Naomba Ushauri na Saa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba Ushauri na Saa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlenge, Mar 2, 2010.

 1. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #1
  Mar 2, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Kusemaga ule ukweli,

  Zamani nilipokuwa nasikia 'serikali ina mpango kamambe wa...' (fill in the blanks: 'maji kwa wote ifikapo mwaka 2000; 'afya kwa wote ifikapo mwaka 1990'; 'Structural Adjustment Program'; 'Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano' ), nilikuwa na dhana kwamba kweli nchi iko serious kujitahidi kufikia hayo malengo, na iwapo hayatafikiwa, basi wahusika duara watajisikia huzuni, n.k.

  Hivi sasa, baada ya 'uzoefu wa miaka mingi', ninaposikia lolote lenye mwelekeo huo, I take it "with grain of salt".

  MKUKUTA: Huo ni mradi wa kutumia hela 'za World Bank' kuandaa makabrasha na masemina.
  Kilimo Kwanza: Maneno mazuri ya kuelekea kwenye uchaguzi.
  MKURABITA: Pesa zimetolewa na 'wafadhili 'kuandaa document hiyo na kuripoti 'mafanikio' yake.
  "Maisha bora kwa Kila Mtanzania": Kampeni ya Uchaguzi.
  Sekondari za kata: Njia nyingine ya kutumia mkopo wa World Bank / IMF...

  Nimejiwekea 'embargo' ya kusikiliza redio na kusoma magazeti yenye habari za nyumbani, kwa vile karibu kila habari ni kama inathibitisha nadharia ya hapo juu.
  Ndio maana hata hapa JF tunaposti na kusoma mada kama njia mojawapo ya kurelieve pressure za siku, ni aina fulani ya 'entertainment'. I anticipate, despite all the noises, nothing will change as a result. Ni sawa na kelele za chura kisimani... watu wanaendelea kujichotea maji tani yao...

  Kwa ufupi, kama alivyoniambia rafiki yangu mmoja, sasa hivi sera inayotamba Tanzania ni MKUKUBI: Mpango wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini BInafsi. Mengine yote maneno tu yanayosemwa kama sehemu ya kazi.
   
 2. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kichwa cha habari hakijakaa sawa. Unaomba Ushauri na Saa. Unaomba ushauri na saa ipi, ya mkononi, mezani, ukutani au saa ipi ????? Sema....... "Naomba Ushauri Nasaha". Upo wakwetu, Kiswahili ni lugha ya Taifa bwana. ​
   
 3. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2010
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,622
  Likes Received: 1,093
  Trophy Points: 280
  nilipokuwa nasoma sekondari kuna swali lilikuwa linaulizwa hivi, je kichwa cha habari kinasadifu yaliyomo kwenye kitabu? jibu ni NO
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Umesahau ile ..KILIMO KWANZA!!
   
 5. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #5
  Mar 2, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Mzee Kibiongo, ndio nataka Saa pia, siyo ushauri peke yake.

  Mnyikungu, inabidi uangalie 'between the lines'
   
 6. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #6
  Mar 2, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  PakaJimmy, (Where is MbwaTom, BTW?)

  Palikuwaga na katuni inaonyesha kuku, ubavuni kaandikwa 'SIRIKALI', kataga yai "MKUKUTA", "MKURABITA", na mayai mengine, halafu anasema, "Na Bado!"
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...