Naomba ushauri: Mpangaji wangu msumbufu kulipa kodi nataka nifungie vitu vyake

Mzee makoti

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
2,571
3,055
Wakuu habari:

Unajua hizi nyumba za kupangisha zina matatizo sana, mtu umetumia pesa kibao kuwekeza, bado tena unakuja kupangisha majitu ambayo hayajielewi.

Ni hivi, kuna mpangaji wangu now anakaribia miaka miwili kama na nusu kwenye mabanda yangu, sasa huyu tangu kipindi cha Corona ya kwanza hile mambo yake hayajakaa sawa, nilikuwa namdai milioni, alilipa laki nne Bado laki sita, sasa saundi zimekuwa nyingi, mara subiri kidogo, mara week ijayo, mara mwisho wa mwezi.

Sasa nilichofikiria huyu bwana mdogo labda nikuzuia vitu vyake vyote, na kufunga nyumba Hadi hapo atakaponilipa pesa yangu.

Sasa je nikiwa na mjumbe siinatosha kiushaidi kwenda kumtimua hili nifunge nyumba Hadi atakapolipa deni?

Au wazee wenzangu mwashaurije katika hili, maana sitaki kutumia ubabe sheria itanibana
 
Busara ni kumpa notes alipe ama aondoke nyumba iwe wazi aje mwingine,ukiwa mwenye nyumba ndani ya miezi3 ukiona mtu hajalipa Basi ni vyema ukamtaka muachane tu maana hata Maisha hubadilika anaweza tafuta nyumba atayoimudu kwa muda huu, iwe ni nje ya mji kabisa ambazo kodi ni nafuu sana au maeneo kama mabibo, Manzese, Tandale ,kigogo,buguruni ama Mbagala anaweza pata chumba na sebule KWA 40000 tu na akajihifadhi na kujipanga upya.

Nenda KWA step pia maana naye ni binadamu na anahaki zake,ukikosea tu anaweza kukubadilikia na kukuhamza maana mtu akishmbuliwa na Tatzo la kodi hupatwa na stress sana,hata me pia
 
Mzee kuwa makini sanaa....mjumbe ni bure tu mbele ya sheria

Kuna kisa kama hiki kilitokea

Jamaa alikuwa anadaiwa laki 4 na mwenye nyumba ,mwenye nyumba akamchukua mjumbe wakafunga nyumba ,yule mpangaji akasafiri zake wala hakuhaingaika na kitu chchte

Badae mwenye nyumba akaona nyumba yake ipo tu watu wanakuja kuulizia nyumba lkn ndo hvyo kuna vitu vya jamaa.

Akamwita mjumbe wakavunja na kuadika mali walizokuta ndani wakavipakia store, wakapangisha nyumbaa.

eeeeeh hilo ndo likawa kosa kubwa kwao

Jamaa alivyorudi na kukuta ile hali hakuongea na mtu akanyoosha mahakamani na kufungua kesi ,na katika ile kesi alidai kulikuwa na fedha taslimu million 5 kwenye bahasha ambazo zilikiwa ndani ya nyumba

Mwenye nyumba na mjumbe waliipata kisawasawa walilipa million 6 na laki 3 kwa awamu 3 huku mahakama ikaweka amri ya kuvirejesha vitu vyake ndani na apewe muda wa mwezi mmoja (notice) ndo ahame

Jamaa akabeba hela wala hakurudi kwenye hyo nyumba akasepa na kitita akaishiaa zake


KUWA MAKINI SANAA ..UKIKUTANA NA MTU ANAYEIJUA SHERIAA UTAIPATA VZR
 
Usimfanyie hivyo, mpe muda andikishiana nae kwa mjumbe kwamba hadi kufikia let say Disemba mosi ulipe pesa yangu laa nitafunga chumba na nitazuia vitu vyako hadi hapo utakapokuja kulipa pesa yangu.
Sasa akianza kuhamisha vitu vya thamani mwezi ukifika akuachie masufuria.Hapo ni kumkazia sa hivi haina kusubiri,deni linazidi kuongezeka na uwezo hana.
 
mzee kuwa makini sanaa....mjumbe ni bure tu mbele ya sheria ...

kuna kisa kama hiki kilitokea
jamaa alikuwa anadaiwa laki 4 na mwenye nyumba ,mwenye nyumba akamchukua mjumbe wakafunga nyumba ,yule mpangaji akasafiri zake wala hakuhaingaika na kitu chchte ,

badae mwenye nyumba akaona nyumba yake ipo tu watu wanakuja kuulizia nyumba lkn ndo hvyo kuna vitu vya jamaa...

