Naomba ushauri juu ya biashara ya Uber, Bolt

Inategemea na gari lenyewe sasa! Gari zingine hazifai mfano gari 1800cc 8km/l unaifanyaje bolt na hayo mafoleni! Uende trip ubungo mbagala ikusomee 8000 wakati litre ya mafuta ni 2400 hehehe umeenda umbali wa almost kilometre 20+ kurudi ukose napo mtu, utamanage vipi? Kuna jamaa ana ki vits tu cha 990cc ila analia lia!

Hapo tairi hazijaisha oil haijadai changes!
Nilitoka tmj mikocheni hadi kinyerezi mwisho kwa 12000 ,nikaanza kupiga story na dereva akaniambia wanapata hela ya kula tu biashara ngumu
 
Nilitoka tmj mikocheni hadi kinyerezi mwisho kwa 12000 ,nikaanza kupiga story na dereva akaniambia wanapata hela ya kula tu biashara ngumu
Ile biashara sio! Bora ku bargain na mteja ile fairplay! Japo wengine walikuwa wanawapiga sana😅 ila kwa hali ya mafuta ilivyo wengi watakabidhi gari kwa wenyewe! Zamani uliweza mtoa mtu mbez mwisho mpaka Segerea kwa 25K tu! Ndio bei zilipokuwa zimefikia minimum 15K hapo trip kawaida!

Bolt kwa boda boda ndio wanainjoy sababu litre1 tu inaenda almost 40km! Sasa akikupeleka we mbagala ikasoma 8000 ana litre 3 na nusu humo! Trip fupi fupi zile anaweza tengeneza hesabu ya siku kwa mafuta ya elf 5 tu
 
Nimefanya bolt na uber na nilifanya kwa takribani safari 3001.

Kwanza ili uifurahie kazi ya bolt na uber ni vizuri gari iwe yako hapo kidogo unaweza kuiona hela.

Siku nzuri za kufanya kazi na kuwa na kijimzunguko cha fedha ni kuanzia siku ya ijumaa mpaka ijumapili.

Hesabu kwa matajiri wengi ambao wanaajiri madereva huwa wanachukua laki na nusu kwa week au elf 30 kwa siku.

Changamoto za kazi hii ni pale unapopata trip za nje ya mji mfano unaweza kupata mteja kutoka kariakoo ukampeleka mpaka bunju B but ukishamfikisha bunju B ukarudi bila abiria mpka kariakoo hivyo ikawa kazi ulofanya ni kazi bure na kitu kingine kinachoweza kukusababishia ufungiwe account ni pale unapo cancel trip.

Kama utakuwa una swali lingine la ,iada unaweza uliza hapa au hata dm ntakusaidia

Mimi natamani sana kuendesha hizi bolt lakini leseni yangu ni daraja A B D E naomba unishauri na kama kuna uwezekano wa kupata gari ya hesabu sehemu naomba pia uniunganishe ndugu yangu
 
Watu wanasomesha watoto wanalipa kodi wanatunza family kwa hiyo kazi.

Wewe tu kuwa mkweli hautaki Uber wawe wengi una asili ya roho mbaya.
Ahaaa da umenionea bure,hiyo kazi ni pasua kichwa unajua bei ya mafuta iko juu now ila rate ziko chini mno,kutoka ubungo mpaka mbezi standi 11000 na unarudi tupu sometimes au usubirie sana,hela ya kula utapata ila sio ya kujenga maisha
 
Ahaaa da umenionea bure,hiyo kazi ni pasua kichwa unajua bei ya mafuta iko juu now ila rate ziko chini mno,kutoka ubungo mpaka mbezi standi 11000 na unarudi tupu sometimes au usubirie sana,hela ya kula utapata ila sio ya kujenga maisha
Basi usikatishe watu tamaa kwa maneno ya kusikia....hiyo ishu ingekuwa hailipi watu wasingeagiza magari kwa ajili ya kufanyia uber, kama upo serious unaweza mpaka kujenga kwa uber.
 
