Naomba ushauri kuhusu ndoto hii

Naomba ushauri kuhusu ndoto hii

wainga

Member
Joined
Mar 30, 2017
Posts
73
Reaction score
67
Habari zenu?

Kwanza mimi sio muandishi wala mchangiaji sana wa mada zinazoletwa humu jukwaaan, kwahiyo naomba hicho kisiwe kigezo cha kutonipa ushauri!

Mimi naishi Nyanda za juu kusini katika mojawapo za Wilaya zinazolima mpunga.
Sasa leo nimeota ndoto ilinishangaza sana kitu kilochopelekea kuomba ushauri ili muweze pengine kuniambia tafusri yake.

Nimeota niko kijijini napita karibu na choo cha kilabuni nikaona watu wanatoa kinyesi kwenye hicho choo ambacho inaonekana kimejaa.

Lakini wanatoa hicho kinyesi kwa ndoo na kwenda kukimwaga mahali furani,sasa wakati napita karibu na hapo chooni mmojawapo wa hao wabebaji akanimwagia kinyesi kwa kitu kinachoonekana kama bahati mbaya mwili mzima!

Sasa ni kawa nakwenda kutaka kuoga nyumbani kwa babu yangu,lkn ghafula nikatokea mjini ninako ishi.
Huko sasa nikakutana na watu ninao fanya nao kazi wakawa wana kazi ambazo huwa wananipa mimi hizo kazi kuzifanya,lakini wakawa hawanipi kwa sababu niko na huo uchafu!.

Nimeomba huu ushauri kwa sababu ambazo nakumbana nazo kazini kiasi kwamba hii ndoto naona ina akisi hali hiyo

Hii ndoto nimeota usiku wa kuamkia leo!.
 
Jiandaee kufokewana boc jiandae kuonekana we c lolote hapo kazini

Inshu ni zidisha maombi kma muislam swali sna usiku
 
Jibu ni dogo kaka, wewe soon unakua mtu muhimu na wakutegemewa kimaisha, kama ni uongo utanitafuta. Achana na hofu ndoto huja kinyume, kaaakwa amani mtukuze mungu mafanikio yanakuja, ukikaa na mwenye manukato nawe utanukia, aliekupaka hayo manukato ndio dira yako ya kunukia. Vibaya angekupaka perfum halisi ila hio ww kua na amani.
Mungu awe nawe.
 
Huwa nawashangaa sana watu mnaowekea maanani vitu vidogo kama ndoto.

We bhana msimu wa ubwabwa huu! Endelea kula zako ubwabwa huko Mbarali/Madibira. Hii ni ndoto tu. Hivyo unatakiwa kuipuuzia. Maana haina uhalisia wowote ule.
 
Jibu ni dogo kaka, wewe soon unakua mtu muhimu na wakutegemewa kimaisha, kama ni uongo utanitafuta. Achana na hofu ndoto huja kinyume, kaaakwa amani mtukuze mungu mafanikio yanakuja, ukikaa na mwenye manukato nawe utanukia, aliekupaka hayo manukato ndio dira yako ya kunukia. Vibaya angekupaka perfum halisi ila hio ww kua na amani.
Mungu awe nawe.
Hata mimi ndiyo nilivyoelewa. Ndoto yake ina tafsiri ya mafanikio. Watu wanatafsiri ndoto direct kumbe ndoto ni lugha inayotafsiriwa kitofauti sana na lugha yetu hii.
 
Pole sana, utaingia kwenye kesi kubwa sana...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom