Naomba ushauri: Mpangaji wangu msumbufu kulipa kodi nataka nifungie vitu vyake

Usimfanyie hivyo, mpe muda andikishiana nae kwa mjumbe kwamba hadi kufikia let say Disemba mosi ulipe pesa yangu laa nitafunga chumba na nitazuia vitu vyako hadi hapo utakapokuja kulipa pesa yangu.

😂 😂 😂
 
Sawa kabisa mimi jamaa alishindwa kunilipa shg. 1,500,000/= . akahama na sikumdai mpaka leo. Nyumba ikapata mpangaji mwingine na maisha yanaendelea. Hakuna haja ya kugombana maana akihama nyumba ipo tu.
Exactly, Cha msingi hawezi ondoka na jengo lako
 
Niliwahi kufikwa na hili tatizo, nilipanga geto sehemu nikalipa kodi miezi mitatu, baada ya miezi mitatu kuisha hali yangu kifedha ikawa mbaya sana, ikafikia nikawa nadaiwa miezi sita, mama mwenye nyumba akawa kila siku anaomba hela yake....nikawa narudi usiku sana alafu nawahi kutoka alfajiri kabla hajaamka, siku moja nimerudi usiku nikakuta kikaratasi ndani ya mlango kaandika hivi "NIMEKUCHOKA NAKUPA SIKU 3 UHAME, NA HIYO KODI NINAYOKUDAI NIMEKUSAMEHE" nikalala, asubuhi kama kawaida yangu alfajiri nikasepa....akili ikaanza kufikiri...mapema mida ya saa 9 alasiri nikarudi geto, nikamkuta anafua nikamwambia naomba kuongea nawe...nikamwambia mama naomba unikopeshe laki 3 naweka bondi vyombo vyangu, naenda nyumbani kuna matatizo, akakataa, hiyo yote ilikuwa kum-neutralize asinidai sana, nikaanza kumlipa kidogo kidogo hadi nikamaliza deni

Usiombe kudaiwa kodi na wakati kula tu ni shida...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hamna haja ya kufungia vitu vyake,apo utatafuta uhasama na mpangaji wako,cha kufanya mpe time au mpe notice,
 
huna haja ya kufungia vitu vyake....wewe ni binadamu...usiishi ukijiongezea MAADUI.....ongea nae muyamalize....inawezekana...kuna wakati hali inakuwaga ngumu sana....
 
Kuna jamaa yangu alipanga nyumba akakutana na mpangaji mtata ,miezi 6 ikapita bado anakwepa kulipa,akamwambia ondoka bado anasema ili niondoke lazima unipe notice . Mwenye nyumba alichofanya ni kumwita mjumbe mbele ya jamaa akasema nataka kurepair nyumba yangu aondoke ,mafundi wakaanza kutoa bati,chumba ikawa wazi kwa juu halafu akaacha hapo hapo ,mvua ikija au jua likiwaka watajua wenyewe au akiibiwa atajijua ..mbona aliondoka mwenyewe

Anaweza akawa mlipaji mzuri akakumbana na changamoto za maisha.
Option samehe tu mwambie akuachie nyumba pangisha mwingine, usifungie vitu vyake,utauza nyumba yako Ili umlipe fidia
 
Dah sema wenye nyumba wanakuwaga wababe sana huwa wanaona wameyapatia maisha. Halafu watoto wao wakina kuwa wakubwa wanapitia madhila Yale Yale waliyopitia wapangaji wao. Kama unaweza msamehe tu nyumba hayiami utapata mpangaji mwingine.
Ni rahisi kusema hivyo.Pia wapangaji wengi ukimuachia mda mrefu labda mwaka au miezi 6.Siku akizipata pesa utoroka uona bora akapange kwingine kuliko kulipa deni.
Mpangaji akipita miezi 3 bila kulipa kubali hasara akuachie chumba chako tafuta mpangaji mwingine.
KILA biashara Ina hasara
 
Usimfanyie hivyo, mpe muda andikishiana nae kwa mjumbe kwamba hadi kufikia let say Disemba mosi ulipe pesa yangu laa nitafunga chumba na nitazuia vitu vyako hadi hapo utakapokuja kulipa pesa yangu.
Akifanya hivyo atakuta chumba kitupu mkuu
 
Ngojea nijaribu kufanya hivyo boss,japo nipo mbali nae,hofu yangu hasije kuhama usiku

Mkuu na Mimi pia Nina nyumba za kupangisha apartments za Chumba Sebule choo na jiko.
Nakutanaga Sana na changamoto Kama hiyo yako.
Nakushauri Fanya kwenda ofisi ya Mtendaji wa Mtaa iliyopo hiyo nyumba yako uliyompangisha huyo ndugu anayeshindwa kulipa kodi ukapeleke shauri lako la yeye kushindwa kulipa kodi yako ya pango jitahidi uonane na Mtendaji mwenyewe au Mwenyekiti wa Mtaa, achana na hao sijui wajumbe.
Naamini shauri lako litafanyiwa kazi ipasavyo.
 
Akifanya hivyo atakuta chumba kitupu mkuu

Ni heri tu ahame atafute mpangaji mwengine amlipe kodi.
Nakumbuka nishakuwaga na Mpangaji akapata changamoto ya ugonjwa alikonda jamaa hadi kitaa wakawa wananiambia yule mpangaji wako ameungua.
Jamaa alichoka kazi zake zikakwama mke wake akaondoka na vitu Kama vyote akaenda kwao.
Kodi yake ilipoisha akawa hana uwezo wa kulipa, ukapita mwezi wa 1,2,3 ananipiga sound ila nilikuwa na Mimi namuonea huruma flani kodi yake ilikuwa laki 2 kwa mwezi.
Nikaona isiwe tabu nikampeleka kwa Mtendaji wa Mtaa, akaitwa kwa barua tukaenda jamaa akasema hayupo vizuri na pia ni mgonjwa ,kaenda hospital I ugonjwa hauonekani.
Dah unaambiwa alikuwa anatia huruma.
Mtendaji akamwandika notisi ya mwezi ahame na anilipe kodi anazodaiwa au alipe kodi Kama kawaida ya miezi 6.
Mwezi wa notisi ukaisha jamaa hana kitu nikaenda kumripoti kwa Mtendaji ,Mtendaji mwenyewe akawa anamuonea huruma jinsi anavyoumwa yaani we acha .
Dunia Ina majaribu Sana, Mtendaji anamkoromea jamaa anamwambia kesho nakuja na mgambo kukutoa kwenye hiyo nyumba jamaa anabaki analia , anaambiwa haya nenda kesho ujiandae tunakuja kukutoa.
Mtendaji ananiambia nibaki ,Mtendaji ananiambia nimsikilizie jamaa ni mgonjwa akija kumtoa anaweza asieleweke na jamii. Na Mimi nikawa namkubalia tumsikilizie ikawa ndio hivyo had ikafika miezi 4 Mtendaji anasita kumtoa.
Kuna siku na hasira zangu nikapiga zangu konyagi za kutosha nikasema wacha nikamtoe yule Mpangaji Mimi mwenyewe Mtendaji anazingua.
Nikaenda pale kwangu had I anapoishi nasikia ndani jamaa anakohoa kugonga anauliza wewe nani namjibu mwenyewe nyumba ananiambia ingia ndani.
Dah kuingia ndani nikakuta jamaa alikuwa anatapika kishenzi ndani ya ndoo nyumba chafu jamaa anakitanda nagodoro tu nikamwambia we jamaa unataka kufia hapa kwangu nini. Halafu na kodi hulipi unataka kunipa mzigo nini.
Unaambiwa jamaa akawa analia akaniomba nauli aende kijijini kwao.
Nikashikwa na huruma nikampa elfu hamsini nikamwambia na kodi yangu nimekusamehe .
Kweli jamaa kesho yake tu akatoa vitu vyake akataka kuviuza akakosa mteja akasepa akaviacha nje.
Ikabidi niviweke stoo vitu vyake nikapiga rangi nyumba nikapangisha mtu mwingine.
Baada ya Kama mwaka jamaa alikuja kunisalimia Bahati nzuri akanikuta alikuwa amenawiri amepona yupo fresh,
Aliniambia alivyokwenda kijijini kwao ikaonekana alikuwa ametupiwa majini na ndugu yake hivyo wakamfanyia matibabu akapona.
Jamaa alinishukuru Sana akaniambia amekuja kunilipa kodi niliyokuwa na mdai Yaani bila kutegemea nikala laki nane.
jamaa hadI Leo rafiki yangu.
Kwenye haya maisha kuna watu wanapitia mitihani mikubwa Sana si vyema kumcheka,kumdharau au kumnyanyasa mtu ni swala la kumshukuru Mungu kila wakati Kama amekujalia kuepukana na dhiki ,karaha, na magonjwa.
 
Wakuu habari:

Unajua hizi nyumba za kupangisha zina matatizo Sana,mtu umetumia pesa kibao kuwekeza,Bado Tena unakuja kupangisha majitu ambayo hayajielewi.