Watu wanasomesha watoto wanalipa kodi wanatunza family kwa hiyo kazi.

Wewe tu kuwa mkweli hautaki Uber wawe wengi una asili ya roho mbaya.
Doh. Miji mikubwa ni wazi hii biashara inawaweka watu mjini. Kunaweza kuwa na changamoto kadhaa. Lakini sio kwa kiasi kinachosemwa na wengi wa wachangiaji. Ninaendelea na utafiti ninakusudia kufanya bolt ndani ya kipindi kichache kijacho preferably Dodoma or Arusha.
 
Ahaaa da umenionea bure,hiyo kazi ni pasua kichwa unajua bei ya mafuta iko juu now ila rate ziko chini mno,kutoka ubungo mpaka mbezi standi 11000 na unarudi tupu sometimes au usubirie sana,hela ya kula utapata ila sio ya kujenga maisha
Inalipa Sana kuliko kuajiriwa
 
HII BIASHARA HAILIPI (ili kulaza hiyo 70,000 kwa siku lazima uenyeke sana)

Nianze na UBER. Uber wanalipa kila kilomita sh. 450 na kila dakika sh. 80.

Tuchukulia kinadharia nimeamua ku “ request” Uber nikazunguka nayo masaa 12 na kutembea Dar kilomita 300.

Nakokotoa hesabu

Km 300 x shs. 450 = 135,000
Dakika 12x60x shs. 80 = 57,600

JUMLA NI 192,600

Kilomita 300 kwa Gari kama IST inatumia lita 33-37 inategemea na uendeshaji wa dereva

Tuchukulie lita 35x bei ya petrol sasa 2,123 = 74,305

UBER wanakata chao asilimia 25%
Kwa hiyo (25% x 192,600) - mafuta 74,305 = 70,145

Kwa hiyo dereva anabakiwa 70,145 kama gari ni yako, kama ana boss atoe hiyo t.shs 25,000 au 30,000.

Kuna malipo ya latra , insuarence, parking tickets(unaweza kuona ndogo lakini ziki accumulate ni nyingi.) Gari itahitaji service mara kwa mara maana inatembea km nyingi kwa siku

Uhalisia ni kwamba huwezi pata Request kila muda, kupata 70,000 kwa siku ni kazi kubwa sana

HASARA YA BIASHARA HII
1. Mteja aki “request” ukaenda kumchukua haulipwi kwa km ulizotembea kumfuata, malipo yanaanza pale tu mteja akiingia kwenye gari. Hiyo ni hasara kwa dereva.
2. Kuna maeneo mengi Dar ukimpeleka mteja unarudi kapa. Na hujui abiria unampeleka wapi mpaka aingie kwenye gari.
3. Dar njia nyingi ni mbovu ni kuichosha gari tu.
4. Wateja hawajui kutumia app vizuri, location alipo na alipo “pin” kwenye map ni vitu viwili tofauti. Unahangaika kumtafuta ukimuudhi ana cancel
5. App ya Uber ikikaa masaa 12 mfulizo inajizima, inakulazimisha upumzike angalau masaa 6 ndio inarudi
6. Traffic wameshaijua hii biashara usumbufu wao lazima uache “5,000”

FAIDA labda upate “tips” na kwa wageni, (wabongo hawatoi, wanalaalamika tu kwamba unaendesha taratibu ili hela iongozeke au uawapitisha kwenye foleni.) WABONGO BANA.

Kuna muda UBER wanatoa bonus au kuna mida hela inaongezeka kidogo kipindi kuanzia saa 9 alasiri au kama kuna demand kubwa ya gari

Wateja wakikuzoea wanakuwa wanakupigia simu direct, unakwepa 25% ya UBER

BOLT WANALIPA 400km na t.sh. 72 kwa dakika kama nakumbuka vizuri
Mkuu binafsi nimekuelewa kwa maoni uliyotoa, ila ninaswali, umesema 450@ km ili itapitikane faida inayoridhisha, unashauri litumike gari lenye ukubwa gani wa injini ,"cc"
 
Back
Top Bottom