Naomba ushauri, biashara yangu haiendelei

jay moseif

Member
May 4, 2020
7
4
Habari wanajamvi, nimekuja mbele yenu mm ni kijana wa miaka 25, lengo la kuamdika uzi huu ni kuomba ushauri juu ya biashara yangu.

Mimi ni fundi kuchomea lakini pia nimejiongeza kwa kujifunza ufundi sofa. Lakini biashara yangu haitembei kabisa labda wenye uzoefu na mambo haya wanipe ushauri. Maana biashara haitembei kabisa unafanya kazi zikizkata najikuta natumia hadi akiba. Kazi zikija yani mzunguko unakuwa huo. Naombeni ushauri.

Nawasilisha
 
Tafuta dalali a.k.a marketing officer, ambaye atakuwa anatafuta wateja. Atakuwa anazunguka kwenye nyumba zinazojengwa au zenye uhitaji wa kazi za kuchomelea kama mageti, madirisha etc. Dalali utakuwa una mlipa kwa kazi anazoleta. Mtengenezee vlpeperushi (Catalog) ambavyo vinaonyesha picha za kazi zako. Picha quality. Tafuta mpiga picha na graphic designer kwa ajili ya kazi hiyo. Pia atakutengeneza business card ambazo atakuwa anaziacha kwa wateja.

Hakikisha ukipata kazi unaikamilisha kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu. Kwani biashara kama hizi wateja wake wengi hupatikana kwa njia ya (word of mouth), ikiwa na maana mteja kumuelekeza ndugu yake au rafiki yake. Kwa mfano umetengeneza geti nzuri, mwenye nyumba anapata mgeni, mgeni analipenda hilo geti atamuuliza hili heti nani kakutengenezea .. Atatoa contact zako na utapata mteja mpya kupitia yeye.

Vijana wengi mnaangushwa na vitu viwili.
1. Kutokamilisha kazi kwa wakati. (yaani unamzungusha mteja hadi kazi ikamilike hana hamu na wewe) hivyo hawezi kukuunganisha na mtu mwingine.
2. Kufanya kazi zisizo na ubora au kinyume na makubaliano na mteja.
3. Kuwadanganya wateja. Kwa mfano mmekubaliana dirisha litakuwa na nondo au flat bar za nchi fulani. Na mteja anakulipa hizo nchi.. Wewe kwa tamaa unaenda kufunga za nchi ndogo kuliko mliyokubaliana ukidhani kuwa mteja hatakaa ajue. Siku mteja akijua kuwa uli mrusha ndo inakiwa mwisho wa kuwasiliana na wewe na kamwe hatakuunganisha kazi yoyote.

Kuna kijana nilimpa kazi ya kuchimba kisima, tumekubaliana bei na aina ya material na nikamlipa kama tulivyokubaliana. Kumbe kule chini ya kisima kaweka pipe (mpira wa kutolea maji) ambao ni used na ulikuwa imeppasuka sehemu mbili. Yeye akafunga mipira hizi sehemu akaniwekea. Kisima kimefanya kazi vizuri baada ya miezi mitatu presha ya maji ikawa imepungua sana. Nikamuita lakini kwa sababu alikuwa anajua tatizo alilosababisha hakuja, akajidai amesafiri. Nikatafuta fundi mwingine akafungua akakuta pipe imefungwa na mipira sehemu mbili amabay imefunguka. Ikabidi ninunue pipe mpya ya mita 70.

Sasa unaweza kufikiri ni kiasi gani vijana wasivyo waaminifu. Na mtu kama huyu hawezi kufika mbali maana binafsi nimeshaombwa contact ya mtu aliye nichimbia kisima kama mara tatu hivi ila siwezi kuwapa namba ya huyo kijana. Nawaambia tafuteni tu sehemu nyingine.
 
Ushauri mzuri sana mkuu✅
 
Pole, mbali na ufundi sofa jifunze pia aluminium! Andaa business card, weka namba zako nA huduma unazotoa, sambaza kwenye masaiti tofauti, jenga urafiki na mafundi wakufanyie mchongo wa kaz kwa maboss, pia usiwe bahili uwe unawapooza posho nzuri ! Kizuri kula na nduguyo ndo tunavyoishi !!!!!! Kila la kheri
 
Asante sana mkuu
 
Tafuta dalali a.k.a marketing officer, ambaye atakuwa anatafuta wateja. Atakuwa anazunguka kwenye nyumba zinazojengwa au zenye uhitaji wa kazi za kuchomelea kama mageti, madirisha etc. Dalali utakuwa una mlipa kwa kazi anazoleta. Mtengenezee vlpeperushi (Catalog) ambavyo vinaonyesha picha za kazi zako. Picha quality. Tafuta mpiga picha na graphic designer kwa ajili ya kazi hiyo. Pia atakutengeneza business card ambazo atakuwa anaziacha kwa wateja.

