Naomba Ushauri na Saa

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Kusemaga ule ukweli,

Zamani nilipokuwa nasikia 'serikali ina mpango kamambe wa...' (fill in the blanks: 'maji kwa wote ifikapo mwaka 2000; 'afya kwa wote ifikapo mwaka 1990'; 'Structural Adjustment Program'; 'Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano' ), nilikuwa na dhana kwamba kweli nchi iko serious kujitahidi kufikia hayo malengo, na iwapo hayatafikiwa, basi wahusika duara watajisikia huzuni, n.k.

Hivi sasa, baada ya 'uzoefu wa miaka mingi', ninaposikia lolote lenye mwelekeo huo, I take it "with grain of salt".

MKUKUTA: Huo ni mradi wa kutumia hela 'za World Bank' kuandaa makabrasha na masemina.
Kilimo Kwanza: Maneno mazuri ya kuelekea kwenye uchaguzi.
MKURABITA: Pesa zimetolewa na 'wafadhili 'kuandaa document hiyo na kuripoti 'mafanikio' yake.
"Maisha bora kwa Kila Mtanzania": Kampeni ya Uchaguzi.
Sekondari za kata: Njia nyingine ya kutumia mkopo wa World Bank / IMF...

Nimejiwekea 'embargo' ya kusikiliza redio na kusoma magazeti yenye habari za nyumbani, kwa vile karibu kila habari ni kama inathibitisha nadharia ya hapo juu.
Ndio maana hata hapa JF tunaposti na kusoma mada kama njia mojawapo ya kurelieve pressure za siku, ni aina fulani ya 'entertainment'. I anticipate, despite all the noises, nothing will change as a result. Ni sawa na kelele za chura kisimani... watu wanaendelea kujichotea maji tani yao...

Kwa ufupi, kama alivyoniambia rafiki yangu mmoja, sasa hivi sera inayotamba Tanzania ni MKUKUBI: Mpango wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini BInafsi. Mengine yote maneno tu yanayosemwa kama sehemu ya kazi.
 
Kichwa cha habari hakijakaa sawa. Unaomba Ushauri na Saa. Unaomba ushauri na saa ipi, ya mkononi, mezani, ukutani au saa ipi ????? Sema....... "Naomba Ushauri Nasaha". Upo wakwetu, Kiswahili ni lugha ya Taifa bwana.​
 
nilipokuwa nasoma sekondari kuna swali lilikuwa linaulizwa hivi, je kichwa cha habari kinasadifu yaliyomo kwenye kitabu? jibu ni NO
 
Mzee Kibiongo, ndio nataka Saa pia, siyo ushauri peke yake.

Mnyikungu, inabidi uangalie 'between the lines'
 
PakaJimmy, (Where is MbwaTom, BTW?)

Palikuwaga na katuni inaonyesha kuku, ubavuni kaandikwa 'SIRIKALI', kataga yai "MKUKUTA", "MKURABITA", na mayai mengine, halafu anasema, "Na Bado!"
 
Back
Top Bottom