Naomba ujuzi Jinsi ya kumlea mwanangu wa kike

Katika kujifunza kuhusiana na malezi nimefikia hatua naona hakuna malezi bora bali ni mapokeo ya character aliyonayo unaemlea(nakosa namna fasaha ya kuielezea), na ndio mana kwa kawaida kati ya watoto wanne waliolelewa na mama mmoja wana maudhui tofauti kulingana na mapokeo yao ambayo yapo ndani yao.

Mf. Mlezi anaweza akajitahidi kufundisha watoto kufanya kazi kwa juhudi(uwajibikaji), kusali, nidhamu nk.
Lakini kati ya wanne kati yao wakagawana kimojawapo kati ya nyenzo ulizowapa.

Kati yao akatokea mvivu kupindukia(asiewajibika)
Mchafu, asiemcha Mungu(hii anglia kwenye familia za wachungaji/watu wa dini) lazima kuwe na kilazammoja asiependa kusali ili mradi kutia dosari familia..

Tuliozaa, Rai yangu kwenu tuwakabidhi watoto kwa Mungu, tuwaombee akili yao ipokee mafundisho yetu kama tunavyokusudia. Amina

NB: SIO UCHUNGUZI NI MAONI😉
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom