Naomba ufafanuzi kuhusu kikao cha nidhamu kwa mwajiri kisheria

Myhope

Senior Member
Jul 20, 2017
154
67
Kikao cha nidhamu kikimkuta mwajiriwa anayo hatia lkn hakikutoa mapendekezo ya adhabu, Je Mwajiri anaweza kumfukuza kazi mwajiriwa ktk mazingira kama hayo?
 
Habari, Madhumuni ya kikao cha nidhamu ni kusikiliza mashtaka aliyoshitakiwa mfanyakazi na mwajiri wake. Baada ya kikao hicho kusikiliza shauri hilo, hutoa mapendekezo yake kwa kuzingatia mambo mbalimbali mama uthibitisho/Vithibitisho, maelezo ya mshitakiwa, historia ya kinidhamu ya mshitakiwa n.k Mapendekezo hayo hufanyiwa kazi moja kwa moja na mwajiri. Aidha, endapo pande zote mbili hazitaridhishwa na matokeo basi kamati hiyo inaweza kukaa tena na kusikiliza shauri hilo. Kwa hivyo, kamati ni lazima itoe mapendekezo yake.
 
Nimekuelewa vzr, ila kikao hicho cha nidhamu kimefanya yote hayo na kimemkuta mfanyakazi na hatia lkn hakikutoa mapendekezo ya adhabu, Je Mwajiri anaweza kumwachisha kazi mfanyakazi?
 
Katika fomu ya kikao cha nidhamu kuna kipengele cha maamuzi na mapendekezo ya kamati ni lazima kijazwe na kukamilisha fomu hiyo. Napata ukakasi unaposema kamati haijatoa mapendekezo na maamuzi ya kikao hicho.
 
Kikao chochote lazma kifikie maamuzi/maazimio

Lakn Hilo shitaka liliptia HAtua HAtua zote kisheria
 
Kama hvyooo hakun maamuz Ni dismiss kesi mkuu

Au uliwaloga wasikufanyie maamuz
 
Baada ya kikao hicho kilichosikiliza shauri na kutokutoa mapendekezo ya adhabu, baada ya wiki 3 kilikaa kikao kingine cha pili cha nidhamu ambacho kilikuwa na watu tofauti na wale wa kikao cha kwanza. Hiki kikao cha 2 cha nidhamu ndicho kikaja kutoa mapendekezo ya kufukuzwa kazi.
Lakini kikao hiki cha 2 hakikusikiliza shauri.
Je, hii ni sawa?
 
Mtu umekutwa na hatia bado tu unataka usifukuzwe?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom