Berryblack
Member
- Oct 3, 2022
- 70
- 104
Katika harakati za umiliki wa eneo, ni muhimu kuelewa kwamba kupata Hati ya Ardhi si jambo la siku moja. Ni mchakato unaopitia hatua mbalimbali za kisheria na kiutawala ambazo huwezesha mmiliki kupata umiliki rasmi unaotambulika na Serikali.
Hatua ya kwanza ni kuhakikisha kuwa una umiliki halali wa eneo husika. Lazima uwe na nyaraka zinazothibitisha umiliki wako. Ikiwa ulinunua eneo hilo, mkataba wa mauziano ni mojawapo ya nyaraka muhimu zinazoweza kuthibitisha namna ulivyopata umiliki wa eneo hilo.
Hatua ya pili ni kuhakikisha kwamba eneo lako lipo katika matumizi ya ardhi yaliyopangwa na Serikali. Katika hatua hii, inahitajika kupata mchoro wa mpango mji (Town Planning Drawing) unaoonesha matumizi yaliyopangwa kwa eneo husika kwa mujibu wa mpango wa matumizi ya ardhi uliopo.
Hatua ya tatu ni upimaji wa eneo. Eneo hupimwa na kuwekwa beacons ili kutambuliwa rasmi kwenye ramani za upimaji. Baada ya kukamilika kwa upimaji, kiwanja hupatiwa namba maalum ya utambulisho ambayo hutumika katika hatua zinazofuata za umilikishaji.
Hatua ya nne ni maandalizi ya nyaraka za umilikishaji. Katika hatua hii viongozi wa Serikali za Mitaa huhusika kuthibitisha umiliki na kuweka kumbukumbu zinazohitajika kwa ajili ya maombi ya kumilikishwa eneo husika.
Baada ya hatua hizo kukamilika, maombi rasmi ya kupata Hati ya Ardhi huwasilishwa kwa mamlaka husika kwa ajili ya uchambuzi, uhakiki na idhini. Mwombaji pia anatakiwa kuwa na nyaraka muhimu za utambulisho kama NIDA pamoja na nyaraka nyingine zitakazohitajika kulingana na aina ya umiliki unaoombwa.
Kwa hiyo, upatikanaji wa Hati ya Ardhi ni mchakato unaohitaji maandalizi sahihi ya nyaraka, kufuata taratibu za mipango miji, upimaji wa eneo na idhini kutoka mamlaka husika kabla ya hati kutolewa rasmi
Kwa maswali zaidi karibu