Da tall gal
Member
- Oct 29, 2016
- 11
- 9
Mimi ni msichana wa miaka 20 nipo Chuo Kikuu mwaka wa kwanza lakini nilitokea kuanzisha mhusiano na Mwanaume nikiwa form three. Nampenda na nimekuwa mwaminifu kwake toka nilivyoanzisha mahusiano naye.
Lakini yeye alikuwa mbele yangu kimasomo na alivyomaliza kidato cha nne hakufanikiwa kujiunga na kidato cha tano hivyo akaamua kurudia mtihani mara ya pili. Mimi nilivyomaliza kidato cha nne nilifanikiwa kujiunga na kidato cha tano hivyo nikawa nimemwacha hatua kadhaa nyuma.
Matokeo yake yalivyotoka akawa amefeli tena kwa mara ya pili lakinihakukata tamaa akarudia mtihani kwa mara ya tatu. Sasa mimi nipo Mwaka wa kwanza na yeye anasubiri matokeo ya kidato cha nne.
TATIZO NI KWAMBA NIKIMUULIZA MAISHA YETU YA MBELENI HATAKI TUZUNGUMZIE HILO na ninaona kuwa tayari kila mtu anahitji kutimiza malengo yake na mimi nataka nikimaliza chuo niolewe ila atakuwa bado anasoma.
NAOMBENI USHAURI WENU NIFANYEJE?