Ni hivi, Kuna mpangaji wangu now anakaribia miaka miwili kama na nusu kwenye mabanda yangu, Sasa huyu tangu kipindi cha Corona ya kwanza hile mambo yake hayajakaa sawa, nilikuwa namdai milioni , alilipa laki nne Bado laki sita, Sasa saundi zimekuwa nyingi, mara subiri kidogo, mara week ijayo, mara mwisho wa mwezi ,

Sasa nilichofikiria huyu bwana mdogo labda nikuzuia vitu vyake vyote,na kufunga nyumba Hadi hapo atakaponilipa pesa yangu,

Sasa je nikiwa na mjumbe siinatosha kiushaidi kwenda kumtimua hili nifunge nyumba Hadi atakapolipa Deni!!?

Au wazee wenzangu mwashaurije katika hili, maana sitaki kutumia ubabe sheria itanibana
Mwachie bill za umeme awe analipa yeye hadi pale pesa yako itakapoisha.
 
Ni heri tu ahame atafute mpangaji mwengine amlipe kodi.
Nakumbuka nishakuwaga na Mpangaji akapata changamoto ya ugonjwa alikonda jamaa hadi kitaa wakawa wananiambia yule mpangaji wako ameungua.
Jamaa alichoka kazi zake zikakwama mke wake akaondoka na vitu Kama vyote akaenda kwao.
Kodi yake ilipoisha akawa hana uwezo wa kulipa, ukapita mwezi wa 1,2,3 ananipiga sound ila nilikuwa na Mimi namuonea huruma flani kodi yake ilikuwa laki 2 kwa mwezi.
Nikaona isiwe tabu nikampeleka kwa Mtendaji wa Mtaa, akaitwa kwa barua tukaenda jamaa akasema hayupo vizuri na pia ni mgonjwa ,kaenda hospital I ugonjwa hauonekani.
Dah unaambiwa alikuwa anatia huruma.
Mtendaji akamwandika notisi ya mwezi ahame na anilipe kodi anazodaiwa au alipe kodi Kama kawaida ya miezi 6.
Mwezi wa notisi ukaisha jamaa hana kitu nikaenda kumripoti kwa Mtendaji ,Mtendaji mwenyewe akawa anamuonea huruma jinsi anavyoumwa yaani we acha .
Dunia Ina majaribu Sana, Mtendaji anamkoromea jamaa anamwambia kesho nakuja na mgambo kukutoa kwenye hiyo nyumba jamaa anabaki analia , anaambiwa haya nenda kesho ujiandae tunakuja kukutoa.
Mtendaji ananiambia nibaki ,Mtendaji ananiambia nimsikilizie jamaa ni mgonjwa akija kumtoa anaweza asieleweke na jamii. Na Mimi nikawa namkubalia tumsikilizie ikawa ndio hivyo had ikafika miezi 4 Mtendaji anasita kumtoa.
Kuna siku na hasira zangu nikapiga zangu konyagi za kutosha nikasema wacha nikamtoe yule Mpangaji Mimi mwenyewe Mtendaji anazingua.
Nikaenda pale kwangu had I anapoishi nasikia ndani jamaa anakohoa kugonga anauliza wewe nani namjibu mwenyewe nyumba ananiambia ingia ndani.
Dah kuingia ndani nikakuta jamaa alikuwa anatapika kishenzi ndani ya ndoo nyumba chafu jamaa anakitanda nagodoro tu nikamwambia we jamaa unataka kufia hapa kwangu nini. Halafu na kodi hulipi unataka kunipa mzigo nini.
Unaambiwa jamaa akawa analia akaniomba nauli aende kijijini kwao.
Nikashikwa na huruma nikampa elfu hamsini nikamwambia na kodi yangu nimekusamehe .
Kweli jamaa kesho yake tu akatoa vitu vyake akataka kuviuza akakosa mteja akasepa akaviacha nje.
Ikabidi niviweke stoo vitu vyake nikapiga rangi nyumba nikapangisha mtu mwingine.
Baada ya Kama mwaka jamaa alikuja kunisalimia Bahati nzuri akanikuta alikuwa amenawiri amepona yupo fresh,
Aliniambia alivyokwenda kijijini kwao ikaonekana alikuwa ametupiwa majini na ndugu yake hivyo wakamfanyia matibabu akapona.
Jamaa alinishukuru Sana akaniambia amekuja kunilipa kodi niliyokuwa na mdai Yaani bila kutegemea nikala laki nane.
jamaa hadI Leo rafiki yangu.
Kwenye haya maisha kuna watu wanapitia mitihani mikubwa Sana si vyema kumcheka,kumdharau au kumnyanyasa mtu ni swala la kumshukuru Mungu kila wakati Kama amekujalia kuepukana na dhiki ,karaha, na magonjwa.
Ila we jamaa una roho ngumu kumdai pesa mtu anaumwa looh,
 
Back
Top Bottom