Pole sana kwa majaribu, nakushauri mpuuze, fanya kilichokupeleka.
Mambo yakizidi, basi unaweza kuwasiliana na viongozi wa chama cha wafanyakazi kinachokuwakilisha, utawaeleza changamoto hiyo na vitisho unavyovipata huku ukiwa na ushahidi hata wa meseji.
Hao viongozi watajua mbinu za kuwasiliana na uongozi wa shirika unalofanyia kazi. Lakini pia itaweka tahadhari juu ya mpango wa kukuharibia kazi kwa mambo binafsi na kukufanya kuwa salama zaidi.
Tahadhari: usithubutu kutembea na huyo mama na kama umeanza naye, acha.
Kila la heri.