Habari, Madhumuni ya kikao cha nidhamu ni kusikiliza mashtaka aliyoshitakiwa mfanyakazi na mwajiri wake. Baada ya kikao hicho kusikiliza shauri hilo, hutoa mapendekezo yake kwa kuzingatia mambo mbalimbali mama uthibitisho/Vithibitisho, maelezo ya mshitakiwa, historia ya kinidhamu ya mshitakiwa n.k Mapendekezo hayo hufanyiwa kazi moja kwa moja na mwajiri. Aidha, endapo pande zote mbili hazitaridhishwa na matokeo basi kamati hiyo inaweza kukaa tena na kusikiliza shauri hilo. Kwa hivyo, kamati ni lazima itoe mapendekezo yake.