Naomba ufafanuzi katika hili(dawa/sumu) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba ufafanuzi katika hili(dawa/sumu)

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by KiuyaJibu, Mar 16, 2009.

 1. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Nimekuwa na pata wakati mgumu kukubali au kukataa katika utumiaji wa maneno/sentensi ifuatayo, "Naomba unipatie dawa ya mbu."Hii inatumika sana pale mtu anapofika dukani/supermarket kununua hii bidhaa.
  Kwasababu ninavyojua mimi dawa ni kwaajili ya tiba/matibabu kutokana na maradhi yaliyokupata;sumu,ni kwaajili ya kuangamiza/kuua kiumbe asiyestahili/kisichostahili kuishi hapa duniani.
  Sasa ukisema upatiwe dawa ya mbu ni kweli inakuwa ni kauli sahihi?Cha ajabu watengenezaji na wauzaji wanatumia kauli hiyo bila hata aibu!Wakati ningetegemea wao ndiyo wangekuwa mstari wa mbele kutuweka sawa.Inashangaza kuona kama kuna mtu anadiriki kufuga mbu wakati tunajua madhara yake.
  Anyway,ningependa kufahamu ipi ni kauli sahihi.
   
 2. Nyikanavome

  Nyikanavome JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Mimi sio mwana taaluma katika fani ya lugha ya kiswahili lakini naweza kukupa ufafanuzi ufuatao kuhusu suala lako. Dawa nyingi ni sumu kwa mdudu anayekusudiwa ikiwa ina tumika kwa kiwango kinacho kubalika. mfano unapokunywa dawa ya maleria, kwa binadamu ni dawa lakini kwa vimelea vya maleria ni sumu. Hiyo hiyo dawa ya maleria ikizidishwa dozi inakuwa sumu kwa binadamu. Kwa mtizamo huo ni kuwa dawa zote ni sumu lakini sio sumu zote ni dawa. Kwa muktadha wa dawa ya kuulia mbu, tuna iita dawa kwa vile inamwondolea binadamu bughtha ya mbu. Hapa tunamweka mbu katika kundi moja na vimelea vya maleria. Kwa maoni yangu ni kuwa matumizi ya neno Dawa ya mbu au sumu ya mbu yote yako sawa, inategemea mtizamo wa mzungumzaji kuhusu maana ya sumu na dawa.
   
 3. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Nyikanavome, asante sana umetufafanulia vizuri, sikuwa naelewa hilo.
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Nyikanavome

  Asante kwa ufafanuzi wako.

  Kwa kuwa mada ipo kwenye jukwaa la lugha, si vibaya nikirekebisha yafuatayo:

  Maleria = Malaria (Ni neno la kukopa kutoka kiitaliano, halijatoholewa!)
  Bughtha = Bugudha
   
 5. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Kimsingi hakuna tofauti kati ya sumu na dawa la kutibu ni swali la kiwango.
  Mwili wetu unahitaji chumvi (tunakufa tukikosa chumvi kabisa) lakini inawezekana kumwua mtu kwa chumvi yaani kiasi kikubwa mno. Aspirin ni dawa zuri la kukomesha maumivu lakini yatumiwa pia na watu wanotaka kujiua. Mifano ni mingi.

  Ni dutu chache tu ambayo ni kama sumu pekee kwa sababu haziko kabisa katika mazingira yetu. Mtaalamu wa kale Paracelsus alisema tayari: "Dosis sola facit venenum" - ni kiasi pekee kinachofanya sumu.
   
 6. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Nyongeza: je si pia ya kwamba neno "dawa" latumiwa karibu sawa na "kemikali" zikiathiri watu au wanyama yaani viumbehai?

  Yaani sumu sharti ni kitu kinacholeta hasara (angalau kwa mbu) lakini "dawa" linaweza kuwa na pande mbili inategemea.
   
 7. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ipi sahihi: "dawa ya mbu" au "dawa ya kuulia mbu"?

  Dada aliyeko nyuma ya counter ya pharmacy aliniudhi siku moja aliporekebisha kiswahili changu. Hata hivyo baada ya muda niligundua kuwa mimi ndiye nimekosea.
  Kuna kosa lolote mtu akisema "dawa ya mswaki"?
   
 8. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280

  1. Nadhani 'dawa ya mbu' ni sahihi zaidi kwa mazungumzo ya kijumla. Si dawa zote za mbu ni kwa ajili ya kuua, kuna nyingine ni kwa ajili ya 'kuwafukuza' tu (kama zile za kuchoma (coil) haziui bali zinafukuza tu!). Hata hivyo kama unataka dawa kwa ajili ya kuua mbu (na si kufukuza tu), nadhani ni sahihi na vema ukasema "dawa ya kuulia mbu" (ili upewe 'rungu', 'expel' nk).

  2. 'Dawa ya mswaki': Kama tunazungumzia vitu kama Colgate, Whitedent, Aquafresh nk, nadhani halijakaa sawasawa. Pengine 'dawa ya (kusafishia!) meno' inaweza kuwa sahihi zaidi. Binafsi nikienda dukani hupendelea kutaja jina (brand name) la hiyo bidhaa.

  Ni vema tukumbuke kuwa neno 'dawa' (pamoja na mengineyo) linapata maana kutegemea na muktadha pamoja na lengo la mzungumzaji:

  Dawa = kinga (mf: dawa ya polio)
  Dawa = tiba, -ya kutibu (Mf: dawa ya malaria)
  Dawa = kemikali (mf: dawa ya kusafishia meno, dawa ya 'salfa' nk)
  Dawa = sumu, -enye madhara (mf: dawa za kulevya, dawa ya mbu nk)
  Dawa = suluhisho, jibu (Mf: 'Ukubwa dawa')

  Ni hayo tu kwa sasa.
   
Loading...