Yumbayumba
JF-Expert Member
- May 31, 2012
- 1,240
- 850
Mrejesho: Baada ya kuwasiliana naye,kasema kabla hajaomba msaada kwangu,alikuwa tayari kaonyeshwa eneo la ekari 8 alinunue. Amesita kulinunua kwa vile hajajishauri vya kutosha alime au afuge! Aliambiwa bei ni 5 M. Na ameona bora apate ushauri wa kutosha kabla. Hii ina maana yuko tayari kupokea ushauri wako!
Hilo shamba lipo wapi? Linafaa kulimwa mazao gani? Kuwa ekari 8 na kuuzwa mil 5 sio tatizo
Maana kwenye kilimo tunazingatia shamba lipo wapi mfano mkoa gani, hapo tutajua hali ya hewa ya mkoa husika na ili kujua linafaa kwa zao gani
pia tunazingatia unataka kulima nini, hapo tutaangalia zao unalotaka kulima na udongo uliopo shambani kwako vinaendana?
Tutaangalia upatikanaji wa maji nk
Bei pekee isiwe kigezo cha kununua au kutonunua shamba kwa uchache mwambie azingatie hayo niliyomwambia