Naomba kufahamishwa kuhusu hiki kifaa ETC

Akili 09 Nguvu 01

JF-Expert Member
Jun 23, 2015
693
1,365
Wakuu huu Ugonjwa Chain yake ni ndefu sana na unaenea kwa kasi sana. Tuchukue tahadhari madhubuti.

Sasa nije kwenye lengo kuu,

Ni kuwa katika harakati za kuepuka kuwa Mwana wa Israel (kutembea kwa miguu Miaka 40) nami nimefanikiwa kumiliki Gari, hii ni Toyota (NUMMI) Voltz.

Sasa nakuja kwenu Wataalamu wa Kucheza na kuanza kuendesha Magari tangu zamani mnisaidie kujua hiki kifaa kimeandikwa ELECTRONIC TOLL COLLECTION SYSTEM (ETC)
ni nini na kinafanya kazi gani?

Kifaa hiki nimekikuta kimefungwa hapa juu kidogo ya breki lakini kwakweli sijajua ni kwa ajili ya nini.

Naombeni nielimishwe.

Picha imeambatanishwa.

Screenshot_20200418-221609.jpg
 
Hicho ni kifaa Cha kielektroniki Cha kulipia ushuru wa Mageti barabarani. Kinasoma kadi maalumu Ambayo unairecharge pesa.

Kwa mfano pale darajani kigamboni, badala ya wewe kulipa cash ndo upite, kwa japani hicho kifaa kinafanya malipo automatikali.

Ko ukifika tu geti linafunguka unapita. Hela inakua imeishakatwa.
 
Hicho ni kifaa Cha kielektroniki Cha kulipia ushuru wa Mageti barabarani. Kinasoma kadi maalumu Ambayo unairecharge pesa. Kwa mfano pale darajani kigamboni, badala ya wewe kulipa cash ndo upite, kwa japani hicho kifaa kinafanya malipo automatikali. Ko ukifika tu geti linafunguka unapita. Hela inakua imeishakatwa.
Ahsante sana mkuu nimekuelewa vizuri mno
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom