Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,801
- 43,177
Habari za mchana wapendwa!!
Kwa wasionifahamu naitwa Kasinde aka mka wa mwana mbogo
(Kasimbagoo, kasimbagoo, kabhuka........kasimbago....)
Baada ya kumaliza kidato cha sita niliolewa na na mfanyabiashara mmoja ambae tulibahatika kuzaa watoto 2, mmoja wa kike mmoja wa kiume. Mume wangu biashara zake zilikua na alifanikiwa sana wakati huo nikiwa mama wa nyumbani. Nilimpenda mume na watoto wangu na kuijali na kuihudumia muda wote. Pamoja na vituko na manyanyaso aliyonifanyia mume wangu sikuiacha familia yangu.
Nilimvumilia mume wangu kwa mengi bila kulalama na baada ya watoto wote kwenda boarding sekondari nilimuomba mume wangu nisome chuo ili nijiendeleze kieleimu haikuwa hivyo, mume wangu alikataa katu katu na kunitaka nikae jikoni. Nilinyanyasika sana, nikatamani kufanya biashara walau nipate shilingi miatano ya jasho langu. Nikamuomba mume wangu ruhusa ya kufanya biashara aliruhusu kwa kunipa mtaji wa shilingi laki 1 niwe napika vitafunio vya chai asubuhi na kuuza.
Siku isiyo na jina napokea taarifa kunamwanaume kafia gesti ya mtaani bila majeraha yoyote. Sikushawishika kwenda kumuona ila watu wa mtaani waliotoka kwenye tukio walinifata na kunihoji habari za mume wangu nina taarifa nae zipi. Sijakaa sawa polisi wanafika na kunitaka nikatambue mwili unaosadikiwa ni mume wangu. Looh kutahamaki huku nikiwa na hofu kubwa nilimtambua mume wangu na nilipoteza fahamu kwa masaa kadhaa.
Baada ya mazishi ya mume wangu maisha yalikuwa magumu mnoo, mali za mume wangu sikuwahi zijua hata maana muda wote nilikuwa mama wa nyumbani na mpika vitafunio vya chai, wqatoto walikuwa bado boarding. Baada ya miaka 3 kupita siku moja nikiwa napika vitafunio vya chai nikaletewa barua na mtoto mmoja wa miaka 10 kisha mtoto yule akakimbia, sikuwahi kumuona hapo mtaani. Nilipoisoma ile barua iliandika... '' NAOMBA UJE MAKTABA SQUARE JUMATATU SAA 4 ASUBUHI'' chini akaweka namba ya simu na jina lake Mark.
Nilipiga simu ile ya Mark haikupokelewa, ila ujumbe uliingia usiache kuja. Nilienda Maktaba Square saa 5 badala ya saa 4 nikapiga ile simu na alipokea mark akasema nimekuona nakuja. Akatokea Baba mmoja akasema yeye ni mark na anahitaji kuongea kirefu na mimi. Niliongea na Mark kwa marefu na mapana...... To make the long story short, Mark alikuwa hajaoa, alinifahamu muda mrefu pale mtaani na alikuwa ananipenda vile niko muaminifui kwa mume wangu. Aliniposa kwa upya na kunilea kama malkia, alinisomesha, tukafunga ndoa na sasa nina miaka 3 naishi na mark kwa raha na upendo. Watoto wangu anawalea kama wake, kila nikimpigia Mark namtania tukutane MAKTABA SQUARE.....
Shosti wangu kidawa alimalizia kusoma maneno hayo ya riwaya za babu.
Jioni njema.