akamwita mjumbe wakavunja na kuadika mali walizokuta ndani wakavipakia store ,wakapangisha nyumbaa....

eeeeeh hilo ndo likawa kosa kubwa kwao,

jamaa alivyorudi na kukuta ile hali hakuongea na mtu akanyoosha mahakamani na kufungua kesi ,na katika ile kesi alidai kulikuwa na fedha taslimu million 5 kwenye bahasha ambazo zilikiwa ndani ya nyumba..

mwenyenyumba na mjumbe waliipata kisawasawa ..walilipa million 6 na laki 3 kwa awamu 3 huku mahakama ikaweka amri ya kuvirejesha vitu vyake ndani na apewe muda wa mwezi mmoja (notice) ndo ahame ....

jamaa akabeba hela wala hakurudi kwenye hyo nyumba akasepa na kitita akaishiaa zake


KUWA MAKINI SANAA ..UKIKUTANA NA MTU ANAYEIJUA SHERIAA UTAIPATA VZR
ila huyo jamaa hawezi maliza maosha bila kukumbana na makubwa zaidi ya hayo aliyo wafanyia wenzie japo sio hapo kwa hapo hata akizeeka yaani muda wowote tu kulia huwa kupokezana hajui tu.
 
Mkuu kama unaweza kuliko kugombana na jamaa bora mwambie akupa hata kidogo kidogo. Hata laki mbili mbili au hata moja moja. Then akimaliza mkataba mwambie asepe zake.

Msaidie tu hivyo mkuu.
 
Usimfanyie hivyo, mpe muda andikishiana nae kwa mjumbe kwamba hadi kufikia let say Disemba mosi ulipe pesa yangu laa nitafunga chumba na nitazuia vitu vyako hadi hapo utakapokuja kulipa pesa yangu.
hapo waandikishane mpaka miezi kadhaa huku ameweka dhamana ya hivo vitu vyake ,bila hivo atamtoroka usiku na kusomba vitu vyake na mwenye hasara atakuwa ni mwenye nyumba
 
Kuna jamaa yangu alipanga nyumba akakutana na mpangaji mtata ,miezi 6 ikapita bado anakwepa kulipa,akamwambia ondoka bado anasema ili niondoke lazima unipe notice . Mwenye nyumba alichofanya ni kumwita mjumbe mbele ya jamaa akasema nataka kurepair nyumba yangu aondoke ,mafundi wakaanza kutoa bati,chumba ikawa wazi kwa juu halafu akaacha hapo hapo ,mvua ikija au jua likiwaka watajua wenyewe au akiibiwa atajijua ..mbona aliondoka mwenyewe
 
Dah sema wenye nyumba wanakuwaga wababe sana huwa wanaona wameyapatia maisha. Halafu watoto wao wakina kuwa wakubwa wanapitia madhila Yale Yale waliyopitia wapangaji wao. Kama unaweza msamehe tu nyumba hayiami utapata mpangaji mwingine.
 
Wakuu habari:

Unajua hizi nyumba za kupangisha zina matatizo Sana,mtu umetumia pesa kibao kuwekeza,Bado Tena unakuja kupangisha majitu ambayo hayajielewi.

Ni hivi, Kuna mpangaji wangu now anakaribia miaka miwili kama na nusu kwenye mabanda yangu, Sasa huyu tangu kipindi cha Corona ya kwanza hile mambo yake hayajakaa sawa, nilikuwa namdai milioni na laki mbili, alilipa laki nne Bado laki sita, Sasa saundi zimekuwa nyingi, mara subiri kidogo, mara week ijayo, mara mwisho wa mwezi ,

Sasa nilichofikiria huyu bwana mdogo labda nikuzuia vitu vyake vyote,na kufunga nyumba Hadi hapo atakaponilipa pesa yangu,

Sasa je nikiwa na mjumbe siinatosha kiushaidi kwenda kumtimua hili nifunge nyumba Hadi atakapolipa Deni!!?

Au wazee wenzangu mwashaurije katika hili, maana sitaki kutumia ubabe sheria itanibana
Mkuu sasa kulikuwa na haja gani kuja kunitangaza huku? Chumba chenyewe banda tunaishi na panya, nzi mchana mbu usiku. Acha hizo bana duniani tunapita.
 
Back
Top Bottom