Naomba ufafanuzi kuhusu kibali cha kujenga

  • Kibali cha ujenzi ni ubunifu wa kupata mapato kwa wizara husika.
  • Unachotakiwa kufanya peleka nakala ya michoro ya jengo lako pamoja na nakala ya umiliki wa eneo
  • kama ni jengo la kawaida haitazidi laki
Hatua hizi
1. Tafuta michoro ya Architectural drawing, site plan, floor plan, na elevation. Hakikisha kwenye site plan zile setback yaani distance kati ya mipaka wa kiwanja na Kuta za nyumba zisipungue angalau mita 2

2. Nenda kwa mtendaji wa eneo lako, utapewa form utaajaza baada ya hapo mtendaji atagonga muhuri wake, hapa hakikisha unaenda na hati ya kiwanja au mkataba wa mauziano

3. Ambatanisha hivyo hiyo michoro niliyorodhesha kwenye namba Moja pamoja na hizo form ulizojaziwa kwa mtendaji. Nenda halmashauri yako husika idara ya ardhi wakabidhi viambatanisho

4. Idara ya ardhi, Chini ya Engineer wao atapiga hesabu ya square mita katika Ile ramani kujua kiwango Cha Pesa unachotakiwa kulipa, Sam 1 Huwa ni around 800 hivi

5. Utajulishwa kiwango Cha Pesa unachotakiwa kulipa, utapewa control number ili ulipie. Baada ya malipo subiria kibali

** Sam zinazovyokuwa ndogo ndio utalipia kidogo, kama ramani yako ni kubwa sana basi Pesa nayo inakuwa kubwa.

Watu hufanya ujanja wakusubmit Raman ndogo ili alipe kidogo. Halafu anakuja kujenga Ile ramani kubwa. Hii ni kwa sehem ambazo hawafuatilii kile kilichopelekwa wilayani ndicho kinachojengwa site.
 
Kama unajenga banda la kuku au mifugo we jenga tu Achana na mavibali wezi tu hao.

lakini kama una jenga nyumba utakayoishi wewe au wateja wako utaowapangisha, Nyumba isiyopungua thamani ya 10m kupanda Juu

Sidhani kama kuna haja ya kujiingiza kwenye shida zinazoepukika,Lipia tu hicho kibali.

Hata wakikwambia ni 500k just pay it, Ndio ni wezi lakini tutafanyaje sasa ndio ushakubali Kuishi Tanzania nchi yako kuna vitu usiulize hata ilimradi ndio wenyewe wanakwambia "ni utaratibu wao" we Wape tu.

Ila ndio hivyo mazoea mazoe ya kuja kwako wambie hutaki,wakati mwingine haya ma vibali/kodi/ushuru/ tutoe tu ili tuoshi zetu kwa amani.

nchi lenyewe hili ni lakuishi bila DOA maana DOA 1 tu linaweza kuku cost maisha.
 
Asante mkuu lakini huko ni kupotezeana mda kwa mizunguko yote hiyo, si hivyo tu kila sehemu utakayo enda lazima uache kitu
 
Kama unajenga banda la kuku au mifugo we jenga tu Achana na mavibali wezi tu hao.

lakini kama una jenga nyumba utakayoishi wewe au wateja wako utaowapangisha, Nyumba isiyopungua thamani ya 10m kupanda Juu

Sidhani kama kuna haja ya kujiingiza kwenye shida zinazoepukika,Lipia tu hicho kibali.

Hata wakikwambia ni 500k just pay it, Ndio ni wezi lakini tutafanyaje sasa ndio ushakubali Kuishi Tanzania nchi yako kuna vitu usiulize hata ilimradi ndio wenyewe wanakwambia "ni utaratibu wao" we Wape tu.

Ila ndio hivyo mazoea mazoe ya kuja kwako wambie hutaki,wakati mwingine haya ma vibali/kodi/ushuru/ tutoe tu ili tuoshi zetu kwa amani.

nchi lenyewe hili ni lakuishi bila DOA maana DOA 1 tu linaweza kuku cost maisha.
Ni banda la kuku na vifaranga vyake, sema huku mikoani wametukazia sana
 
Mimi wamenistopisha Juzi kati hapa, Wilaya Kinondoni.Bado sijaenda kuwaona. Yaani wakikuta nyumba hata haijamaliziwa lakini anaishi mtu hawafanyi chochote.
 
Nami nimezuiwa na mtendaji hapa
Na kibali ninacho ila nilikipata 2019
Ila ujenzi ukaanza wiki mbili zilizopita
Mtendaji anasema kibali kimeisha
Sasa namuuliza niifanye nini ili kazi iendelee hasemi anakazania simamisha ujenzi
 
Inabidi ukaombe upya hua kinaexpire miez 6
 
Mi nimeomba kibali nikaona wananichelewesha nikaona isiwe tabu ngoja nianze zangu wakikitoa mi ntakua nimeshamaliza kupandisha boma labda
 
Haya mambo yanachanganya sana ...watu wengi nawafahamu wamejenga bila kibali

Sasa sijui mtu uchague lipi
Jenga na kibali itasaidia maana wakikuoa kibali wameshathibitisha eneo kwamba ni sahihi kwa makazi ya watu na hata ikitokea wanatak kuendeleza miji unalipwa fidia maana serekali ndo ilikupa kibali tofaut nakujeng holela
 
Hili ni la msingi zaidi

Thanks much mkuu
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom