nashindwa kabisa,

Ningekushauri uwalete wanao kutoka kwa bibi yao lakini moto watakao kutana nao huku kwa mama yao mdogo sio wa kitoto, nimeyashuhudia hayo kwa familia kama hizo ingawa hapa kwetu jirani kuna familia mbayo huyo mama upendo anaowapa watoto wa mme wake hata watoto wake sidhani kama wanaupata, Yaani anawapenda watoto wa mwanamke mwenzie balaa na ukizingatia mama yao alisha fariki,

Huyu mama amekuwa mfano wa kuigwa hapa mtaani kwetu, yaani huyu mama nashindwa nimuelezeje, amewatuza tangu wakiwa wadogo mpaka sasa baadhi wamesha olewa,
 
Ushauri tafadhali!

Umeoa mke mwenye mtoto na unaishi naye huyo mtoto ukihudumia huduma zote!!

Huko nyumbani nawe una mtoto pia yuko kwa bibi yake (mama yako) anaishi na kusoma, mama wa mtoto wako ametangulia mbele ya haki.

Hapo kwa bibi yake anaishi na mtoto wa kaka yako (dada yake) wanaofanana umri, na historia ikiwemo ya kufiwa mama. hawa watoto wamekuwa kama mapacha, hawatenganishiki.

Ukinunua kitu lazima uwanunulie wote, ukitaka akutembelee mtoto wako bila huyo mwingine basi lazima utaonekana mbaguzi na hauko sawa na huyo utakayemuacha atakuwa kwenye msongo wa mawazo sana.

Maisha ya kuishi kwa bibi yana changamoto zake za hapa na pale; huduma hazitoshelezi, kukosa hela ya shule, kukosa vitafunwa, kukosa nguo, kutoshiba, kutokula unachotaka n.k. Umbali kati yako na mtoto huchangia zaidi changamoto hizi.

Uwezo wako hautoshi kuhudumia kwa kiwango sawa pande hizi mbili, frankly, upande wako na mkeo unapata huduma bora zaidi.

Katikati ya changamoto hizi kwa mtoto wako wa kumzaa, mtoto wako wa kambo unayeishi nae anakula hadi anasaza, anaoga anavyotaka, anapata 200 au zaidi ya kutumia shule kila siku, ananyosha kwa umeme wako kila siku, anapendeza, ananawiri kwa huduma.

Kama nilivyoeleza juu, wako ni tofauti kwani unyoshaji hufanyika kwa pasi ya mkaa, ulaji si wa kuamua, kukosa hela na vitafunwa ni jambo la kawaida, kulala na mlo wa ugali usiku ni kawaida n.k.

Unafikiria kumhamisha na kumleta unakoishi, lkn kuna changamoto hizi zinakutatiza;

1. Shule ya msingi iliyopo eneo lako ni mbovu kuliko huko kwa bibi anakoishi - walimu wachache, ufaulu si wa kuridhisha

2. Ukimhamisha huyo basi kuna uwezekano mkubwa ukalazimika kumhamisha na huyo mwenzie anayeishi nae. Nae ni mkiwa na anahitaji msaada; kaka yako hali si nzuri na yuko mbali huko katika kuhangaika na maisha.

3. Bibi (mama yako) nae ni changamoto nyingine kwani hao watoto ndo kampani yake kuu, upweke atakaojisikia ukiwatoa si wa nchi hii.

Kama binadamu, dukuduku fulani linajaa kila siku kifuani kwamba mtoto asiye wangu anafaidi vyangu huku wangu akihangaika, inafikia kipindi mpaka unamuota binti yako kwa mawazo. Hisia za kukosa baraka kwa Mungu kwa hili zinaanza kukujia kichwani maana unaona kama unamuonea huyu mtoto!!

Mawazo yenu wadau katika hili.......
mwambie mke wako unataka kwenda kumchukua mtoto mje muishi nae kama mnavyoishi na wa kwake!
 
Back
Top Bottom