Naomba ushauri juu ya huyu boss

Mimi alikua kama wako, ni mtu wa kulaumu, kufokafoka hata mkiwa na maongezi ya kawaida, nikawa nakausha tu, siku moja nikasema kama mbwai mbwai tu, nikamchana sana tena disrespectively kabisa, akawa mdogo, siku hizi tunaenda sawa wala haniletei mikwara ya kijinga. Usiwe mnyonge sana...
 
Namaanisha baadhi ya ndugu zake nao waliwahi kuniuliza unaishije na boss wako, ndo ikapelekea kumjua kiundani
Ebu tumia ID ya zamani maana hii naona ni maalum kwa ajili ya huu uzi tu.Utapata ushauri mzuri sana. Huoni mzee tupatupa kapotea.
 
Siku nyingine akikutoa out then akaanzisha mboyoyo mboyoyo za ofisini unamtia vitasa vya maana then kesho yake unamuomba msamaha na kumwambia ni pombe
Hajasema kama akimtoa out wanakunywa pombe mkuu. Muulize huko out huwa anamfanya nini hadi akubali kwenda hata kama anatukanwa.
 
anakufokea na mnatoka out weekend! fanya kazi maneno yake usiyafuatilie yatakutoa kwenye njia.
 
ni siri tu miongoni mwa weengi.... the best way ni kujiajiri na kudeal na busines.... asilimia 90 ya waajiriwa.. kufokeana ni kawaida saaaaana... komaaa tu
 
Hivi huyo DC amejiajiri?
atajiaili siku akitumbuliwa, niliwahi kuacha kazi mahali sababu ya bosi mjinga mjinga sikutaka kudhalilisha professional yangu, cha msingi ni kuweka misingi ya kujiajili wakati upo kibaruani
 
Pole sana mkuu, mimi boss wangu alikuwa mpaka ananiita bogus, hakuna unachokifanya kwake kikaonekana chema. Muda wa kuripoti ofisini ni sa mbili kamili ila alikuwa anataka mtu aingie sa moja na nusu. Ukienda lunch one hour anakusema, anasema watanzania ni wavivu wanapenda kula. Muda wa kutoka anataka utoke kuanzia sa kumi na mbili na nusu. Inshort alikuwa umiza kichwa, mwisho wa siku niliamua kuacha kazi maana ilikuwa too much. Niliona naweza pata ugonjwa wa moyo. Pole sana mkuu ila kwa style hiyo huwezi fyrahia kazi yako.
 
Jitahd kuvumilia hivyo hivyo Ila Tafuta plan b yaan kup a ta kaz sehemu nyingine ukifanikiwa acha
 
Ukitoka job switch lyn ambayo hana no yako itumie ikifika muda wa kulala irudishie tena ya zamani,akikutoa out mwambie una dharura huwezi kwenda .
 
Mimi ni mwajiriwa wa taasisi fulani inayohusika na maswala ya ununuzi, nimeajiriwa tangu mwaka juzi.

Tatizo nililonalo ni huyu boss wangu amekuwa ni mtu wa hasira sana ukikosea kidogo tu lazima achukue siku nzima kukusema na yupo radhi hata weekend akupgie simu mtoke wote ila mkifika kwanye huo mtoko lazima akuanzishie mambo ya ofisini na kukusema tena kibaya zaidi ukimjibu ndo anazidisha mara ooh mpumbavu we hutumii akili yani inshort napata wakati mgumu natamani kuacha kazi ila nashindwa kwan familia inantegemea.

Nimejiuliza kwa watu wake wakaribu wanadai sio wewe tu ndivyo alivyo kwani ni mtu anayeamini yuko sahihi kwa kila kitu na pia jeuri ya fedha inampa kiburi

Tafadhali naomba ushauri wenu nifanyeje ili niweze kuendana na huyu boss wangu.
Fanya kazi kwa bidii bila kuongea nae ovyo.
 
Wanaume wa dar bwana shida kwel.
Weekend anakuita kwenye mtoko kama nani? Ww ni dereva wake? Huna familia ya kuenjoy hiyo weekend? Au mtoko ni sehemu ya kazi?

Huyo ni mwanaume mwenzio na hayo ni maswala ya kazi...unaleta hoja hapa love forum inaonekana kuna kitu usha gundua hapo lkn unajifanya kuficha.

Huyo anataka huduma ya mtandao pendwa tafadhali kwa vile huna pa kushika we mhudumie tuuu na atakulipa zaidi.
Maana huko kufoka ni ww kuto kujiongeza
..
 
Back
Top Bottom