Mkuu kama nimekuelewa, hicho ni kifaa kinachotumika kwenye High way (bara bara za kulipia). Mmiliki wa hiyo gari inaonekana alifunga kifaa hicho kukataa usumbufu kila akiingia high way kusimama kulipa, badala yake akaamua anunue ETC Machine na card yake ili akiingia High way anapita upande wa ETC tu na kulipa tozo ya matumizi ya High way Mwisho wa mwezi.Kama kifaa nnachokielezea ndio hicho kilicho kwenye gari yako basi kwa nyumbani hakina kazi. Ili kupata uhakika na hicho kifaa kilicho kwenye gari yako kama ni kweli ETC Mashine, hebu nikuulize, kina sehemu ya kuweka card? Card yenye ukubwa Sawa na hizi za bank.