Naomba ufafanuzi kuhusu hili la kuwapa watoto majina

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Wakuu, naomba kuelimishwa katika hili la majina! Natamani kufahamu yafuatayo:

1. Mtoto anaweza kutumia jina la mama yake kwenye utambulisho wa majina yake? Mfano, kama mtoto anaitwa Bakari na mama yake anaitwa Amina, anaweza kusajiliwa kama Bakari Amina?

2. Mwanamke kuwa na majina mawili ya kike ni utamaduni wa wapi? Aliyekuwa mke wa marehemu Dr. Reginald Mengi aliitwa Mercy Anna Mengi. Naona majina mawili ya mwanzo, kulingana na uelewa wangu, ni ya kike.

Jina "Anna" kama lilivyotumika hapo ni la kwake au la mama yake au la baba yake? Inaonekana ni jina la kike.

Kwa uelewa wa wengi, mimi nikiwemo, jina la baba ndilo linalopaswa kuwemo kwenye utambulisho wa jina la mtoto. Ilikuwaje kwa mama Mercy Anna Mengi? Anna ni jina la kiume?

Ikiwa jina la pili la mtu si la baba yake, kama ilivyokuwa kwa mama Mercy Anna Mengi, akitakiwa kujaza nyaraka zenye vipengele vya kujaza jina la baba, labda yeye anaitwa Mercy Anna Mengi na baba yake anaitwa Joshua Ally (mfano tu), haitaleta utata wa Kisheria? Uhusiano wao hautatiliwa mashaka, kwamba huenda si mtu na mtoto wake?

3. Inawezekanaje mtu kutokutumia kabisa jina la baba yake kwenye utambulisho wa majina yake? Utamaduni huo chimbuko lake ni wapi?

Baadhi ya watu wenye majina ambayo hayataji majina ya baba zao ni pamoja na:

1. Mtoto wa marehemu Dr. Raginald Abraham Mengi, marehemu Rodney Mutie Mengi. Jina la baba yake, Reginald, halijajumuishwa kwenye utambulisho wa majina yake. Baba yake aliitwa Reginald Abraham Mengi na mtoto aliitwa Rodney Mutie Mengi.

2. Watoto wa Yoweri Kaguta Museveni:
(A). Muhoozi Kainerugaba
Jina la baba yake halijatajwa kabisa.

(B). Natasha Museveni Karugire

(C). Patience Museveni Rwabwogo

(D). Diana Museveni Kamuntu

Naomba mwenye uelewa wa hayo mambo anisaidie🙏
 
Utakavyoandikisha shule ndo hivyo, enzi zetu walimu wametumika kutubalisha majina sana n kama mzazi ndo hajapata wazo ndo basi tena ukija stuka mtoto ashafanya mtihani wa Taifa tayari

Ila pia mtu kuwa na majina mawili au namna ya uitaji wa majina ni vile watakavyopenda wazazi kumuandikisha
 
🙏
 
Ni uamuzi tu mkuu kwa mfano Mimi jina langu halisi naitwa Marwa Mahende ila kwenye Cheti nàitwa Emmanuel John
Papo hapo mkuu🙏

Fikiri mtu anaitwa Juma James Rashidi! Anaweza kumpa mwanaye jina lisilokuwa lake au la ukoo wake? Kwamba, jina la pili na la tatu yakawa ni ya kutungwa tu, kwa maana kwamba hayapo kwenye ukoo wake?

Kama Juma James Rashi ana mtoto aitwaye Robert, itatarajiwa aitwe Robert Juma James au Robert Juma Rashidi. Babaye anaweza kuamua kumpa majina tofauti na hayo, kwamba aitwe Robert Bosco Sr? Akifanya hivyo hakutaleta mkanganyiko wa Kisheria hasa kwenye cheti cha kuzaliwa?

Ufafanuzi kidogo mkuu, tafadhali🙏
 
Wakuu, naomba kuelimishwa katika hili la majina! Natamani kufahamu yafuatayo:

1. Mtoto anaweza kutumia jina la mama yake kwenye utambulisho wa majina yake? Mfano, kama mtoto anaitwa Bakari na mama yake anaitwa Amina, anaweza kusajiliwa kama Bakari Amina?

2. Mwanamke kuwa na majina mawili ya kike ni utamaduni wa wapi? Aliyekuwa mke wa marehemu Dr. Reginald Mengi aliitwa Mercy Anna Mengi. Naona majina mawili ya mwanzo, kulingana na uelewa wangu, ni ya kike.

Jina "Anna" kama lilivyotumika hapo ni la kwake au la mama yake au la baba yake? Inaonekana ni jina la kike.

Kwa uelewa wa wengi, mimi nikiwemo, jina la baba ndilo linalopaswa kuwemo kwenye utambulisho wa jina la mtoto. Ilikuwaje kwa mama Mercy Anna Mengi? Anna ni jina la kiume?

Ikiwa jina la pili la mtu si la baba yake, kama ilivyokuwa kwa mama Mercy Anna Mengi, akitakiwa kujaza nyaraka zenye vipengele vya kujaza jina la baba, labda yeye anaitwa Mercy Anna Mengi na baba yake anaitwa Joshua Ally (mfano tu), haitaleta utata wa Kisheria? Uhusiano wao hautatiliwa mashaka, kwamba huenda si mtu na mtoto wake?

3. Inawezekanaje mtu kutokutumia kabisa jina la baba yake kwenye utambulisho wa majina yake? Utamaduni huo chimbuko lake ni wapi?

Baadhi ya watu wenye majina ambayo hayataji majina ya baba zao ni pamoja na:

1. Mtoto wa marehemu Dr. Raginald Abraham Mengi, marehemu Rodney Mutie Mengi. Jina la baba yake, Reginald, halijajumuishwa kwenye utambulisho wa majina yake. Baba yake aliitwa Reginald Abraham Mengi na mtoto aliitwa Rodney Mutie Mengi.

2. Watoto wa Yoweri Kaguta Museveni:
(A). Muhoozi Kainerugaba
Jina la baba yake halijatajwa kabisa.

(B). Natasha Museveni Karugire

(C). Patience Museveni Rwabwogo

(D). Diana Museveni Kamuntu

Naomba mwenye uelewa wa hayo mambo anisaidie🙏
Au labda Asha Rose Migiro, huyu Rose ni nani?
 
Nafikiri Asha na Rose ni mtu huyo huyo. Migiro ndilo jina la mzazi/ukoo n.k.

"Nahisi" mwanzoni alikuwa akiitwa Rose na baadaye alipobadili dini akalirekebisha jina kwa kuongeza na Asha. Kwa hiyo jina lake limebeba la Kiislamu na la Kikristo.

Sijui kama mimepatia😀.

Maelezo hayo ni kwa mujibu wa simulizi niliyokutana nayo siku za nyuma alipokuwa UN.
 
Back
Top Bottom