Habarini wana jamvi,
Nina shida kuhusiana na kichwa cha habari husika hapo juu
Iko hivi Miezi 6 iliyo pita nilinunua kiwanja cha makazi maeneo ya Kinyerezi Dar es Salaam,
Baada ya kuwa nimeonyeshwa mipaka ya eneo na michoro ya kiwanja katika ramani ya mipango miji na mhusika wiki moja badae nikaenda ofisi za serekali ya mtaa za eneo husika ili kujiridhisha na mmiliki wa eneo pamoja na uhalali wa kiwanja.
Nakukuta kuwa jamaa anatambulika kama mmiliki halali wa eneo kupitia hati ya serikali ya mitaa na limerasimishwa kama eneo la makazi, nikampigia jamaa simu ilikesho yake tukaandikishane nilipie.
Kesho yake mimi na mashahidi wangu wawili ambao ni ndugu zangu pamoja na mmiliki wa kiwanja na shahidi wake mmoja tukaenda ofisi za mtendaji ili watuandikie hati ya mauziano mimi na mmiliki wa eneo pamoja na mashahidi wetu tuka sign ile document na ikapigwa mihuru na mtendaji.
Baada ya hapo tukatoa copy kadhaa za ile hati ya mauziano na kuacha copy mbili ofisi za mtendaji baada ya hapo tukaenda bank nikamlipa mmiliki wa kiwanja na akanipa ile hati ya mauziano, kila mtu akaendelea na maisha yake sasa shida imekuja juzi nimeenda sight nimekuta kuna jirani yangu mmoja kaweka uzio kwenye eneo ambalo ndio njia ya mimi kuingilia kiwanjani kwangu yani kama ni nyumba itajengwa basi njia ya mimi kuingia nyumbani kwangu itabidi iwe hapo sasa ikabidi nimfate na kumuuliza KULIKONI na jamaa akanitolea ramani yake ya mpango miji ikionyesha kuwa kile kiwanja changu ni kiwanja kisichokuwa na njia na kuwa ile ramani niliyopewa na jamaa aliyeniuzia ni fake japo inafanana asilimia 98 na ramani halisi ya eneo lile kwa kuwa kasoro iliyopo ni hicho kipande cha njia tu ndio kimeeditiwa kutoka kwenye ramani halisia.
Naombeni mnishauri nini naweza kufanya maana nilivyoenda serikali za mitaa nilionyeshwa ramani na nikapewa copy ikionyesha kuwa njia itafika mpaka ndani ya eneo langu kumbe sivyo huyu jamaa kanifanyia usanii.
Naombeni kujua nini natakiwa kukifanya maana najaribu kumpigia jamaa kuhusu hili ila kila tukiongea ananiambia nipe muda kidogo walau wiki nitakuja tutayamaliza lakini naona kila ifikapo hiyo wiki ninapo mtafuta ana leta usanii sanii tuu na sasahivi hapokei simu zangu kabisa ndugu na rafiki zangu wakaribu wananiambia nirudi kuwaeleza serikali ya mtaa kilichotokea kupitia baraza la ardhi ili wamuite tujadili maana aliponiuzia kiwanja ramani aliyonipa na aliyotoa serekali ya mtaa ilikuwa ikionyesha njia inafika mpaka kwenye kiwanja sasa sahivi nagundua ilikua ni mchezo,
Jamaa nyumbani kwake ni meter 100 tu kutoka hapa kwenye kiwanja lakini kila nikija sight ananikwepa hatuonani na naambiwa huwa yupo tu kila siku saa 10 anakuwa kashatoka kazini yupo mtaani watu wanamuona
Naombeni mnishauri nifanyeje