Naomba ushauri juu ya huyu boss

WAR

Member
Dec 16, 2016
41
95
Mimi ni mwajiriwa wa taasisi fulani inayohusika na maswala ya ununuzi, nimeajiriwa tangu mwaka juzi.

Tatizo nililonalo ni huyu boss wangu amekuwa ni mtu wa hasira sana ukikosea kidogo tu lazima achukue siku nzima kukusema na yupo radhi hata weekend akupgie simu mtoke wote ila mkifika kwanye huo mtoko lazima akuanzishie mambo ya ofisini na kukusema tena kibaya zaidi ukimjibu ndo anazidisha mara ooh mpumbavu we hutumii akili yani inshort napata wakati mgumu natamani kuacha kazi ila nashindwa kwan familia inantegemea.

Nimejiuliza kwa watu wake wakaribu wanadai sio wewe tu ndivyo alivyo kwani ni mtu anayeamini yuko sahihi kwa kila kitu na pia jeuri ya fedha inampa kiburi

Tafadhali naomba ushauri wenu nifanyeje ili niweze kuendana na huyu boss wangu.
 

tejay

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
1,255
2,000
Mimi ni mwajiliwa wa taasisi fulani inayohusika na maswala ya ununuzi, nimeajiriwa tangu mwaka juzi. Tatizo nililonalo ni huyu boss wangu amekuwa ni mtu wa hasira sana ukikosea kidogo tu lazima achukue siku nzima kukusema na yupo radhi hata wekeend akupgie simu mtoke wote ila mkifika kwanye huo mtoko lazima akuanzishie mambo ya ofisini na kukusema tena kibaya zaidi ukimjibu ndo anazidisha mara ooh mpumbavu we hutumii akili yani inshort napata wakati mgumu natamani kuacha kazi ila nashindwa kwan familia inantegemea.

Nimejiuliza kwa watu wake wakaribu wanadai sio wewe tu ndivyo alivyo kwani ni mtu anayeamini yuko sahihi kwa kila kitu na pia jeuri ya fedha inampa kiburi

Tafadhari naomba ushauri wenu nifanyeje ili niweze kuendana na huyu boss wangu.
Acha kazi
 

MO11

JF-Expert Member
Mar 23, 2014
17,454
2,000
Tatizo unafikiri ukiacha kazi hapo unahisi hutopata kazi kwengine
dawa yake unampa mitusi ili aone hujali.

au kama bosi demu anakutaka
 

Hamis Juma

Verified Member
Nov 4, 2011
2,220
2,000
Mpotezee, mradi watoto wanaenda chooni... Stress zake anamalizia kwenu, jifanye kama hujali piga kazi kila sehemu mabosi wana shida zao.
 

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
173,855
2,000
Pole,wapo watakaokubeza ila yakiwafika watakumbuka post yako na kuja kusoma ushauri uliopewa. Maboss wa namna hiyo wengi ni attention seeker. Na anataka awe juu tu. Hivyo ili uendane nae inabidi uishi kama mtumwa.
 

Idofi

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
2,007
2,000
DC hapi alisema kuajiliwa ni sehemu ya utumwa, kwa hiyo ukikubali utumwa vumilia, ukitaka uhuru kuwa mjasiriamali
 

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
10,632
2,000
Watu wake wa karibu wapi hao! Mie nadhani nyie na wewe ukiwemo mnae shinda nae nae ofisini ndio watu wa karibu.tena kwa miaka 3 uponaye ofisi moja kwa kila siku mpo nae masaa zaidi ya 9 huo ni ukaribu tosha
 

WAR

Member
Dec 16, 2016
41
95
Watu wake wa karibu wapi hao! Mie nadhani nyie na wewe ukiwemo mnae shinda nae nae ofisini ndio watu wa karibu.tena kwa miaka 3 uponaye ofisi moja kwa kila siku mpo nae masaa zaidi ya 9 huo ni ukaribu tosha
Namaanisha baadhi ya ndugu zake nao waliwahi kuniuliza unaishije na boss wako, ndo ikapelekea kumjua kiundani
 

wehoodie

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
985
1,000
Msome hulka zake kisha uishi nae kwa jinsi alivyo. Ujue mtu ukishayajua madhaifu yake mchukulie kama mlemavu tu. Wewe mpotezee tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom