Ushauri tafadhali!
Umeoa mke mwenye mtoto na unaishi naye huyo mtoto ukihudumia huduma zote!!
Huko nyumbani nawe una mtoto pia yuko kwa bibi yake (mama yako) anaishi na kusoma, mama wa mtoto wako ametangulia mbele ya haki.
Hapo kwa bibi yake anaishi na mtoto wa kaka yako (dada yake) wanaofanana umri, na historia ikiwemo ya kufiwa mama. hawa watoto wamekuwa kama mapacha, hawatenganishiki.
Ukinunua kitu lazima uwanunulie wote, ukitaka akutembelee mtoto wako bila huyo mwingine basi lazima utaonekana mbaguzi na hauko sawa na huyo utakayemuacha atakuwa kwenye msongo wa mawazo sana.
Maisha ya kuishi kwa bibi yana changamoto zake za hapa na pale; huduma hazitoshelezi, kukosa hela ya shule, kukosa vitafunwa, kukosa nguo, kutoshiba, kutokula unachotaka n.k. Umbali kati yako na mtoto huchangia zaidi changamoto hizi.
Uwezo wako hautoshi kuhudumia kwa kiwango sawa pande hizi mbili, frankly, upande wako na mkeo unapata huduma bora zaidi.
Katikati ya changamoto hizi kwa mtoto wako wa kumzaa, mtoto wako wa kambo unayeishi nae anakula hadi anasaza, anaoga anavyotaka, anapata 200 au zaidi ya kutumia shule kila siku, ananyosha kwa umeme wako kila siku, anapendeza, ananawiri kwa huduma.
Kama nilivyoeleza juu, wako ni tofauti kwani unyoshaji hufanyika kwa pasi ya mkaa, ulaji si wa kuamua, kukosa hela na vitafunwa ni jambo la kawaida, kulala na mlo wa ugali usiku ni kawaida n.k.
Unafikiria kumhamisha na kumleta unakoishi, lkn kuna changamoto hizi zinakutatiza;
1. Shule ya msingi iliyopo eneo lako ni mbovu kuliko huko kwa bibi anakoishi - walimu wachache, ufaulu si wa kuridhisha
2. Ukimhamisha huyo basi kuna uwezekano mkubwa ukalazimika kumhamisha na huyo mwenzie anayeishi nae. Nae ni mkiwa na anahitaji msaada; kaka yako hali si nzuri na yuko mbali huko katika kuhangaika na maisha.
3. Bibi (mama yako) nae ni changamoto nyingine kwani hao watoto ndo kampani yake kuu, upweke atakaojisikia ukiwatoa si wa nchi hii.
Kama binadamu, dukuduku fulani linajaa kila siku kifuani kwamba mtoto asiye wangu anafaidi vyangu huku wangu akihangaika, inafikia kipindi mpaka unamuota binti yako kwa mawazo. Hisia za kukosa baraka kwa Mungu kwa hili zinaanza kukujia kichwani maana unaona kama unamuonea huyu mtoto!!
Mawazo yenu wadau katika hili.......