Ipi sahihi: "dawa ya mbu" au "dawa ya kuulia mbu"?
Dada aliyeko nyuma ya counter ya pharmacy aliniudhi siku moja aliporekebisha kiswahili changu. Hata hivyo baada ya muda niligundua kuwa mimi ndiye nimekosea.
Kuna kosa lolote mtu akisema "dawa ya mswaki"?
1. Nadhani 'dawa ya mbu' ni sahihi zaidi kwa mazungumzo ya kijumla. Si dawa zote za mbu ni kwa ajili ya kuua, kuna nyingine ni kwa ajili ya 'kuwafukuza' tu (kama zile za kuchoma (coil) haziui bali zinafukuza tu!). Hata hivyo kama unataka dawa kwa ajili ya kuua mbu (na si kufukuza tu), nadhani ni sahihi na vema ukasema "dawa ya kuulia mbu" (ili upewe 'rungu', 'expel' nk).
2. 'Dawa ya mswaki': Kama tunazungumzia vitu kama Colgate, Whitedent, Aquafresh nk, nadhani halijakaa sawasawa. Pengine 'dawa ya (kusafishia!) meno' inaweza kuwa sahihi zaidi. Binafsi nikienda dukani hupendelea kutaja jina (brand name) la hiyo bidhaa.
Ni vema tukumbuke kuwa neno 'dawa' (pamoja na mengineyo) linapata maana kutegemea na muktadha pamoja na lengo la mzungumzaji:
Dawa = kinga (mf: dawa ya polio)
Dawa = tiba, -ya kutibu (Mf: dawa ya malaria)
Dawa = kemikali (mf: dawa ya kusafishia meno, dawa ya 'salfa' nk)
Dawa = sumu, -enye madhara (mf: dawa za kulevya, dawa ya mbu nk)
Dawa = suluhisho, jibu (Mf: 'Ukubwa dawa')
Ni hayo tu kwa sasa.