Hakikisha ukipata kazi unaikamilisha kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu. Kwani biashara kama hizi wateja wake wengi hupatikana kwa njia ya (word of mouth), ikiwa na maana mteja kumuelekeza ndugu yake au rafiki yake. Kwa mfano umetengeneza geti nzuri, mwenye nyumba anapata mgeni, mgeni analipenda hilo geti atamuuliza hili heti nani kakutengenezea .. Atatoa contact zako na utapata mteja mpya kupitia yeye.

Vijana wengi mnaangushwa na vitu viwili.
1. Kutokamilisha kazi kwa wakati. (yaani unamzungusha mteja hadi kazi ikamilike hana hamu na wewe) hivyo hawezi kukuunganisha na mtu mwingine.
2. Kufanya kazi zisizo na ubora au kinyume na makubaliano na mteja.
3. Kuwadanganya wateja. Kwa mfano mmekubaliana dirisha litakuwa na nondo au flat bar za nchi fulani. Na mteja anakulipa hizo nchi.. Wewe kwa tamaa unaenda kufunga za nchi ndogo kuliko mliyokubaliana ukidhani kuwa mteja hatakaa ajue. Siku mteja akijua kuwa uli mrusha ndo inakiwa mwisho wa kuwasiliana na wewe na kamwe hatakuunganisha kazi yoyote.

Kuna kijana nilimpa kazi ya kuchimba kisima, tumekubaliana bei na aina ya material na nikamlipa kama tulivyokubaliana. Kumbe kule chini ya kisima kaweka pipe (mpira wa kutolea maji) ambao ni used na ulikuwa imeppasuka sehemu mbili. Yeye akafunga mipira hizi sehemu akaniwekea. Kisima kimefanya kazi vizuri baada ya miezi mitatu presha ya maji ikawa imepungua sana. Nikamuita lakini kwa sababu alikuwa anajua tatizo alilosababisha hakuja, akajidai amesafiri. Nikatafuta fundi mwingine akafungua akakuta pipe imefungwa na mipira sehemu mbili amabay imefunguka. Ikabidi ninunue pipe mpya ya mita 70.

Sasa unaweza kufikiri ni kiasi gani vijana wasivyo waaminifu. Na mtu kama huyu hawezi kufika mbali maana binafsi nimeshaombwa contact ya mtu aliye nichimbia kisima kama mara tatu hivi ila siwezi kuwapa namba ya huyo kijana. Nawaambia tafuteni tu sehemu nyingine.
Ubarikiwe sana mkuu asante kwa ushauri
 
Unatumia njia gani kujitangaza? Jitangaze mkuu kwa kutembelea sites na katika mitandao.

Jumlisha ushauri wa adabu na nidhamu ya kazi.

Nakupa challenge mpaka sasa una list ya wateja ambao uliwahudumia vizuri, je umejenga mahusiano nao.

Au kwa ambao umejenga mahusiano nao unajitahidi wakati mwingine kuwasiliana nao bila kuwapa presha ya nipe tenda, nitafutie kazi n.k?
 
Naichukua hii
UAMINIFU.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Inshu nyingine mafundi wengi mno. Kwa hiyo ushi dani ni mkubwa. Jambo linalosababisha bei kuwa chini kitu kinachopunguza faida.
 
Habari wanajamvi, nimekuja mbele yenu mm ni kijana wa miaka 25, lengo la kuamdika uzi huu ni kuomba ushauri juu ya biashara yangu.

Mimi ni fundi kuchomea lakini pia nimejiongeza kwa kujifunza ufundi sofa. Lakini biashara yangu haitembei kabisa labda wenye uzoefu na mambo haya wanipe ushauri. Maana biashara haitembei kabisa unafanya kazi zikizkata najikuta natumia hadi akiba. Kazi zikija yani mzunguko unakuwa huo. Naombeni ushauri.

Nawasilisha
Unajichanganya viwanja ama ni mzee wa pokea pokea..kwa mwamposa.
 
Unatumia njia gani kujitangaza? Jitangaze mkuu kwa kutembelea sites na katika mitandao.

Jumlisha ushauri wa adabu na nidhamu ya kazi.

Nakupa challenge mpaka sasa una list ya wateja ambao uliwahudumia vizuri, je umejenga mahusiano nao.

Au kwa ambao umejenga mahusiano nao unajitahidi wakati mwingine kuwasiliana nao bila kuwapa presha ya nipe tenda, nitafutie kazi n.k?
Mkuu Asante sana kwa ushauri. Mbinu hii ckuwahi kuifanya kabla
 
Back
Top Bottom