Naomba Ushauri katika ufugaji wa nguruwe

MEK_TZ

Senior Member
Apr 21, 2021
171
348
Habari ya leo wana JF matumaini yangu tu wazima kwa uweza wa muumba atutiaye nguvu na uzima.
Naomba kurejesha ombi langu juu ya kupata msaada namna gani naweza fanikiwa katika ufugaji wa nguruwe.

Niliwahi andika uzi juu ya kutaka ushauri wa biashara ipi itanifaa kupitia mtaji/kiasi nilicho bahatika kufikisha katika kujitafuta kwangu kama kijana ninae pambana kujikwamua kiuchumi.
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽

Kupitia ushauri wa wadau mbalimbali na mawazo tofauti nimefanya research na kubaini kuwa kila biashara ni nzuri ukituliza akili na kijituma unaweza toboa. Pia nimebaini kila biashara inafaida zake na changamoto zake hivyo nikajipa muda niweze fanya maamuzi yatakayo nivusha hatua.

Binafsi nimeona biashara ya ufugaji wa nguruwe unaweza endesha maisha yangu hivyo naomba kupata msaada juu ya mambo yafuatayo.

  1. Namna ya ufugaji bora na wa kisasa.
  2. Soko la uuzaji na ununuzi wa mifugo hiyo
  3. Faida na hasara za ufugaji wa nguruwe.
Zaidi ni kuwa nahitaji kujikita kwenye mradi huu wa nguruwe hivyo nahitaji msaada wa Elimu na mengine yatakayo nisaidia katika safari yangu ya Biashara.
Asanteni.
MEK
 
Salama mkuu?

Kwanza nikupongeze kwa wazo zuri la kutaka kuingia kwenye biashara ya ufugaji wa Nguruwe!
Nitakujibu maswali yako kutokana na uzoefu wangu katika hii biashara:

1. Namna ya ufugaji bora wa kisasa:
Ufugaji bora wenye tija huzingatia vitu vitatu:
I. Miundombinu bora
II. Lishe bora
III. Mbegu bora.

I. Miundombinu bora
Hapa tunazungumzia mabanda bora kwaajili ya wanyama wako kuishi,banda bora linatakiwa kuwa na mzunguko mzuri wa hewa ,floor nzuri isiyoteleza, isiyotuamisha maji na mkojo,pia ambayo ni rahisi kusafishika!
Paa imara linalo mkinga mnyama dhidi ya upepo mkali,jua kali na mvua!

II. Lishe bora
Mnyama anatakiwa apate mlo kamili unaokidhi mahitaji yake ya mwili kutokana na Umri wake.
Chakula hiki kinaweza kutengenezwa na mfugaji mwenyewe kwa kununua malighafi kama unga wa dagaa,mashudu,chokaa,premix n.k ,au kununua kilichotengenezwa tayari madukani(Concentrates) na kuchanganya na pumba au mahindi paraza. Pia uwepo wa maji safi ya kunywa muda wote.

III. Mbegu bora
Ili ufugaji wako uwe na tija na wenye kukuletea manufaa utahitaji mbegu bora.Mbegu ambayo ina sifa za Ukuaji wa haraka,Kuzaa watoto wengi,Uleaji mzuri wa watoto pamoja na utengenezaji wa nyama nyingi isiyokuwa na mafuta mengi(Lean Meat). Zipo aina mbalimbali za mbegu ambazo uhitaji wake kwenye mradi wako itategemea na malengo yako! Mfano wapo Large white, Landrace, Duroc & Pietrain.

N.B: Kupata matokeo mazuri zaidi lazima ujikamilishe katika miundombinu bora na lishe bora, kuwa na mbegu bora bila Lishe na Miundombinu bora hutapata matokeo tarajiwa.

2. Soko la uuzaji wa Mifugo hiyo
Hapa hutegemea na malengo yako katika ufugaji wako,Mfano kuna wanaofuga wakilenga kuuza mbegu;watoto wa miezi mitatu(Growers) ina maana hapa wateja wako mainly ni wale wanaofikiria kuanza miradi au wale wanaotaka kuboresha miradi kwa kupata mbegu bora zaidi. Mara myingi bei huanzia 300,000mpaka 500,000. Kutegemea na aina ya mbegu,mazingira uliyopo na matunzo yako.

