Naomba ufafanuzi juu ya kifaa cha microchip

Hamjambo ? Naombeni kujua kiundani kifaa hiki ni kweli kinarelate to Illuminati numbers 666 ?
Nimeona Wamarekani wameanza kuweka kifaa hicho mkononi , wao wanadai ni kama mastercard kuna ukweli wowote ?
Wanatupeleka 666 lazima itimie
 
Let me try to explain to you.
Katika historia ya ugunduzi wa kompyuta ilipitia generation mbalimbali kwa mfano. Computer za mwanzo kabisa zilikuwa kubwa sana na zilikuwa hazitumii microchip bali zilikuwa zinatumia vacuum tube. Ugunduzi wa microchip (microprocessor) uliwezesha computer kuweza kuwa na spidi na uwezo mkubwa lakini pia kupungua sana umbo hapo utapata laptop, desktop, au smartphone.
Microchip ni nini?
Microchip ndio hii tunaita processor au CPU ni kifaa flani kama kibanzi ambacho hu tumika kuendesha mifumo yote ya computer. Neno micro limetumika kuonyesha udogo wake, pia microchip zaweza kutumika sehemu mbalimbali mfano viwandani kupitia maroboti au kwenye satellite
 
Hamjambo ? Naombeni kujua kiundani kifaa hiki ni kweli kinarelate to Illuminati numbers 666 ?
Nimeona Wamarekani wameanza kuweka kifaa hicho mkononi , wao wanadai ni kama mastercard kuna ukweli wowote ?
.....ndio baadae kutakuwa hamna pesa yaani hizi coins na notes na tutakuwa na sarafu moja duniani na zitakuwa kwenye mfumo wa electronic, pamoja na taarifa zako zote so, hutahitaji kubeba cheti cha kuzaliwa au kadi ya benki wala passport kila kitu kitakuwa huko kwenye hiyo microchip.....then.....ndio ile kilio na kusaga meno
 
Let me try to explain to you.
Katika historia ya ugunduzi wa kompyuta ilipitia generation mbalimbali kwa mfano. Computer za mwanzo kabisa zilikuwa kubwa sana na zilikuwa hazitumii microchip bali zilikuwa zinatumia vacuum tube. Ugunduzi wa microchip (microprocessor) uliwezesha computer kuweza kuwa na spidi na uwezo mkubwa lakini pia kupungua sana umbo hapo utapata laptop, desktop, au smartphone.
Microchip ni nini?
Microchip ndio hii tunaita processor au CPU ni kifaa flani kama kibanzi ambacho hu tumika kuendesha mifumo yote ya computer. Neno micro limetumika kuonyesha udogo wake, pia microchip zaweza kutumika sehemu mbalimbali mfano viwandani kupitia maroboti au kwenye satellite
Ingia Google search Microchip, utagundua hilo ni kampuni linalotengeneza microcontroller zinazoitwa PIC zinatumika kwenye embedded systems!
Unachanganya microchip Na microprocessor
 
Ingia Google search Microchip, utagundua hilo ni kampuni linalotengeneza microcontroller zinazoitwa PIC zinatumika kwenye embedded systems!
Unachanganya microchip Na microprocessor
Microchip ndio hio integrated circuit na processor pia ni microchip sema zenyewe ni general purpose circuits tofauti na hizo ambazo ni emneded kwenye vitu kama remote nk ambazo zipo specific, kampuni unayoisema inaitwa microchip technology, na sio microchip Bali microchip ni neno ambalo linamaanisha integrated circuit.
 
Neno lenyewe linasadifu maana

Microchip

Micro -ndogo
Chip-kikadi kidogo kinachohifadhi taarifa.

Kwahiyo microchip ni kadi ndogo maalum ambayo imetengenezwa kwa ajili ya kuhifadhi data za mhusika.

Matumizi hapo ndo itategemea

Ya kifedha
Ki intelligencia
Na mengineyo.

Ushawahi jiuliza zile simcard unazokata kufit kwenye smartphone zinaitwaje
 
Wote nimewaelewa ..ila nimeomba ufafanuzi kujua juu ya kifaa hicho kama kinarelate na ile chapa iliyoandikwa kwenye biblia na msaafu ,ya anti christ yaani 666 nimeona barcode 666 na kinawekwa mkononi au katika paji la uso....IS IT TRUE NI MAMBO YA NEW WORLD ORDER ???
 
y

Mkuu Eiyer kesho imefika tunakusubiria au hakujawa majaliwa?
Well...

Nilikuwa nimebanwa kiaina wakuu...

Iko namna hii,kwa namna nijuavyo na kwa mujibu wa utafiti ambao nimeufanya na ninaoendelea kuufanya kuhusu chapa ya mnyama na hii microchip ni kwamba mambo haya yanaweza kuhusiana lakini hayafanani au kwa lugha nyingine microchip siyo ile chapa iliyoandikwa kwenye ufunuo 13 ambayo ni 666 kwasababu zifuatazo...

1;Huwezi kuwa na chapa hii bila ya kuwa na mhusika ambaye ni mnyama [ufalme/mfalme] hivyo dhana kuwa microchip iliyopo ambayo watu wanawekewa kuwa ni hiyo chapa siyo sahihi maana maandiko yanazungumza vizuri tu namna itakavyokuwa....

2;Chapa iliyoandiokwa kwenye Ufunuo 13 siyo kifaa bali ni hesabu ya jina,tunachopaswa kujua ni kwamba hapo inazungumzwa habari ya jina na hesabu ya jina lake siyo kifaa chochote.Watu,kwa maana ya maandiko matakatifu ya Ufunuo 13:16-18 watapigwa chapa kwenye mapaji ya uso na kwenye mikono yao ya kuume na kuwatambulisha kuwa wao wamekubaliana na kile ambacho mnyama wa pili [Ufunuo 13:11-15] anakifanya kwa niaba ya mnyama wa kwanza [Ufunuo 13:1] kwa maana hiyo hapa tutakuwa na wanyama wawili lakini jina ambalo chapa yake ni 666 ni la mnyama wa kwanza,huyu wa pili atakuja kufanikisha upigwaji wa chapa hii.....

Kwa maana hii hutaweza kuona chapa hii yenye hesabu ya jina la mnyama kabla hujamjua mnyama mwenyewe.Mnyama anayezungumzwa hapo kwenye Ufuno 13:1-3 sijamuona na kwa maoni yangu bado hajakuwepo duniani,sasa utakuwaje na chapa kabla ya mhusika kuwepo?

Maandiko yanasema kuwa mnyama huyo atakuja kwanza kisha atakuja mwingine ambaye atafanikisha hilo zoezi,sasa yote haya yametokea wapi?

Inawezekana hii microchip ni aina ya maandalizi ya chapa hiyo kwa namna moja au nyingine lakini bado hatuwezi kusema hiyo ndiyo chapa yenyewe.Pia,inawezekana kifaa hiki kikaja kusaidia upigwaji wa chapa hii lakini kwa sasa hatuwezi kusema chenyewe ndiyo 666....

ONYO: Usikurupuke kukubali kitu usichojua malengo yake hasa kwa dunia hii ya sasa,tumia muda wako kufanya utafiti kabla hujakubali maana unaweza kujikuta kwenye wakati mbaya sana hapo baadaye....

Ahsanteni....
 
Mkuu Eiyer yawezekana wengi hatuelewi kwa haya mambo ya microchip na namba 666 ndio maana tumekuwa waamini wa kile tunachopotoshwa.

Sasa nimekuelewa!
 
Back
Top Bottom