Naomba ushauri kuhusu dini

Naomba ushauri kuhusu dini

Empress_sheila

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
293
Reaction score
339
Mimi ni Muislam kwa baba na mama na hatuna historia ya dini nyingine labda huko nyuma kabisa ambapo hata bibi zangu hawakuwepo au hawajui, imetokea mimi tu kuupenda ukiristo kiasi ambacho tangu niko form one miaka zaidi ya ishirini kubadili majina yangu na kuwa ya Kikiristo na nilikua nikisema baba yangu mkristo mama yangu ndiyo Muislam.

Bahati mbaya nikiwa form two nilikaa hostel ya waroma kwahivyo nilikuwa napenda wakati mwingine kwenda kanisani japo nilikua sielewi kitu, kuna wakati napotezea naanza kusali kiislam kwasababu dini ya Kiislam naijua nimesoma madrasa nikiwa mdogo na hakuna kitabu cha dini kina kina kinanishinda kusoma na hapo zamani nilikua nikisia mtu anasoma kuruan nalia bila kujua nalilia nini nikawa namwambia mama mbona nie nalia nikiona au kusikia kuruan inasomwa? Mama ananiambia tu inaitwa midadi hiyo.

Nimejikuta tu wanangu sijawapeleka madrasa na shule nimewapeleka shule za kikiristo na sipendi kabisa za kiislam wala madrasa na huwa nawaambia wanangu nendeni kanisani, na utu uzima huu kuna wakati nilipata majanga makubwa nikaona njia sahihi ni kuombewa kanisani nikaenda roma kuombewa ndani ya siku tatu pepo likatoka na nimeendelea kusali kiroma nikiwa nyumbani na natumia maji ya baraka wakati mwingi nahisi kabisa yananisaidia, halafu nikiwa kanisani nina amani zote nachokisema nakielewa nachokisali nakielewa! Naona mahubiri ya father nayaelewa vizuri na hapa nyumbani redio nasikiliza redio Maria tu na naifurahia.

Sasa wakuu nisaidieni hili ni pepo au nini? Je nibadili dini na utu uzima huu? Au nifanyaje nifute historia hii? Yaan sasa hivi ndiyo nazidi kuzama kwenye ukristo kiasi ambacho hata wanangu natamani waanze mafundisho, au kuna sehemu sijielewi?
 
Mimi ni muislam kwa baba na mama na hatuna historia ya dini nyingine labda huko nyuma kabisa ambapo hata bibi zangu hawakuwepo au hawajui, imetokea mimi tu kuupenda ukiristo kiasi ambacho tangu niko form one miaka zaid ya ishirini kubadili majina yangu na kuwa ya kikiristo na nilikua nikisema baba yangu mktisto mama yangu ndiyo muislam, bahat mbaya nikiwa form two nilikaa hostel ya waroma kwahivyo nilikua napenda wakati
Naamini Mungu ni mmoja, kokote unakojisikia kuguswa nako zaidi, fata huko huko.
 
Kwanza nakupa pole sana, umesema umesoma madrasa na unaijua Dini ya kiislamu? Kwa mtu anayeijua Dini ya Kiislam hawezi kuja kuomba msaada hapa jukwaani, naamini wewe ungekuwa msaada kwa wengine kuwaingiza kwenye Uisilamu.

Kama kweli ulichokifanya unakijua na malipo yako utakuwa unayajua baada ya kufa kaburini na siku ya kiaama. Kibaya zaidi unadiriki hata kuwapotosha watoto zako wakati wazazi wako wamekupa kheri zote? Nimejaribu kuandika lakini nashindwa kuuendelea, angalia wanaokupotosha wanakwambia Dini zote ni sawa, wapi na wapi? Nenda kwa wazazi wako ukawaambie kuhusu msimamo wako nadhani watakusaidia zaidi
 
Upo sahihi kabisa ndugu na tena Mungu anataka umjue kupitia Yesu Kristo, endelea kuwa mkristo tena shika imani yako vizuri kabisa nawe utakuwa na amani tele na kuupata ufalme wa mbinguni mwishowe. Ubarikiwe!
 
Kwanza nakupa pole sana,umesema umesoma madrasa na unaijua Dini ya kiislamu?kwa mtu anayeijua Dini ya Kiislam hawezi kuja kuomba msaada hapa jukwaani,naamini wewe ungekuwa msaada kwa wengine kuwaingiza kwenye Uisilamu.

Kama kweli ulichokifanya unakijua na malipo yako utakuwa unayajua baada ya kufa kaburini na siku ya kiaama.Kibaya zaidi unadiriki hata kuwapotosha watoto zako unawaingiza kwenye Ukafiri wakati wazazi wako wamekupa kheri zote? Nimejaribu kuandika lakini nashindwa kuuendelea,angalia wanaokupotosha wanakwambia Dini zote ni sawa,wapi na wapi? Nenda kwa wazazi wako ukawaambie kuhusu msimamo wako nazani watakusaidia zaidi
Usije kwa mkwara mkuu! Nimekuja hapa kuomba ushauri pengine usome tena uelewe! Niko njia panda, hata wewe unayejiita muislam unaweza kuwa kafiri vilevile nadhani unajua kama kwel unaujua huo uislam, sitak kubishana na wewe badala yake kutokana na nilichohadithia hapo nishauri tu.
 
Upo sahihi kabisa ndugu na tena Mungu anataka umjue kupitia Yesu Kristo, endelea kuwa mkristo tena shika imani yako vizuri kabisa nawe utakuwa na amani tele na kuupata ufalme wa mbinguni mwishowe. Ubarikiwe!
Kwasababu zip?
 
Back
Top Bottom