Pia wapo wanaofuga kwa lengo la kuzalisha na kunenepesha wanyama ili kuchinja.(kuuza nyama)
Soko la Nyama ni kubwa sijajua upo mkoa gani,lakini nijuavyokila mkoa demand ya kitimoto ni kubwa mno.Ukiwa na mzigo mkubwa unaweza watafuta watu wa Dar mkaja kumalizana shambani kwa kuuziana kwa bei ya jumla(6000 mpaka7000/kg ya nyama).

3. Faida na hasara za ufugaji huu
□Kwa experience yangu Faida ipo,hutegemea na stratergy unayotumia kuendesha mradi wako.
●Unafanya nini kuhakikisha unapunguza gharama za uendeshaji (hasa chakula)ili kupata faida zaidi?.
●Unatumia mbinu gani kuhakikisha unapata wateja zaidi(hasa kwenye uuzaji wa mbegu),
●Unaweza kuongeza thamani ya Nyama ili kuza kwa bei nzuri zaidi?
Hayo ni kwa ufupi ila yapo mabo mengine mengi.

Hasara
Hasara kubwa kwenye mradi huu ambayo huwa naiona iko wazi ni Ugonjwa wa Mlipuko wa homa ya nguruwe(AFRICA SWINE FEVER) hii ikitokea mzee hakuna kitu utaokoa ni hasara big time!
Japo unaweza kucontrol kwa Biosecurity kuhakikisha kuwa hufikiwi na hawa virus kwenye mradi wako!

Changamoto nyingine ambazo zinaziweza kukupa hasara kama vile Vifo vya watoto,magonjwa ya uzazi, na homa za kawaida pamoja na Wizi hizi zote zinatatulika!

Kwa leo niishie hapa,Tusubiri wajuvi wengine kwa michango!
 
Mjadala ufungwe umemaliza kila kitu
 
Asante sana mkuu Mungu akubariki.
 
Habari ya leo wana JF matumaini yangu tu wazima kwa uweza wa muumba atutiaye nguvu na uzima.
Naomba kurejesha ombi langu juu ya kupata msaada namna gani naweza fanikiwa katika ufugaji wa nguruwe.

Niliwahi andika uzi juu ya kutaka ushauri wa biashara ipi itanifaa kupitia mtaji/kiasi nilicho bahatika kufikisha katika kujitafuta kwangu kama kijana ninae pambana kujikwamua kiuchumi.
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽

Kupitia ushauri wa wadau mbalimbali na mawazo tofauti nimefanya research na kubaini kuwa kila biashara ni nzuri ukituliza akili na kijituma unaweza toboa. Pia nimebaini kila biashara inafaida zake na changamoto zake hivyo nikajipa muda niweze fanya maamuzi yatakayo nivusha hatua.

Binafsi nimeona biashara ya ufugaji wa nguruwe unaweza endesha maisha yangu hivyo naomba kupata msaada juu ya mambo yafuatayo.

  1. Namna ya ufugaji bora na wa kisasa.
  2. Soko la uuzaji na ununuzi wa mifugo hiyo
  3. Faida na hasara za ufugaji wa nguruwe.
Zaidi ni kuwa nahitaji kujikita kwenye mradi huu wa nguruwe hivyo nahitaji msaada wa Elimu na mengine yatakayo nisaidia katika safari yangu ya Biashara.
Asanteni.
MEK
0752 742 617, ELLYFARM Mwenyekiti wa wafuga Nguruwe. atakusaidia sana ktk elimu juu ya ufugaji Nguruwe, barikiwa sana ktk wazo lako. Ukipenda na group atakujumlisha.
 
Mwenyekiti wa mkoa au taifa?
Yeye yupo Mwanza lakini anaweza kukusaidia upande wowote wa Nchi. Naomba uwasiliane nae atakusaidia sana kwa upande wa mifugo ya Nguruwe, mimi msaada wangu ni kwa Mbuzi.
 
Back
Top Bottom