Naomba tupeane ushauri wa jumla kilimo vs ufugaji

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
4,006
3,643
Nina rafiki yangu amestaafu utumishi wa Umma. Anataka afanye investment katika kilimo au ufugaji. Ameniomba ushauri kumchagulia awekeze wapi?
Kwa vile jukwaa hili ni la ushauri,naye siyo mwanachama,naombeni ushauri kulingana na hali halisi iliyopo sasa.
 
Inategemea na mahali alipo, mtaji alionao, interests nk
Asante. Kaniambia anataka aanze na 20 M. Yuko interested na vyote,ila alitaka afanye kimoja tu kati ya kilimo au ufugaji. Anaishi Morogoro kama Km 10 nje ya mji.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Ufugaji au ukulima unataka eneo kwanza. Anatakiwa ajue anataka kufanya shughuli hiyo katika ukubwa gani? Sio kusema tuu 20m mtaji huku hajui kwa level gani anayotaka. Kama amestaafu kiserikali nazan atakuwa na zaidi ya 55years. Hebu akupe taarifa zilizoshiba harafu uje tena.
 
Ana afya njema tuu. Kastaafu kwa hiari at 55. Na anao mtaji nilioutaja. Hayuko decided afanye kilimo au ufugaji! Kwa nia ya kumsaidia,ajielekeze wapi,na ikibidi unaweza kumpa mchanganuo wa utakachomshauri. Asante.
 
Sasa kama ana 55 hadi Leo hana hata eka 5. Kijana hebu mwambie anunue kwanza shamba la eka 10 hapa Moro akipata anitafte nimpe somo la ufugaji.
Yawezekana ndiyo maana hataki kufanya makosa ya nyuma kwa kuomba ushauri. Ameona ameingia kwenye fainali,asifanye masihara. Ninashukuru kwa ushauri. Nitamjulisha,nakupa feedback karibuni. Thanks.
 
Sasa kama ana 55 hadi Leo hana hata eka 5. Kijana hebu mwambie anunue kwanza shamba la eka 10 hapa Moro akipata anitafte nimpe somo la ufugaji.
Mrejesho: Baada ya kuwasiliana naye,kasema kabla hajaomba msaada kwangu,alikuwa tayari kaonyeshwa eneo la ekari 8 alinunue. Amesita kulinunua kwa vile hajajishauri vya kutosha alime au afuge! Aliambiwa bei ni 5 M. Na ameona bora apate ushauri wa kutosha kabla. Hii ina maana yuko tayari kupokea ushauri wako!
 
Back
Top Bottom